johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Katibu mkuu wa CCM Dkt. Bashiru amesema CCM itapata ushindi mkubwa na wa kihistoria ambao haijawahi kuupata tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Bashiru amesema mwaka huu CCM iliyoshikamana bila uwepo wa makundi inashindana na vyama dhaifu sana vya upinzani.
Chanzo: ITV habari
------
MWANDISHI: Baada ya kubaki siku 12 kuelekea uchaguzi mkuu, labda status ikoje kwa upande wa chama cha mapinduzi?
BASHIRU: Ni ushindi mkubwa sana, unajua mwaka huu tumeshindana na vyama dhaifu kuliko wakati wote. Sasa vyama dhaifu hata vingekuwa na wagombea wazuri lazima pia utendaji wao uendane na uwezo wa vyama vyao kwa hiyo mwaka huu ukilinganisha na mwaka 2015 tumeshindana na vyama dhaifu.
Kwa mfano ACT ni chama kipya, chama kilichokuwa na mbunge mmoja wa Kigoma mjini na halmashauri moja, hakikuwa na muwakilishi hata mmoja Zanzibar wala mbunge Zanzibar.
Kimesimamisha mgombea wa Muungano ambae sijui amepotelea wapi, namtafuta sijui yuko wapi? Ningekuwa ndie katibu wake mkuu ningeshaenda polisi, sasa hao ndio tunaoshindana nao.
Wengine ambao wanajikakamua vyama ni dhaifu, kulikuwa na chama ambacho kilikuwa kidogo kimejiimarisha cha CHADEMA lakini kilikuwa na washauri wazuri waliokipa ushindi, wakina mzee Lowassa, mzee Sumaye wako CCM, wako majukwaani wanakitafutia kura.
Kwa hiyo mwaka huu tutegemee matokeo na ushindi ni mkubwa kuliko ilivyowahi kutokea katika mfumo wa vyama vingi kwa hiyo tunashindana na vyama dhaifu, vyama vilivyogawanyika, vyama vipya.
Sisi ni chama kikongwe, chama imara, chama ambacho kina umoja zaidi na kinachotupa nguvu ni kwamba mwaka huu hatuna migogoro ndani ya chama, tumeshikamana na hiyo umeiona wakati tunateuana.
MWANDISHI: Kati ya wagombea kuna mgombea gani tishio?
BASHIRU: Hakuna tishio hata mmoja, nimeshakwambia kwamba vyama vyote ni vipya na vyama vyote ni dhaifu kwa hiyo hatuna mgombea tishio