Freddie Matuja
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,479
- 2,877
Rais John Pombe Magufuli leo karejesha form ili kuwania ungwe ya dakika 45 za pili kukamilisha dakika 90 za awamu ya 5 ambayo ni miaka 10. Leo naomba kuwananga vijana hasa UVCCM ili muoni nini mnaweza kufanya dakika 45 zilizosalia. Naandika haya nikiwa na hakika mgombea wenu ana nafasi kubwa sana ya kupata uteuzi wa CCM na kupigiwa kura October mwaka huu.
Magufuli Rais wangu nakusifu sana sio kama wale wengine wanaoitwa “Paise Team” ila kwa kuwa umekuwa na upekee kuiona nchi hii ni tajiri na umekuwa ukijangamba kwa nguvu kwenye hili huku ukitekeleza mengi kwa ilani ya CCM na kufanya yale yalio kwenye mpango wa taifa ili kuifikia Tanzania Dev. Vision 2025.
Pamoja na mengi yanayofanyika serikalini baada ya kuja na kauli mbiu ya kuijenga Tanzania na kukuza uchumi wake kwa kutumia viwanda, nadhani ndani ya chama chako CCM kuna watu wanakosa msaada kwa wana CCM na Watanzania as a whole; hapa ntawagusa vijana maana wana nguvu ya kifikra na ilitakiwa moja ya fikra iwe kufikiria na kutekeleza kwa vitendo kwa walau kuwa na model factory inayomilikiwa na vijana hata kama hawausiki moja kwa moja na management ya daily operations. Ntafanua na kuja na mifano rahisi.
Mmoja wa wahusika kwenye changamoto hii ni pamoja na Dr. Frank Haule ambae ni Mkuu wa Idara ya Uchumi ya CCM.
Nadhani wengi tunakumbuka kuwa Mwl. Nyerere ameiachia CCM assets nyingi sana ikiwemo majengo na viwanja maeneo mengi na sehemu za kimkakati kabisa kama Lumumba Dar au Mwanza na miji mingine. Mpaka sasa majengo yamekuwa ni asset kwa kupangisha na hivyo kuingiza fedha kwenye kapu kuu pia kutoa ajira. Majengo ni service sector. Nataka niwafikirishe kwenda kwenye manufacturing sector.
Kwa kuwa vijana wa CCM mna bahati ya kuwa na Mkiti wa CCM ndg. Magufuli ambae ana sifa kubwa ya kudiriki na kutekeleza makubwa, nadhani ilitakiwa vijana ndani ya chama toka JPM ameingia madarakani walau wangekuwa wamejenga hata kiwanda kimoja. Say, kiwanda cha kuchambua pamba na kutengeneza vitambaa vya kijani/njano au vitenge kwa soko la CCM kwa kuwanzia. Kwakuwa chama kina wanachama zaidi la milioni 6, maana yake kiwanda kikitengeneza skafu, vitambaa vya leso, bendera kubwa, bendera za mezani, vitenge/ batiki kama uniform ya mwenge kila mwaka, vitambaa vyeusi kwa ajili ya suruali au sketi; hizi fedha za kuagiza kila siku india basi CCM kama taasisi ifanye vitu kwa ubora ili kutengeneza ajira kwa wana CCM ambao watapata ajira viwandani au mtanzania yeyote.
Kampeni za mwaka huu, ingenogeshwa kwa vitambaa vya mapambo na hiena hiena zote zikiwa ni made in Tanzania kupitia industries owned by CCM hususan wing ya vijana.
Kwanini chini ya UVCCM kusianzishwe kurugenzi maalumu ya kukuza uchumi na biashara kwa kutumia viwanda vya kimkakati ambavyo soko lake hata likilenga wana CCM kwa kuanzia kama mtaji. Mpaka lini kwenye kampeni ndio Tshirts za skafu za wabunge zinatoka CHINA; hapa nawashaurini mfanye namna mdake fursa ungwe ya 2020-25
Najinasibu na kujivunia Tanzania yangu kwa maana naona JPM anaota ndoto kubwa sana, ila anakosa wasaidizi ikiwamo kwenye level ya chama kutafsiri ndoto kwa picha kutengeneza bidhaa ambazo CCM kama taasisi na watu wake wanaweza kuwa consumers.
Cha msingi kuwa na nidhamu kwa kuwa na menejimenti mahiri ili uendeshaji wa kiwanda usifanyike kisiasa na malipo yafanyike kwa kila bidhaa itakayonunuliwa kiwandani kwa mahitaji ya bendera, vitambaa, vitenge, batiki nk.
China kwanini hanunui bendera zake Marekani; China kwanini hanunui sare za watu wake marekani au India?
Sina maana kuwakosea heshima wenye chama chenu, ila niko hapa kuwapa kufikiri sana kwa manufaa ya kumfagilia Mkulu ila wakati huo huo, namna gani kudaka kwa vitendo ndoto ya kujenga kiwanda ambacho vitambaa vya aina mbalimbali vutakavyozalishwa hapo kwa ubora wa soko, vitaweza kuwashawishi mafundi cherehani wawe na chama au hawana chama kununua kwenu.
Hili likifanyika, litaongeza mzunguko wa fedha kwa kupunguza imports za vitambaa toka China/India au kokote kule ambako kila mwaka tuna-agiza. Sio ufahari kuagiza kila mwaka vitu ambavyo malighafi pamba ipo na soko la wanaovaa nguo wapo.
Mkiona mnakosa watu wenye DNA ya kufikiri hivyo ndani ya CCM, maana yake watafutwe ndani ya Tanzania, wakikosekana basi hata nje ya nchi tuwalete ili kujenga uchumi jumuishi.
Nimetoa mfano wa textile industry, linaweza lisiwe wazo feasible kwenu, ila kwanini msifikiri kwenye sekta zingine ambazo soko lake lipo. Mfani mwingine, sukari ya matumizi ya nyumbani na viwanda kila mwaka tuna import zaidi ya tani 50,000.
Kama jengo la vijana ambalo Nyerere kaliacha lina function kuingiza fedha mpaka sasa, kwanini basi lisitafutwe wazo hata la kiwanda cha kutengeneza soft brooms na hard brooms, na moppers kwa ajili ya matumizi ya maofisi na majumbani na kuacha kununua mifagio na moppers made and imported from China.
Ni wazo tu kwenu wakubwa, mnapojenga miundombinu ya uchumi mkubwa kama SGR na Nyerere Hydro Electric Power Dam, pia hata huu uchumi mdogo mdogo wa mifagio ya maofisini ikiwa made in Tanzania kuna fedha si haba zitaingia kwenye mifuko, mabenki, mobile money na kote huko kuna deductions serikali inapata in the course of spending.
Shalom.