Mbowe ameamua kudai tume huru, na wewe unaweza kudai katiba mpya on your own.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Tume ya UchaguziMasharti ya kazi ya Wabunge Sheria ya 1984 Na.15 ib.13Sheria ya 2000Na.3 ib.1474.-(1)
Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:-
(a)Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;
(b)Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;
(c)wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge.
(2) Rais atamteua Makamu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kwa kufuata kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.
(3) Watu wafuatao hawataweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi yaani-(a)Waziri au Naibu Waziri;(b)mtu mwenye madaraka ya aina yoyote iliyotajwa mahsusi na sheria iliyotunga na Bunge kwamba ni mwiko kwa mtu mwenye madaraka hayo kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi;(c)Mbunge, Diwani au mtu mwingine mwenye madaraka ya aina yaliyotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa masharti ya aya ya (g) ya ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 67 ya Katiba hii.(d)Kiongozi wa chama chochote cha siasa.
(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi atakoma kuwa Mjumbe litokeapo lolote katika ya mambo yafuatayo-(a)Ukimalizika muda wa miaka mitano tangu alipoteuliwa; au(b)ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mjumbe wa Tume, lingemfanya asiweze kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.
(5) Rais aweza tu kumwondoa katika madaraka Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake, ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote, au kwa sababu ya tabia mbaya au kupoteza sifa za kuwa mjumbe.
(6) Majukumu ya Tume ya Uchaguzi yatakuwa ni-(a)kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano;(b)kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais na Wabunge; (c)kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge;(d)kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura na uendeshaji wa uchaguzi wa madiwani;(e)kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.
(7) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake yaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge.
(8) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya kuweka utaratibu wa kusimamia uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi.
(9) Tume ya Uchaguzi yaweza kutekeleza shughuli zake bila ya kujali kwamba kuna nafasi miongoni mwa viti vya wajumbe au kwamba Mjumbe mmojawapo hayupo, lakini kila uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengi kati ya Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi.
(10) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya kuweka utaratibu wa kuwateua Wajumbe wa kusimamia uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi na, bila ya kuathiri masharti ya Sheria kama hiyo au maagizo ya Tume ya Uchaguzi, madaraka ya Tume ya Uchaguzi ya kusimamia uchaguzi yaweza kutekelezwa na wajumbe hao.
(11) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, Tume ya Uchaguzi haitalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali, au maoni ya chama chochote cha siasa.
(12) Hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(13) Katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano itashauriana mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi ya Tanzania Zanzibar.
(14) Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kila mmoja wao atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
15) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (14) watu wanaohusika na uchaguzi ni-(a)Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,(b)Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,(c)Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi,(d)Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote wa Tume ya Uchaguzi,(e)Wasimamizi wote wa Uchaguzi katika miji na wilaya
Jamani tuheshimuni katiba bila shuruti