Dkt. Bashiru Ally, Mjamaa aliyeshindwa kutuonesha ujamaa kwenye Uchaguzi

Mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM ilikuwa ni rushwa tupu.
Leo wamepitisha watu corrupt kugombea ubunge na kisha wakawashindisha kinguvu bila ridhaa ya wananchi.
Kiufupi wametuletea bunge corrupt.
Bunge la namna hii haliwezi kuithibiti serikali katika issue za ubadhirifu wa pesa za wananchi au ufisadi, maana vitu hivyo ndiyo nature yao haswaa!
Umewahi kuona wapi shetani akimtoa shetani mwenzie?
Dawa yao itakuja kuwarudia wenyewe na Miaka mitano hii watakata mpaka mishahara yao kuleta maendeleo nchi nzima mana hakuna atakayetaka kuona miradi ikizinduliwa ukanda mmoja tu kila siku kwenye maTV huku jimbo lake likikosa hata barabara ya lami daraja la tatu.

Wamebugi na wataiua CCM muda sio mrefu. Damu za watu hazishangiliwi zikimwagika. Polepole ,Bashiru na Musiba na Kheri wanashangilia wanapoona damu za binadamu wenzao zikimwagwa kwa sababu tu ya tofauti za kisiasa.
Hivi mtu akipinga jambo anampunguzia nini Waziri au Rais au mbunge wa jimbo lingine anayeumgwa mkono na wengine?
Kwa nini auawe kwa sababu ya kupinga tu ?
Bashiru ,Polepole n,Kheri na Musiba wawekwe kwenye kumbukumbu mbaya na watangazwe kama nduli IDDI AMINI kwa vizazi vijavyo ambavyo havitapenda kamwe kuona damu za marafiki zao ,ndugu zao ,waafrika wenzao na jamaa zao wakiuawa na kutesa bila sababu.
 
Nadhani kama hujanilewa nilivyoeleza kuhusu Economic Planning and Command Economy kwa nchi za kikomunisti sidhani kama hata nikitembea kichwa chini miguu juu utanielewa. Lakini kama ulivyosema It's not rocket science basi wafuate waliosomea uchumi wa ujamaa Shivji na Bashiru halafu waambie wakueleze dhana nzima za Base and / Superstructure/Economic Planning and Command Economy.

Nilihisi unafahamu vizuri lakini kumbe na wewe una shida kubwa pahala kuhusu uelewa wa baadhi ya mambo. Ngoja nikuoneshe umufulisi wa hoja yako hii kitaalamu. Usiponielewa hapa basi hata malaika ashuke hutakaa unielewe na sintakuwa na muda wa kubishana na wewe:

Mosi, unapoiangalia Keynesian Economic Model kwa jicho la Economic Stimulus Packages bila kuangalia mambo mengine kama Tax Cuts & Tax Rebates na Government Spending nadhani utakuwa na parcohial understanding of the world. Unaponiambia kwamba tangu kipindi cha Nixon nchi ya Marekani hawajafanya matumizi yoyote kwenye miondombinu napata ukakasi sana na jinsi unavyoelewa mambo: Ronald Reagan alifanya massive Tax Cuts. Kuhusu miradi nakushauri fanya tafiti tena, kuna miradi mikubwa sana imefanyika nchini Marekani.

Pili, umenishangaza sana uliposema kwamba matumizi ya jeshi huwa hayahesabiki kwenye uchumi na kuendelea kukomaa kwamba Stimulus Packages pekee ndiyo kanuni pekee ya Keynesian Economic Model. Wachumi wakubwa duniani kama Professor Stanley Fischer wanasema matumizi ya jeshi ni muhimu sana katika kupima na kuangalia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mashirika makubwa kama Goldman Sachs na The Institute of Strategic Studies kwenye chapisho lao liitwalo The Military Balance wameenda mbali zaidi na kusema siku hizi wanatumia PPP (Purchasing Power Parity) kama ndiyo benchmark ya kupimia Uchumi wa taifa kuliko kutumia GNP na GDP: Ukitumia hii njia basi ni lazima uzingatiea matumizi ya kijeshi ambayo wewe ndugu yangu bwana Mwanzi umekanusha. Mchumi kwanini unashindwa kuelewa hili jambo rahisi kabisa ???

Tatu, wewe siyo mtu mkweli au aidha huelewi nilichokisema: Tanzania hatuna Progressive Tax tuna Proportional Tax.
Makundi yote hulipa asilimia moja ya pesa katika vipato vyao, kama ipo hebu tupe mifano. Uchina ukiwa tajiri na kodi inaanza kuwa Progressive. Kafanye tafiti zaidi au kama unataka tuanze kuongelea kodi basi fungua uzi mwingine.

Mimi nikajua kwamba nazungumza na mtu mwenye elewa wa mambo kumbe I'm just laboring in futility. Hivi malipo ya Tsh 20,000 ya vitambulisho vya machinga nayo ni kodi ??? Kama ni kodi basi naomba unitajie basi ni kodi ya aina gani na iko kwa mijali ya sheria ipi.

Hiyo takwimu ya ruzuku ya dola za Kimarekani Trillioni moja umeitoa wapi na imetolewa lini na serikali ya Marekani ?
Hizo ruzuku za zinazotolewa na umoja wa Ulaya zinatolewa kwenye sekta zipi ???
Je, WTO Rules zinaruhusu utoaji wa ruzuku ???

