Dkt. Emmannuel Nchimbi afukuzwa uanachama wa CCM

Dkt. Emmannuel Nchimbi afukuzwa uanachama wa CCM

wacha kiherehere potiii
AMEFUKUZWA uanachama.
Itakuwa hata ile barua wameandika wao

Seems jamaa aligoma kutoa ushirikiano na summon zao za kifala

Inaonekana jamaa kawekwa Quarantine na kaambiwa asifanye chochote . Wahuni wana handle kila kitu
Seems jamaa hayupo hata kwenye mawasiliano

Makamu wa Rais kweli ajiuzulu kwenye mitandao duh

Ila that is good sign

Ili mbegu iote lazima ioze
TZ inapoelekea ni kwenye ukumbozi
 
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imemfutia uanachama wa Chama hicho leo Agosti 26, 2026 aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmannuel Nchimbi ambaye alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa jana Agosti, 25, 2026.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro leo Agosti 26, 2026 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba.

Dkt. Migiro ameeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa mara baada ya kukaliwa kwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho ambavyo vilijadili suala la maadili ya Dkt. Nchimbi na vikaazimia kwa pamoja kumfuta uanachama mwanachama huyo.

Soma Pia: Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Kitakacho fuatia ni kumpolepole.
 
Wanajua ataendelea kuwasumbua kwa sababu ana wafuasi wake wengi ndani ya chama. Walichokifanya hapa ni kukata mti na pia kung'oa kabisa na mizizi ili matawi ya huo mti nayo yakauke.

Ni umafia wa hali ya juu sana.
kama Kuna matawi yapo ccm yapo tu hata ukikata huo unasema ni mzizi.
Hata hivyo nchimbi kaamua kukaa upande SAHIHI.
hao wengine wanataka mpaka waje kutolewa na mtoa roho.
 
Nchimbi kama bado hujazingirwa mahali kokote uliko wahi ubalozi wowote usepe nje ya nchi.

Usije sema sikukwambia!!

Kama utasoma hapa(maana kwa hali hii sidhani kama upo huru hata kishika simu yako. Wajuba watakuwa wapo na wewe bampa to bampa)


Tlaatlaah aa ile ajenda yako inazidi kuzikwa. Nilikutahadharisha usikimbie ID. Yako
 
Back
Top Bottom