Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
- Thread starter
-
- #21
Wewe ndio unapotosha hapa, unapotaka kuleta kitu ambacho unaona wewe kwako ni muhimu basi unataka wote waone hivyo.
Ndio maana niliweka neno "LAZIMA" hili neno likishakua haina mjadala tena, lakini Ndoa sio Lazima ni hiyari, watoto ambao unataka wapatikane kwa njia hiyo pia sio lazima, na hata kufanya tendo lenyewe ili mtoto atokee sio lazima.
Wewe km mafanikio yako ni Ndoa, ni wewe wala hujapangiwa au kuzuiwa, ila kupangia na kuzuia wenzio wanaoona Ndoa sio Mafanikio, hapo ndio unakosea.
Kama unaongelea mafanikio binafasi ni sawa maana hata kwa Wasukuma kuoa mwanamke mweupe ni mafanikio, kwa wanaume wengi wa wabongo wengi kuwa na mwanamke mwenye makalio makubwa ila kwa Wazungu na Wa-Asia ni kinyume chake.Upo sahihi kabisa.
Na huwezi sema sehemu ambazo hujafanikiwa wewe sio mafanikio.
Fikiria mtu aseme kupata unprofessional sio mafanikio. Imagine mtu huyo wewe utamuonaje?
Au mtu akuambie kumiliki Gari aina fulani sio mafanikio. Wewe utamuonaje?
Mabilionea wasio na ndoa,
Elon Musk
Jack Dorsey
Putin
Oprah Winfrey
DiCaprio
Ian Khama
Kama unaongelea mafanikio binafasi ni sawa maana hata kwa Wasukuma kuoa mwanamke mweupe ni mafanikio, kwa wanaume wengi wa wabongo wengi kuwa na mwanamke mwenye makalio makubwa ila kwa Wazungu na Wa-Asia ni kinyume chake.
Ndoa ni mafanikio Binafsi au Jumla?Kwenye haya maisha hakuna kitu cha lazima.
Kitu hata kama sio cha lazima kwako haimaanishi kwamba sio mafanikio. Hiyo ndio hoja yangu.
Mfano kufikisha miaka 90 ni mafanikio lakini najua kuna vichwa panzi wenzako kwa vile wanaona sio lazima watakuambia sio mafanikio.
Ndoa ni mafanikio. Ni wewe tuu na wenzako wasiojua mifumo ya ulimwengu ndio hawaelewi haya mambo.
Kuna mdau hapo juu nimemwambia na narudia kwako.
Ukiona jambo lolote limetungiwa sheria, unapewa Vibali, au vyeti na serikali ujue kuwa nalo jambo hilo ni mafanikio. Najua utabisha tena
Ndoa ni mafanikio Binafsi au Jumla?
Wewe miaka 30 ijayo ndio watu hawatasikia tena jina lako pamoja na kuwa na ndoa ya wake wanne na watoto ishirini.Hao wamefanikiwa kiuchumi lakini kwenye ndoa wamefeli.
Sasa angalia baada yao je nini kitatokea. Ndoa na familia ndio kitu pekee ambacho mafanikio mengine yanaweza kurithishwa kutoka kizazi hata kizazi.
Huyo Elon Musk miaka 100 ijayo hutosikia jina lake tena.
Nenda uarabuni, matajiri wanautajiri miaka na miaka, karne na karne. Hiyo ndio kazi ya ndoa Babu.
Hao wazungu wenyewe mifumo yao sasa hivi inaenda kufeli vibaya sana ndio maana wanahangaika na waarabu
Kabla ya mkoloni, Wamatumbi walikua na akili ipi kubwa? Em tujuze hapa tuone.Ndoa ni mafanikio sio tuu ya binadamu bali mpaka wanyama.
Hao wazungu ni na Waasia sehemu ndogo sana ya ulimwengu.
Elimu ya mkoloni imeharibu akili zenu aiseeh! FaizaFoxy hapa yupo sahihi
Wewe miaka 30 ijayo ndio watu hawatasikia tena jina lako pamoja na kuwa na ndoa ya wake wanne na watoto ishirini.
Mtibeli, Naomba Ule uzi wako wa "Dunia inaogopesha Maisha sio Mashindano" Uliuandika Mwaka 2023 kama sikosei... Ulimwaga Madini Mengi Sana Mulee....
Nisaidie Ule Uzi Kaka....!!!
Kama ulivyosema hapo mkuu.Upo sahihi kabisa.
Na huwezi sema sehemu ambazo hujafanikiwa wewe sio ,
Hivyo basi,Ndoa ni moja ya vipimo vya mafanikio ya mtu. Hilo mtu yeyote ambaye anaakili timamu analijua. Sasa mtu umeenda shule mpaka umefika chuo kikuu. Ukaongeza na elimu. Unashindwaje kujua jambo dogo kama hilo?
Kabla ya mkoloni, Wamatumbi walikua na akili ipi kubwa? Em tujuze hapa tuone.
Wewe unachozungumzia ni Mazoea, basi.
Kwani usiweke jumla unaweka Taifa? Nini maana yake?Ndoa ni mafanikio ya kibinafsi na kitaifa.
Bila ndoa hakuna taifa.
Sijui kwa nini haya hamyajui. Ni kwamba uwezo mdogo au hamfundiShwi?
Ndoa inaongeza nguvu kwenye familia zenye Akili na madaraka.
Serikali bila ndoa haiwezi kuendeshwa. Hili pia mtabisha
Ian Khama ni MuAfricaHuwezi kunielewa kwa akili zako mpaka uige au usome kwa watu au wazungu. Akili zako ungezitumia vizuri ungeelewa mada ndogo kama hii.
Kama ulivyosema hapo mkuu.
Hivyo basi,
Mafanikio ya mtu yanapimwa kwa malengo yake binafsi.
Ndoa inaweza isiwepo au iwepo kwenye malengo ya mtu kufikia safari yake ya mafanikio.
Nikichambua mafanikio kwa undani zaidi Nbinafsi nahitimisha wewe na Dr mpo sahihi. Kila mtu kwa upande wake.View attachment 3697470
Ian Khama ni MuAfrica
Ndoa ni nini? Na mume na mke ni nini?Wamatumbi walikuwa na Akili kuliko sasa hivi.
Sasa hivi wamatumbi ndio hawana Akili.
Mtu hajui hata maana ya ndoa, hajui umuhimu wa ndoa, haoni umuhimu wa kuwa na mke au mume. Alafu muda huohuo anaona umuhimu wa kuwa na watoto. Utasema huyo zimetimia?
Kilichowarostisha wamatumbi ni usaliti tuu.
Kwani usiweke jumla unaweka Taifa? Nini maana yake?
Ndoa ni mafanikio binafsi, wala sio jumla, na hata huko Taifa unakozungumzia, ni uongo, hoja yako ni watu au uzao, sasa watu au uzao unaweza kupatikana bila ndoa.
Ndoa ni nini? Na mume na mke ni nini?
Kabla ya kujibu, soma vizuri na uelewe halafu twende sawa.