Basi kama hii ndiyo hoja yako, basi kila nchi duniani ni Mixed Economy na ulikuwa huna haja ya kuniuliza swali kama hili kwasababu It wouldn't have made any diffference, considering that aspects of private and public enterprise are in sync and prevalent in almost all global economies.
Ni kweli na wala hujakosea, wengine sisi ni mbumbu ambao hatuna hadhi ya kuhoji mambo mazito kama haya. Marehemu Steve Jobs alisema maneno mazuri sana na sintayasahau ...STAY HUNGRY, STAY FOOLISH.

Mkuu, post yangu ya nyuma nimejirkeza kadiri ya uwezo wangu kwamba Marekani ikiachana na mfumo Keynesian tangia enzi za Nixon 70's. Rais ambaye aliyetaka kuufufua huo mfumo alikuwa Obama, lakini na yeye alipata shida kutoka na upande wa Republican kutaka pesa itumike kuokowa mabenki na capital investments na huku yeye Obama akitaka kusaidia watu wa kawaida aliopoteza kazi na wengine kushindwa kulipa mikopo ya nyumba nk. Kwenye kipengele hicho hicho nimesema mfumo Keynesian unadokolewa kidogo kidogo na rais aliye madarakani ili kuepusha uchumi kuyumba. Hapo ndio unaposema tax cut, lakini hiyo sio sababu ya kusema Marekani inatumia mfumo huu kuendesha uchumi wao wa kila siku au kila mwaka. Kama hivyo ni kweli, Biden anapanga kupandisha kodi na Trump amepunguza ruziki kwenda kwa wakulima na sekta zingine 2020, je na hapa bado kuna huo mfumo bado upo? Na kwa nini watumie huo mfumo wakati uchumi ulikuwa unaajiendesha wenyewe (pre Covid)?

Humu JF Kuna watanzania wanaishi Marekani, ladba watowe ushuhuda kama infrastructure ya Marekani bado iko up to world stand au ndio mguu mmoja unachungulia kwenye kaburi. Tokea miaka ya 70, mimi sijaona uwekezaji mkubwa kama kwenye reli mpya, treni mpya super highway mpya. Ukilinganisha na nchi ndogo za Asia, Marekani wamejisahau kabisa kwenye nyanja ya miundo mbinu. Trump alijitutumua na msemo wake wa America First, akaahidi atafanya maajabu ya kurudisha viwanda, kujenga viwanda vipya, na hata kujenga reli nchi nzima. Mwaka wa nne huu, hata reliable 5G infrastructure ni shida. Hata Tanzania tumewashinda, tukichukulia ukubwa wa nchi yetu pamoja na ukubwa wa uchumi wetu, ndani ya miaka mitano tumeweza kuanzisha na kuendeleza major infrastructure projects tatu na zingine ziko kwenye pipelene.

Labda niseme tena, military spending can not and will not stimulate economy. Swali moja la kujiuliza kwani wanaojihusisha na jeshi (iwe kampuni binafsi za supply au hata wanajeshi wenyewe) wako wangapi? How can you compare agricultural spending with military spending in terms of value of return. Infact, kila $ inayokwenda kwenye matumizi ya kijeshi, ni pesa iliyopokonywa kutoka miradi mingine ya maendeleo ambayo ingeweza kuleta chachu kwenye uchumi.

https://www.investopedia.com/articles/investing/072115/how-military-spending-affects-economy.asp

Haya mambo ya kutumia PPP vs GDP kulinganisha pesa ya nchi moja kwa nyingine ndio kujuwa uchumi wa nchi unafananaje, ni maswali yenye utata mwingi. Nchi nyingi viwango vyao vya thamani ya pesa inashuka kulinganisha na walivyokuwa wanatumia zamani GDP. Kuna report inaonyesha Marekani hawajapishana sana na China kama walitumia PPP.

Hii hapa ni kauli yako:
Tatu, wewe siyo mtu mkweli au aidha huelewi nilichokisema: Tanzania hatuna Progressive Tax tuna Proportional Tax.

Makundi yote hulipa asilimia moja ya pesa katika vipato vyao, kama ipo hebu tupe mifano. Uchina ukiwa tajiri na kodi inaanza kuwa Progressive. Kafanye tafiti zaidi au kama unataka tuanze kuongelea kodi basi fungua uzi mwingine.

Sasa kama hatuna progressive tax, rate ya 9% to 30% inatoka wapi na nani anatakiwa kuilipa? Ukimuuliza Google kama Tanzania ina tumia progressive tax, atatoa majibu ya haraka sana.

Umeniuliza ruzuku ya Marekani ya trilioni moja nimeitoa wapi, jibu ni bajeti ya Marekani ya mwaka 2019 iko wazi kabisa.

Imeulizwa kama subsidies za US haziingiliani na masharti ya WTO....

Unafikiri kwanini USA wanamkataa yule mama MNigeria Ngozi asuchukuwe ukurugenzi wa WTO? America will protect America.
 
Kukurekebisha tu, kitambulisho cha wamachinga siyo kodi, wenyewe waliovitngeneza walidai eti hiyo ni "gharama za kuvichapisha tu", kiufupi ni mradi wenye maswali mengi kuliko majibu!
Mazee, kunradhi nilishindwa kujibu kwa wakati, kazi ndio tatizo. Wengine wiki yetu inaazia jumamosi

Hivi vitambulisho kwa sasa watu wanaviona kama sio kodi, lakini kwa sasa viko kama Pilot Scheme. Ni idea mpya na kitu ambacho hakijawahi kujaribiwa popote pale duniani, Tanzania ndio nchi ya kwanza kujaribu kutafuta suluhishi la wafanyabishara wasio rasmi. Mwaka sasa data zimekusanywa na mapokezi ya vitambulisho yamekuwa mazuri. Phase two, kurasimisha kama ni bunge au presidential decree, kuboresha vitambulisho vyenyewe viweze kubenda taarifa za ziada fursa ya kupata mikopo nafuu, au mafunzo kwa bei nafuu, au hata afya kwa bei nafuu. Jukumu lako kama mtumiaji ni nini, ni kulipa kila mwaka 20,000 na hiyo inakuwezesha kufanya biashara ndogo ndogo popote pale nchini. 20,000 inakwenda wapi? Hazina, kama sio kodi ni nini?
 
