Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru: Wanaotegemea Tume Huru iwape ushindi wanajidanganya! Tume haipigi kura

Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru: Wanaotegemea Tume Huru iwape ushindi wanajidanganya! Tume haipigi kura

unabadilishaje kipengele cha Katiba bila ridhaa ya wananchi?
Nyie ndio mizigo iliyoteuliwa na JPM akidhani itamsaidia kumbe gunia la misumari. Wakati mwingine anabebeshwa lawama kumbe zinatokana na mizigo yake.
Zinazobadilishwa ni zile sheria zionekanazo zimekwenda kinyume na katiba mfano sheria ya uundaji wa Tume hiyo ya uchaguzi.
Ndio shida ya vyeo vya pachupachu hii!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hivi, usitake kutupia lawama kusiko stahili, wananchi ndio walitaka tume huru kwenye maoni yao, na wala wanaccm waliobaki bungeni hawakuwa na uhalali wowote wa kubadilisha maoni ya wananchi. Sasa unaposema wapinzani ndio waliosababisha huo mchakato kukwama kwa ajili ya kulazimisha serikali tatu, sijui hata unaongea nini. Hilo bunge la katiba zaidi ya 2/3 ilikuwa ni wanaccm, hata kama hao wapinzani wangebaki, una uhakika gani kuwa hilo suala wanaccm wangelikubali? Hivi unadhani hatukuona jinsi kanuni zilivyokuwa zinapindwa kila bunge lile lilivyokuwa linaendelea, ili kukidhi matakwa ya ccm? Kama kuna watu walipiga kura wakiwa nje ya bunge na nchi ili kuhalalisha katiba chafu, kipi kinachokufanya uamini kuwa tume huru ya uchaguzi ingepitishwa ndani ya bunge lile?

Angalau basi UKAWA ingeundwa kwasababu ya kutetea tume huru kwenye Katiba mpya, badala yake UKAWA agenda yake kuu ilikuwa kupinga Muungano wa serikali 2 kwenye Katiba. Angekuwa mm ndiye mwenyekiti wa CHADEMA kipindi kile ningewashauri wenzangu tukubali serikali 2 kwa sasa hadi hapo tutakoingia Ikulu baada ya kuwa na tume huru. Maana busara inaonyesha kuwa ccm wako wengi hivyo huwezi kuwashinda kwa hoja wala kwa kususia.

Nyie mnasusia na kupiga kelele mkidhani watu kama AU, EU, UN, IMF na wahisani watawasikia kelele zenu na kuchukua hatua, hapo ndio mnapokosea, mnasahau kuwa kwenye UKAWA kuna vibalagashia vinavyotiliwa mashaka na mabeberu kuwa vinadhamini ugaidi duniani ambavyo havipaswi kupata nguvu duniani.

Ondoeni kinyama kinachotoa harufu kwenye mfuko wenu wa koti kwanza. Hivyo wapinzani wenu "call you a bad name" to the western countries kwamba mnataka kusaidia kusimika Islamic state somewhere kwahiyo you deserve uninterupted harsh treatment.
 
Angalau basi UKAWA ingeundwa kwasababu ya kutetea tume huru kwenye Katiba mpya, badala yake UKAWA agenda yake kuu ilikuwa kupinga Muungano wa serikali 2 kwenye Katiba. Angekuwa mm ndiye mwenyekiti wa CHADEMA kipindi kile ningewashauri wenzangu tukubali serikali 2 kwa sasa hadi hapo tutakoingia Ikulu baada ya kuwa na tume huru. Maana busara inaonyesha kuwa ccm wako wengi hivyo huwezi kuwashinda kwa hoja wala kwa kususia.

Nyie mnasusia na kupiga kelele mkidhani watu kama AU, EU, UN, IMF na wahisani watawasikia kelele zenu na kuchukua hatua, hapo ndio mnapokosea, mnasahau kuwa kwenye UKAWA kuna vibalagashia vinavyotiliwa mashaka na mabeberu kuwa vinadhamini ugaidi duniani ambavyo havipaswi kupata nguvu duniani.