Pilot scheme huwa ni small scale, huwa haiwi rolled nchi nzima tena kwa vitisho vya wakuu wa wilaya, mkoa, wakurugenzi etc.

Wewe unasema ni kodi, Magufuli wakati anavizindua alisema anavitoa bure ila tu hiyo 20000 ni ya kurudisha gharama ya kuvitengeneza!.

Sasa hapo kuna mawili mmoja kati yako au Magufuli ni muongo. Kama hiyo 20000 ni kodi kwa nini wakati anavizindua aviite ni bure!. Na kama ni kodi aliianzisha hiyo kodi kwa mamlaka yapi, maana kisheria kodi inawekwa na bunge au serikali za mitaa!.

Hivyo vitambulisho vilichapwa na nani kwa procurement ipi iliyotangazwa na serikali?

Waseme tu kuwa buku 20 za wamachinga wamezichikichia, hakuna cha hazina wala nini!. Kama Magufuli alisema buku 20 ni hela za kurudisha gharama za kuvitengeneza basi hizo peza haziwezi kwenda kwenye account za TRA, maana TRA hawakusanyi peza zisizo za kikodi!. Kwa hiyo hatujui hizo pesa zimeingia kwenye account ipi, na hatujui huyo aliyebichapa alivichapa kwa gharama gani halisi!
 
Ni kweli na wala hujakosea, wengine sisi ni mbumbu ambao hatuna hadhi ya kuhoji mambo mazito kama haya. Marehemu Steve Jobs alisema maneno mazuri sana na sintayasahau ...STAY HUNGRY, STAY FOOLISH.

Mkuu, post yangu ya nyuma nimejirkeza kadiri ya uwezo wangu kwamba Marekani ikiachana na mfumo Keynesian tangia enzi za Nixon 70's. Rais ambaye aliyetaka kuufufua huo mfumo alikuwa Obama, lakini na yeye alipata shida kutoka na upande wa Republican kutaka pesa itumike kuokowa mabenki na capital investments na huku yeye Obama akitaka kusaidia watu wa kawaida aliopoteza kazi na wengine kushindwa kulipa mikopo ya nyumba nk. Kwenye kipengele hicho hicho nimesema mfumo Keynesian unadokolewa kidogo kidogo na rais aliye madarakani ili kuepusha uchumi kuyumba. Hapo ndio unaposema tax cut, lakini hiyo sio sababu ya kusema Marekani inatumia mfumo huu kuendesha uchumi wao wa kila siku au kila mwaka. Kama hivyo ni kweli, Biden anapanga kupandisha kodi na Trump amepunguza ruziki kwenda kwa wakulima na sekta zingine 2020, je na hapa bado kuna huo mfumo bado upo? Na kwa nini watumie huo mfumo wakati uchumi ulikuwa unaajiendesha wenyewe (pre Covid)?

Humu JF Kuna watanzania wanaishi Marekani, ladba watowe ushuhuda kama infrastructure ya Marekani bado iko up to world stand au ndio mguu mmoja unachungulia kwenye kaburi. Tokea miaka ya 70, mimi sijaona uwekezaji mkubwa kama kwenye reli mpya, treni mpya super highway mpya. Ukilinganisha na nchi ndogo za Asia, Marekani wamejisahau kabisa kwenye nyanja ya miundo mbinu. Trump alijitutumua na msemo wake wa America First, akaahidi atafanya maajabu ya kurudisha viwanda, kujenga viwanda vipya, na hata kujenga reli nchi nzima. Mwaka wa nne huu, hata reliable 5G infrastructure ni shida. Hata Tanzania tumewashinda, tukichukulia ukubwa wa nchi yetu pamoja na ukubwa wa uchumi wetu, ndani ya miaka mitano tumeweza kuanzisha na kuendeleza major infrastructure projects tatu na zingine ziko kwenye pipelene.

Labda niseme tena, military spending can not and will not stimulate economy. Swali moja la kujiuliza kwani wanaojihusisha na jeshi (iwe kampuni binafsi za supply au hata wanajeshi wenyewe) wako wangapi? How can you compare agricultural spending with military spending in terms of value of return. Infact, kila $ inayokwenda kwenye matumizi ya kijeshi, ni pesa iliyopokonywa kutoka miradi mingine ya maendeleo ambayo ingeweza kuleta chachu kwenye uchumi.

https://www.investopedia.com/articles/investing/072115/how-military-spending-affects-economy.asp

Haya mambo ya kutumia PPP vs GDP kulinganisha pesa ya nchi moja kwa nyingine ndio kujuwa uchumi wa nchi unafananaje, ni maswali yenye utata mwingi. Nchi nyingi viwango vyao vya thamani ya pesa inashuka kulinganisha na walivyokuwa wanatumia zamani GDP. Kuna report inaonyesha Marekani hawajapishana sana na China kama walitumia PPP.