Ondoeni kinyama kinachotoa harufu kwenye mfuko wenu wa koti kwanza. Hivyo wapinzani wenu "call you a bad name" to the western countries kwamba mnataka kusaidia kusimika Islamic state somewhere kwahiyo you deserve uninterupted harsh treatment.

Agenda haikuwa moja kwenye bunge la katiba bali zilikuwa nyingi. Kila mtu ana uhuru wa kutetea anachoamini. Kama hao Ukawa wangeacha kutetea wanachoamini na kutii watakacho ccm, je hiyo tume huru ccm walikuwa wanaitaka? Kama ccm waliendelea kushikilia msimamo wao ni kipi kunakufanya uamini hiyo tume huru wangeikubali?

Nakupa mfano mmoja ujue kuwa ccm wangesimamia msimamo wao bila kujali wananchi wanataka nini kwenye hayo maoni, kumbuka kulikuwa na kifungu cha kumuwajibisha mbunge asipofanya vizuri, je kifungu hicho kilipita, au kiliondolewa kwa faida ya ccm? Ni hivi huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani.

Kwa taarifa yako hizo taasisi ilizotaka sijui EU nk sio wenye madai yetu, bali wao wanaweza kuweka msukumo tu. Ila kilichokuwepo kwenye rasimu ya Warioba ni madai halali ya wananchi. Usitake kuleta upotoshaji wako wa kidini kwenye hilo Jambo. Kama huna hoja kaa kimya.
 
Tatizo mmekaririshwa tu. Unajua hii katiba tulionayo, imefanyiwa amendment zaidi ya mara 4? Je hizo amendment zote ilipigiwa kura ya maoni?

Acheni upoyoyo katiba inabadilishwa kwa njia nyingi, acheni kumsikiliza Polepole amekuwa chizi baada ya kushiba. Kipindi anatembea kwa mguu ndio alikuwa na akili.

Katiba inadalishwa kutoka na mahitaji ya wakati, yawe ya kipindi kifupi, cha Kati na cha muda mrefu.

Hitaji letu sasa ni Tume huru ya uchaguzi, inatakiwa upelekwe mswaada bungeni kwa ajli ya kuunda tume huru.
Sasa iatundwaje, utaratibu wake, wajumbe wake na kazi zake hizo zitajadiliwa bungeni na kupitishwa kuwa sheria.
Hapo ndio utakapoingizwa kwenye katiba.

Sasa meambukizwa ujinga, na kujifanya mmesoma kumbe mafi ya umbwa kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bajeti ya kutekeleza hayo marekebisho unayo? Kwa muda uliobaki; utaweza kuajiri watumishi wapya wa hiyo tume? Kumbuka kazi ya uchaguzi inasimamiwa na wakurugenzi wa halmashauri nchi nzima na watumishi wengine, je mtaweza kupata pesa ya wage bill ya hiyo tume?

Je, mtaweza kuajiri watumishi wa tume kwa muda uliobaki?

Kenya wanayo tume huru na unajua nini ikitokea huko sihitaji kukumbusha. Mbatia ameuliza swali he ni nani anaweza ku define tume huru ni nini?

Elekeza rasilimali kwenye maandalizi ya uchaguzi wa 2020 Tume huru hutaipata kwa muda uliobaki.MLIKUWA WAPI MIAKA YOTE MINNE?
 
Nyenzo kuu ya kuingia Ikulu ni tume huru kwelikweli mambo mengine yote ni rahisi kuyabadilisha ukishafika Ikulu, wakati ule wa mchakato wa kuandika katiba mpya wapinzani walitakiwa kuona kipengele cha tume kimekaa vizuri kuliko kipengele kingine chochote. Lakini wapinzani waling'ang'ania serikali 3 na muungano wa mkataba hadi mchakato ukakwama kabisa. Hii yote ni kuonyesha kuwa upinzani ama hakuna weledi wa kutosha au kuna mamluki wengi saaana wanaowazuga wananchi.
Upinzani wa kweli utakuwepo siku CCM ikikatika vipande lakini hawa wapinzani ni shibe ndiyo inasumbua.
 