Hii hapa ni kauli yako:
Tatu, wewe siyo mtu mkweli au aidha huelewi nilichokisema: Tanzania hatuna Progressive Tax tuna Proportional Tax.

Makundi yote hulipa asilimia moja ya pesa katika vipato vyao, kama ipo hebu tupe mifano. Uchina ukiwa tajiri na kodi inaanza kuwa Progressive. Kafanye tafiti zaidi au kama unataka tuanze kuongelea kodi basi fungua uzi mwingine.

Sasa kama hatuna progressive tax, rate ya 9% to 30% inatoka wapi na nani anatakiwa kuilipa? Ukimuuliza Google kama Tanzania ina tumia progressive tax, atatoa majibu ya haraka sana.

Umeniuliza ruzuku ya Marekani ya trilioni moja nimeitoa wapi, jibu ni bajeti ya Marekani ya mwaka 2019 iko wazi kabisa.

Imeulizwa kama subsidies za US haziingiliani na masharti ya WTO....

Unafikiri kwanini USA wanamkataa yule mama MNigeria Ngozi asuchukuwe ukurugenzi wa WTO? America will protect America.
Okay Good Luck Mkuu.....
 
jf ni zaidi ya darasa binafsi nadhani Kama serikali ingeifanya hii platform kuwa rafiki tungesogea mbele Kama nchi coz Kuna muda Mason yanayotupwa humu mpk unajiuliza how come tu maskini mpk leo🤣🤣
 
Alianza na kauli, kwa kusema chama chenye dola kushindwa kutetea dola yake ni uzembe!. Alishangaa iweje uwe na dola kisha upoteze dola.

Naam!. Kwenye uchaguzi huu tumeona alichomaanisha!. Bila shaka sote tuliona nini maana ya kutumia dola kubaki na dola, Tulishuhudia Kura kwenye vikapu vya akina mama, nyingine kwenye mabegi. Wapo waliozishika hizo kura na kuzipekeka polisi, polisi wakawajibu kwa mkato tu "Hatushughulikii masuala ya uchaguzi".

Maelfu kwa maelfu ya Mawakala wa vyama shindani wakapigwa zengwe, wakazuiwa kuingia, na wale walioningia wakapigwa zengwe wasipate nakala za matokeo.

Kule Zanzibar watu wakaonekana wanaopiga kura kwa lumbesa, mtu mmoja kura lundo.

Falsafa ya Bashiru Ally Kakurwa mtoto wa Kiislamu huyo aliyepitia madrasa!

Lakini huyu ni mwalimu wa chuo kikuu, msomi mkubwa, kafundisha wanafunzi wengi tu nadharia za demokrasia, ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi ya nchi yao wenyewe. Kafundisha sana masuala ya class struggle, ni role model wa maelfu ya wanafunzi wake wa ndani ya darasa na nje ya darasa! Sijui ametuma ujumbe gani kwa watu ambao walikuwa inspired naye kabla ya kuingia kwenye siasa pale wanapoona amekuwa katibu mkuu wa chama ambacho leo kimenufaika kwa mchakato feki na haramu kabisa wa uchaguzi, uliogubikwa na wizi wa kura wa kutisha katika historia ya nchi hii toka uhuru!

Lakini cha kuchekesha zaidi, Sheikh Bashiru Ally Kakurwa eti ni mjamaa, mfuasi wa Nyerere. Eti naye alikuwa mdau mkubwa wa Kigoda cha mwalimu. Eti naye alikuwa akiimba kama kasuku kuhusu uadilifu na sense ya haki ya mwalimu Nyerere.

Haya hatukuhadithiwa, tumeona kwenye TV mihadhara ya kigoda cha Mwalimu, Tumemuona Bashiru Ally Channel ten akielezea falsafa za haki, uadilifu, demokrasia, uhuru, umoja, n. k lakini hatukujua kuwa miaka michache baadaye, Bashiru huyuhuyu atakuwa ni katibu mkuu wa chama kilichonufaika kwa kuhujumu wananchi kuwaweka madarakani watu wawatakao wao wenyewe kupitia sanduku la kura!

Nikiangalia miaka michache ijayo nini itakuwa Legacy ya Bashiru Ally kwenye utumishi wa CCM, Siioni zaidi ya kushiriki kuwanyima wananchi viongozi na wawakilishi wawatakao watokanao na ridhaa zao wenyewe!. Kiufupi naye ni mshiriki asiyeweza kujivua lawama kwa dhulma hii kubwa waliyotendewa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata kama ngazi ya urais wa Muungano mlikuwa mkiitaka kwa udi na uvumba lakini Bashiru, hivi kweli Hussein ni wa kumshinda Maalim Seif kwa zaidi ya 57%?

Bashiru hivi kweli Tulia ni wa kumshinda Sugu Mbeya?

Hivi kweli Zitto ni wa kushindwa na yule Jamaa pale Kigoma? na mifano ya ya namna hii ni mingi nchi nzima!

Msomi na Mjamaa Bashiru hongera sana kwa kushiriki ipasavyo kuithibiti demokrasia vilivyo!, Maana sasa demokrasia ni kama adui yenu mliyefanikiwa kumdhibiti asifurukute!, But ngoja nikwambie kitu kimoja mko myopic sana kwa hizi moves zenu, kwa sababu ili mfanikiwe katika lengo lenu hilo ovu itabidi muwe wanafiki zaidi, walaghai zaidi, waonevu zaidi, madhulumati zaidi, msiheshimu wananchi zaidi.

Mtafanya hivyo mpaka mtakapokutana na kigingi kutoka kule ambako hamkukudhania kabisa, kisha hapo common sense zitawarudia kuwa ni USELESS KUDHANI KIKUNDI KIDOGO KINA AKILI KULIKO UMMA, maana umma utasimama na nguvu yeyote itakayokema yaani itakayoweka kigingi cha kuzuia dhulma zenu, nguvu ya kuzuia uonevu wenu, nguvu ya kuzuia ulaghai wenu!. Nguvu hiyo Ama inaweza iwe ni nguvu yoyote ya ndani ya nchi au ya nje ya nchi au zote mbili kwa pamoja as long as wananchi wataona hii inasimama nao na inawatetea wataiunga mkono kwa maua, nderemo, vifijo, bashasha, kucheza, kusifu, n. k!.

Mwalimu Bashiru, Nikukumbushe tu kuwa mahali popote pale duniani uchaguzi hovyo na corrupt, huzaa serikali hovyo na corrupt na hutengeneza bunge hovyo na corrupt lisiloogopa wananchi bali wale waliowawezesha kuingia bungeni kwa njia corrupt!. Kamwe haiwezekani kupata maendeleo kwa bunge na serikali ya aina hiyo, maana hiyo si serikali na bunge la watu kwa ajili ya watu, bali ni kundi tu la watu wachche tu wenye "special interests" lenye kumiliki silaha na kwa silaha hizo huwatisha wananchi wasinyanyuke na kudai haki yao ya kuwa na viongozi watokanao na ridhaa yao, lakini ukweli ni kuwa serikali ya hivyo na bunge la hivyo havina legitimacy mbele ya watu hao!

Bashiru Umeshiriki dhambi ya kuwadhulumu haki wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, unajisikiaje, "umewaweza" wapinzani au "umeiweza" nchi?. Kwamba umeacha alama ya heshima au alama ya aibu?

Shame on you!
Bashiru muuza ndizi ni tapeli kama gwajima tu
 
Pilot scheme huwa ni small scale, huwa haiwi rolled nchi nzima tena kwa vitisho vya wakuu wa wilaya, mkoa, wakurugenzi etc.

Wewe unasema ni kodi, Magufuli wakati anavizindua alisema anavitoa bure ila tu hiyo 20000 ni ya kurudisha gharama ya kuvitengeneza!.

Sasa hapo kuna mawili mmoja kati yako au Magufuli ni muongo. Kama hiyo 20000 ni kodi kwa nini wakati anavizindua aviite ni bure!. Na kama ni kodi aliianzisha hiyo kodi kwa mamlaka yapi, maana kisheria kodi inawekwa na bunge au serikali za mitaa!.

Hivyo vitambulisho vilichapwa na nani kwa procurement ipi iliyotangazwa na serikali?

Waseme tu kuwa buku 20 za wamachinga wamezichikichia, hakuna cha hazina wala nini!. Kama Magufuli alisema buku 20 ni hela za kurudisha gharama za kuvitengeneza basi hizo peza haziwezi kwenda kwenye account za TRA, maana TRA hawakusanyi peza zisizo za kikodi!. Kwa hiyo hatujui hizo pesa zimeingia kwenye account ipi, na hatujui huyo aliyebichapa alivichapa kwa gharama gani halisi!
Haha, kwanza hakuna tafsiri yoyote inayolazimisha neno Pilot Scheme kutumika wa watu wachache au eneo dogo. Ni dhumuni lako ndio litapona ukubwa wa Scheme unayotaka kuifanya. Pili, rais ana mamlaka ya kuidhinisha malipo au kusitisha malipo ya hazina. Na inaonekana umemuelewa vibaya aliposema pesa nimeitoa mimi, hakumanisha pesa imetoka mfukoni mwake ila fedha imeidhinishwa kwa tamisemi (ambayo iko chini ya office ya rais) kutengeneza vitambulisho. Vitambukishimo vyenyewe vina maneno yanasema KWA MATUMIZI YA TRA. Sasa TRA kazi yake ni nini kama sio kukusanya kodi? Wakati wakuu wa mikoa na wilaya wakibebeshwa maboksi ya vitambulisho waliambiwa mkiviuza kwa wajasiriamali, pesa yote inakwenda TRA na TRA iwape risiti. TRA ikikupa risiti ina maana gani kama sio utambulisho umelipa kodi? Ukinunua kitambulisho kwa Sh 20,000 sio kama ndio utakitumia milele na hulipi tena, kula mwaka TRA itataka 20,000 yake au kiwango kitakachohitajika mbeleni..
 
Alianza na kauli, kwa kusema chama chenye dola kushindwa kutetea dola yake ni uzembe!. Alishangaa iweje uwe na dola kisha upoteze dola.

Naam!. Kwenye uchaguzi huu tumeona alichomaanisha!. Bila shaka sote tuliona nini maana ya kutumia dola kubaki na dola, Tulishuhudia Kura kwenye vikapu vya akina mama, nyingine kwenye mabegi. Wapo waliozishika hizo kura na kuzipekeka polisi, polisi wakawajibu kwa mkato tu "Hatushughulikii masuala ya uchaguzi".

Maelfu kwa maelfu ya Mawakala wa vyama shindani wakapigwa zengwe, wakazuiwa kuingia, na wale walioningia wakapigwa zengwe wasipate nakala za matokeo.

Kule Zanzibar watu wakaonekana wanaopiga kura kwa lumbesa, mtu mmoja kura lundo.

Falsafa ya Bashiru Ally Kakurwa mtoto wa Kiislamu huyo aliyepitia madrasa!