Upinzani wa kweli utakuwepo siku ccm ikikatika vipande lakini hawa wapinzani ni shibe ndiyo inasumbua.
Wao wanafahamu kwa 300% kuwa kwa Katiba na tume hii hawawezi kuingia Ikulu, bali wanachotaka ni ajira yao, ruzuku na ulinzi wa mali zao kwakutumia jasho la wananchi wenye nia ya mabadiliko.

Hama hama ya wapinzani kurejea CCM ni ushahidi wa hili. Wanawazuga walalahoi na kuwaamisha kuwa wataingia Ikulu, na wakishindwa kwenda Ikulu wanawadanganya kuwa tume iliyowatangaza wao kwenda bungeni imeiba kura za urais, shame upon them.
 
Agenda haikuwa moja kwenye bunge la katiba bali zilikuwa nyingi. Kila mtu ana uhuru wa kutetea anachoamini. Kama hao Ukawa wangeacha kutetea wanachoamini na kutii watakacho ccm, je hiyo tume huru ccm walikuwa wanaitaka? Kama ccm waliendelea kushikilia msimamo wao ni kipi kunakufanya uamini hiyo tume huru wangeikubali? Nakupa mfano mmoja ujue kuwa ccm wangesimamia msimamo wao bila kujali wananchi wanataka nini kwenye hayo maoni, kumbuka kulikuwa na kifungu cha kumuwajibisha mbunge asipofanya vizuri, je kifungu hicho kilipita, au kiliondolewa kwa faida ya ccm? Ni hivi huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani.

Kwa taarifa yako hizo taasisi ilizotaka sijui EU nk sio wenye madai yetu, bali wao wanaweza kuweka msukumo tu. Ila kilichokuwepo kwenye rasimu ya Warioba ni madai halali ya wananchi. Usitake kuleta upotoshaji wako wa kidini kwenye hilo Jambo. Kama huna hoja kaa kimya.
Ccm tunawaonea saa nyingine, Sura ya Kumi na mbili sehemu ya pili ya rasimu ya Katiba mpya ilikuwa inahusu Tume Huru ya Uchaguzi. Kwenye sehemu ile kulipendekezwa kuwe na kamati ya uteuzi wa wajumbe wa tume Huru ya Uchaguzi ambayo itawapendekeza kwa rais kwa uteuzi.

Na majina ya wajumbe ilikuwa wapitishwe na bunge kabla ya kuwa wajumbe wa tume Huru ya Uchaguzi. na watu watakaounda hiyo kamati ya uteuzi walitajwa kwa majina. na sifa za wajumbe zilifafanuliwa. Sikuwahi kusikia kama CCM walipinga mapendekezo haya ya uundwaji wa tume Huru ya Uchaguzi . Walichopinga kwa nguvu zao zote na kilichosimamisha mchakato wote ni serikali 3 na aina ya Muungano.

Kikubwa ccm walipingana na serikali 3 na muungano wa mkataba kwa wingi na nguvu zao zote.
 
Wananchi huku mitaani wameichoka kabisa ccm, hivi sasa wanacho ombe hii korona iendelee ili uchaguzi usogezwe mbele.
Wamebaki na nguzo moja tu ya kushilikilia na iking'oka hiyo hawana cha kushikilia tena.

Na nguzo hiyo ni tume ya uchaguzi iliyopo.Upinzani wakifanikiwa kuchanga karata zao vizuri na ikapatikana tume huru ccm itakuwa imebaki historia.

Ni bora hata uchaguzi upelekwe mbele ili kuruhusu mjadala wa kitaifa wa tume huru kuliko kuenenda kwenye uchaguzi na tume hii fake.

Kama wewe ni MATAGA na unataka kuchangia huu mjadala kabla ya kuchangia uje kwanza na jibu Mbunge Cecil Mwambe yupo bungeni kwa kifungu kipi ndio uchangie huu mjadala
 
CCM wamejitengenezea uadui na wananchi kwa kujitakia, no ajira, wanataka wote tusome sayansi ndio tuajiriwe mahospitalini, wameahidi ahidi hewa kibao, hii ya 50M kila kijiji ndio imewaumbua, gharama za maisha zimepanda Mara 10.
 
Back
Top Bottom