Lakini huyu ni mwalimu wa chuo kikuu, msomi mkubwa, kafundisha wanafunzi wengi tu nadharia za demokrasia, ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi ya nchi yao wenyewe. Kafundisha sana masuala ya class struggle, ni role model wa maelfu ya wanafunzi wake wa ndani ya darasa na nje ya darasa! Sijui ametuma ujumbe gani kwa watu ambao walikuwa inspired naye kabla ya kuingia kwenye siasa pale wanapoona amekuwa katibu mkuu wa chama ambacho leo kimenufaika kwa mchakato feki na haramu kabisa wa uchaguzi, uliogubikwa na wizi wa kura wa kutisha katika historia ya nchi hii toka uhuru!

Lakini cha kuchekesha zaidi, Sheikh Bashiru Ally Kakurwa eti ni mjamaa, mfuasi wa Nyerere. Eti naye alikuwa mdau mkubwa wa Kigoda cha mwalimu. Eti naye alikuwa akiimba kama kasuku kuhusu uadilifu na sense ya haki ya mwalimu Nyerere.

Haya hatukuhadithiwa, tumeona kwenye TV mihadhara ya kigoda cha Mwalimu, Tumemuona Bashiru Ally Channel ten akielezea falsafa za haki, uadilifu, demokrasia, uhuru, umoja, n. k lakini hatukujua kuwa miaka michache baadaye, Bashiru huyuhuyu atakuwa ni katibu mkuu wa chama kilichonufaika kwa kuhujumu wananchi kuwaweka madarakani watu wawatakao wao wenyewe kupitia sanduku la kura!

Nikiangalia miaka michache ijayo nini itakuwa Legacy ya Bashiru Ally kwenye utumishi wa CCM, Siioni zaidi ya kushiriki kuwanyima wananchi viongozi na wawakilishi wawatakao watokanao na ridhaa zao wenyewe!. Kiufupi naye ni mshiriki asiyeweza kujivua lawama kwa dhulma hii kubwa waliyotendewa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata kama ngazi ya urais wa Muungano mlikuwa mkiitaka kwa udi na uvumba lakini Bashiru, hivi kweli Hussein ni wa kumshinda Maalim Seif kwa zaidi ya 57%?

Bashiru hivi kweli Tulia ni wa kumshinda Sugu Mbeya?

Hivi kweli Zitto ni wa kushindwa na yule Jamaa pale Kigoma? na mifano ya ya namna hii ni mingi nchi nzima!

Msomi na Mjamaa Bashiru hongera sana kwa kushiriki ipasavyo kuithibiti demokrasia vilivyo!, Maana sasa demokrasia ni kama adui yenu mliyefanikiwa kumdhibiti asifurukute!, But ngoja nikwambie kitu kimoja mko myopic sana kwa hizi moves zenu, kwa sababu ili mfanikiwe katika lengo lenu hilo ovu itabidi muwe wanafiki zaidi, walaghai zaidi, waonevu zaidi, madhulumati zaidi, msiheshimu wananchi zaidi.

Mtafanya hivyo mpaka mtakapokutana na kigingi kutoka kule ambako hamkukudhania kabisa, kisha hapo common sense zitawarudia kuwa ni USELESS KUDHANI KIKUNDI KIDOGO KINA AKILI KULIKO UMMA, maana umma utasimama na nguvu yeyote itakayokema yaani itakayoweka kigingi cha kuzuia dhulma zenu, nguvu ya kuzuia uonevu wenu, nguvu ya kuzuia ulaghai wenu!. Nguvu hiyo Ama inaweza iwe ni nguvu yoyote ya ndani ya nchi au ya nje ya nchi au zote mbili kwa pamoja as long as wananchi wataona hii inasimama nao na inawatetea wataiunga mkono kwa maua, nderemo, vifijo, bashasha, kucheza, kusifu, n. k!.

Mwalimu Bashiru, Nikukumbushe tu kuwa mahali popote pale duniani uchaguzi hovyo na corrupt, huzaa serikali hovyo na corrupt na hutengeneza bunge hovyo na corrupt lisiloogopa wananchi bali wale waliowawezesha kuingia bungeni kwa njia corrupt!. Kamwe haiwezekani kupata maendeleo kwa bunge na serikali ya aina hiyo, maana hiyo si serikali na bunge la watu kwa ajili ya watu, bali ni kundi tu la watu wachche tu wenye "special interests" lenye kumiliki silaha na kwa silaha hizo huwatisha wananchi wasinyanyuke na kudai haki yao ya kuwa na viongozi watokanao na ridhaa yao, lakini ukweli ni kuwa serikali ya hivyo na bunge la hivyo havina legitimacy mbele ya watu hao!

Bashiru Umeshiriki dhambi ya kuwadhulumu haki wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, unajisikiaje, "umewaweza" wapinzani au "umeiweza" nchi?. Kwamba umeacha alama ya heshima au alama ya aibu?

Shame on you!
Amewakomesha!

#LoserLissu.

#PoleniUpinzani
 
Vile vitambulisho havikutolewa risiti, ni magumashi mwanzo mwisho!
 
Keshaingia kwenye siasa uchwara za kuuwana tena hawezi kuwa mjamaa.
 
Vile vitambulisho havikutolewa risiti, ni magumashi mwanzo mwisho!
Hapo kabla halmashauri zilikuwa zikiwalipisha wafanyabiashara ndogondogo kama kati ya 400k na700k hivi kwa mwaka.

Sasa JPM akaja na "idea" kwamba ikitolewa 20,000 kila mwaka kipi bora?

Hapo waangalia mstakabali wa mjasiriamali na biashara yake na pia kipato chake.

Kumbuka kila mwenye TIN aanza kulipa kodi endapo mapato ni zaidi ya 4M kwa mwaka.

Wewe unafikiri vipi hapo?
 
Kwa kweli hata me siamini alichokifanya Mwalimu huyu......
 
Vile vitambulisho havikutolewa risiti, ni magumashi mwanzo mwisho!
Haha, ushahidi upo, pesa unaenda TRA. Lakini kwasababu wenzetu wa upinzani walikuwa wanakimbia Corana badala ya kuwa bungeni na kuhoji, kilichobaki ni kuita kula mtu mwizi.
 
Ni kweli mazingira hayatabiriki kwa sababu mbili kuu.

1. Wawekezaji si wawekezaji halisi na wapo kwa ajili ya kupata faida za harakaharaka na kutaka tax break za miaka mingi.

2. Baadhi ya viongozi wa Afrika au wale walo chini yao kuwa ndumilakuliwi khasa pale wanapofanya negotiations na wawekezaji.

Ni hapo Mchina anapotushinda, yeye kaweka sera za kiuchumi na ni lazima zifuatwe ila ni sera rafiki tu.

Sasa sisi ni kodi inasumbua sana wawekezaji tukifanikiwa hili la kodi tutakuwa sawa.

Kwa mfano serikali ingewaruhusu watanzania wenye uwezo kufanya joint venture na wawekezaji wa kigeni kwenye maeneo kama migahawa kama McDonald's, KFCs na Nandos.

Hivyo hawa wawaweka kwenye kundi maalum lenye kodi maalum.

Si lazima wawe ni wahindi tu kwenye kila kitu.

Hata wabantu nao wajitahidi ili waajiri wabantu wenzao na hapo soko la ajira linakuwa linapanuka.

Ndo maana naona watu kama Charles Kimei wanafaa kwenye biashara kwamba wana maono ya mbali kwenye masuala kama kuboresha micro economies.

Hata hizi reli zinazojengwa ni fursa kubwa sana ya kibiashara kwa mtu anaefahamu kupanga uchumi na sera.
Kwenye hili nakuunga mkono asilimia mia. Kama serikali ikiweka mazingira rafiki ya wazawa kufanya Joint-ventures na watu wa nje itasaidia sana kutatua kero ya ajira.

Lakini leo hii kukiwa na mkono wa raia wa kigeni kwenye biashara yako utasakamwa na kodi hadi utakata tamaa ya kufanya biashara.

Ushahidi ninao, kwa biashara ambayo Leseni kwa mzawa ni Tsh.200,000 kukiwa na mmiliki ambaye sio raia wa Tanzania ambaye amewekeza zaidi ya asilimia 50 kwenye hisa basi Leseni utaambiwa ni Tsh.6,000,000.

Haya nimeyashuhudia ofisi za halmashauri.
 
Sidhani kama ccm kama chama kilikuwa na mkakati na mpangokazi wa kushinda uchaguzi wa 2020 kwa namna ilivyoshinda. Nadhani huu ni mkakati wa vyombo vikishirikiana na Tume ya Uchaguzi. Lakini njia pekee ya Bashiru kunusuru heshima kidogo aliyobaki nayo ni kuachia nafasi ya Katibu Mkuu.
 
Hapo kabla halmashauri zilikuwa zikiwalipisha wafanyabiashara ndogondogo kama kati ya 400k na700k hivi kwa mwaka.

Sasa JPM akaja na "idea" kwamba ikitolewa 20,000 kila mwaka kipi bora?

Hapo waangalia mstakabali wa mjasiriamali na biashara yake na pia kipato chake.

Kumbuka kila mwenye TIN aanza kulipa kodi endapo mapato ni zaidi ya 4M kwa mwaka.

Wewe unafikiri vipi hapo?
Wewe umewahi kuona wapi kitambulisho hakina jina, picha, jinsia na hata kuuzwa kwake hakitolewi risiti!. Hicho kitambulisho kikiwa mfukoni mwako chako nikikichukua nikiweka mfukoni mwangu changu. Sasa hicho ni kitambulisho au magumashi!.

Magufuli alivyoingia madarakani aliponda vitambulisho vya NIDA alivyovikuta akasema namnukuu "vitambulisho vyenewe havina hata saini ya mtu", sasa miaka minne baadae yeye ndo akafunga kazi kabisaaa, akaleta vitambulisho visivyo na jina, wala picha wala hiyo saini, na wala kuuzwa kwake hakukutolewa risiti, na wala mchakato wa kuvichapisha umefanyika gizani.

Yale ni magumashi tu ni upigaji kama upigaji mwingine!
 
Alianza na kauli, kwa kusema chama chenye dola kushindwa kutetea dola yake ni uzembe!. Alishangaa iweje uwe na dola kisha upoteze dola.

Naam!. Kwenye uchaguzi huu tumeona alichomaanisha!. Bila shaka sote tuliona nini maana ya kutumia dola kubaki na dola, Tulishuhudia Kura kwenye vikapu vya akina mama, nyingine kwenye mabegi. Wapo waliozishika hizo kura na kuzipekeka polisi, polisi wakawajibu kwa mkato tu "Hatushughulikii masuala ya uchaguzi".

Maelfu kwa maelfu ya Mawakala wa vyama shindani wakapigwa zengwe, wakazuiwa kuingia, na wale walioningia wakapigwa zengwe wasipate nakala za matokeo.

Kule Zanzibar watu wakaonekana wanaopiga kura kwa lumbesa, mtu mmoja kura lundo.

Falsafa ya Bashiru Ally Kakurwa mtoto wa Kiislamu huyo aliyepitia madrasa!

Lakini huyu ni mwalimu wa chuo kikuu, msomi mkubwa, kafundisha wanafunzi wengi tu nadharia za demokrasia, ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi ya nchi yao wenyewe. Kafundisha sana masuala ya class struggle, ni role model wa maelfu ya wanafunzi wake wa ndani ya darasa na nje ya darasa! Sijui ametuma ujumbe gani kwa watu ambao walikuwa inspired naye kabla ya kuingia kwenye siasa pale wanapoona amekuwa katibu mkuu wa chama ambacho leo kimenufaika kwa mchakato feki na haramu kabisa wa uchaguzi, uliogubikwa na wizi wa kura wa kutisha katika historia ya nchi hii toka uhuru!

Lakini cha kuchekesha zaidi, Sheikh Bashiru Ally Kakurwa eti ni mjamaa, mfuasi wa Nyerere. Eti naye alikuwa mdau mkubwa wa Kigoda cha mwalimu. Eti naye alikuwa akiimba kama kasuku kuhusu uadilifu na sense ya haki ya mwalimu Nyerere.

Haya hatukuhadithiwa, tumeona kwenye TV mihadhara ya kigoda cha Mwalimu, Tumemuona Bashiru Ally Channel ten akielezea falsafa za haki, uadilifu, demokrasia, uhuru, umoja, n. k lakini hatukujua kuwa miaka michache baadaye, Bashiru huyuhuyu atakuwa ni katibu mkuu wa chama kilichonufaika kwa kuhujumu wananchi kuwaweka madarakani watu wawatakao wao wenyewe kupitia sanduku la kura!

Nikiangalia miaka michache ijayo nini itakuwa Legacy ya Bashiru Ally kwenye utumishi wa CCM, Siioni zaidi ya kushiriki kuwanyima wananchi viongozi na wawakilishi wawatakao watokanao na ridhaa zao wenyewe!. Kiufupi naye ni mshiriki asiyeweza kujivua lawama kwa dhulma hii kubwa waliyotendewa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata kama ngazi ya urais wa Muungano mlikuwa mkiitaka kwa udi na uvumba lakini Bashiru, hivi kweli Hussein ni wa kumshinda Maalim Seif kwa zaidi ya 57%?

Bashiru hivi kweli Tulia ni wa kumshinda Sugu Mbeya?

Hivi kweli Zitto ni wa kushindwa na yule Jamaa pale Kigoma? na mifano ya ya namna hii ni mingi nchi nzima!

Msomi na Mjamaa Bashiru hongera sana kwa kushiriki ipasavyo kuithibiti demokrasia vilivyo!, Maana sasa demokrasia ni kama adui yenu mliyefanikiwa kumdhibiti asifurukute!, But ngoja nikwambie kitu kimoja mko myopic sana kwa hizi moves zenu, kwa sababu ili mfanikiwe katika lengo lenu hilo ovu itabidi muwe wanafiki zaidi, walaghai zaidi, waonevu zaidi, madhulumati zaidi, msiheshimu wananchi zaidi.

Mtafanya hivyo mpaka mtakapokutana na kigingi kutoka kule ambako hamkukudhania kabisa, kisha hapo common sense zitawarudia kuwa ni USELESS KUDHANI KIKUNDI KIDOGO KINA AKILI KULIKO UMMA, maana umma utasimama na nguvu yeyote itakayokema yaani itakayoweka kigingi cha kuzuia dhulma zenu, nguvu ya kuzuia uonevu wenu, nguvu ya kuzuia ulaghai wenu!. Nguvu hiyo Ama inaweza iwe ni nguvu yoyote ya ndani ya nchi au ya nje ya nchi au zote mbili kwa pamoja as long as wananchi wataona hii inasimama nao na inawatetea wataiunga mkono kwa maua, nderemo, vifijo, bashasha, kucheza, kusifu, n. k!.

Mwalimu Bashiru, Nikukumbushe tu kuwa mahali popote pale duniani uchaguzi hovyo na corrupt, huzaa serikali hovyo na corrupt na hutengeneza bunge hovyo na corrupt lisiloogopa wananchi bali wale waliowawezesha kuingia bungeni kwa njia corrupt!. Kamwe haiwezekani kupata maendeleo kwa bunge na serikali ya aina hiyo, maana hiyo si serikali na bunge la watu kwa ajili ya watu, bali ni kundi tu la watu wachche tu wenye "special interests" lenye kumiliki silaha na kwa silaha hizo huwatisha wananchi wasinyanyuke na kudai haki yao ya kuwa na viongozi watokanao na ridhaa yao, lakini ukweli ni kuwa serikali ya hivyo na bunge la hivyo havina legitimacy mbele ya watu hao!

Bashiru Umeshiriki dhambi ya kuwadhulumu haki wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, unajisikiaje, "umewaweza" wapinzani au "umeiweza" nchi?. Kwamba umeacha alama ya heshima au alama ya aibu?

Shame on you!
Ukitaka kujua tabia halisi za mtu mpe haya yafuatayo :
1. Mpe pesa (mafanikio ya kiuchumi).
2. Mpe madaraka (mafanikio ya kiutawala)
Na haya yote ndiyo yamewapofusha Bashiru na bosi wake. Hawawezi kusikia la mtu . Majimbo matano mara wamedhulumu
 
Back
Top Bottom