Mtoto halali na hela
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 52,160
- 48,974
Kesho yako ndiyo ndefu hao jamaa wanabebana kishenzi refer kesi ya sabayaHakika hakuna anaejua kesho itakuwaje.
Godbless Lema huwa anasema sana huu msemo. Kesho ni ndefu sana.
Akina mnyeti wanapewa uwaziri!! Hiyo ni sanaa tu kama ya bibi wa miaka 60 na kijana!Hukumu hizi pia zingekuwa zinatoka kwa mawaziri wezi, makatibu wakuu wezi, MaRC wezi nk na hata MaRais wezi bila shaka Taifa lingekuwa mbali sana kiuchumi.
Mnazidi kutucheka tu. Yani wote watatu???Hatari
Hawatamaliza hata miaka miwili wanatoka baada ya kukata rufaa.Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na makosa ya uhujumu uchumi.
Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Agost 31, 2023 na Hakimu Seraphin Nsana, katika kesi namba 5/2023 ya uhujumu uchumi, iliyokuwa inawakabili Dk. Pima, aliyekuwa Mweka Hazina wa jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.
Akisoma hukumu hiyo ya kesi namba 5/2023, mbele ya mahakama hiyo, Hakima Nsana amesema kuwa baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, mahakama imewatia hatiani washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili.
"Kwa kuzingatia maombi ya mawakili wa upande wa washtakiwa, ikiwemo kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, utegemezi wa familia na ushirikiano mlioutoa katika kipindi chote cha uendeshaji wa kesi hii, mahakama inawapa adhabu ya kutumikia miaka 20 jela huku miezi 14 mliokuwa kizuizini ukizingatiwa," amesema
Mbali na hilo, washtakiwa wana haki na nafasi ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu endapo hawajaridhika na hukumu hiyo.
(Imeandikwa na Bertha Ismail)
#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
Hiyo miezi 14 itapunguzwa kwenye hiyo miaka 20 ?.... anyway Ccm imemzamisha.Kwa kuzingatia maombi ya mawakili wa upande wa washtakiwa, ikiwemo kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, utegemezi wa familia na ushirikiano mlioutoa katika kipindi chote cha uendeshaji wa kesi hii, mahakama inawapa adhabu ya kutumikia miaka 20 jela huku miezi 14 mliokuwa kizuizini...
Ilikuwa mwaka gani?Hawa jamaa walijenga soko Moja kioja sana pale mbauda kwa gharama ya 1.4B... yaani pale kama walitumia sana pesa ni 200M, siku ya kulizindua... PM majaliwa alifika akapigwa na butwaa, akageuza msafara akagoma kulifungua akasema ni uchafu ule, akaamuru wakamatwe... Ndo kilichowafunga hao.... Ila ile pesa walipiga wengi tu Hawa ni mbuzi wa kafara
Watakata rufaaWacha watumikie tu kifungo,si waliiba!
Baada ya kifo Cha jpm, nadhani mwaka Jana mwanzoniIlikuwa mwaka gani?
Umesoma ukaelewa?Kwahio ni miezi SITA TU?
Kwanini yasiwepo?, ukihujumu uchumi utaadhibiwa tu.Haya mambo ya uhujumu uchumi si walisema hayatakuwepo tena baada ya Magu kufa..mbona bado yanaendelea sasa?
Lema hata kwa uchaguzi huru hashindi 2025. Labda mgombea wa CCM awe Gambomahakama imefanya vyema maana huyo pima alishiriki kumdhurumu Lema ubunge shenz kabisa.
Hawa kina Pima na baadhi ya inner circle ya Sukuma Gang walikuwa viburi sana enzi zao.... bado Gambo maana naye kipindi akiwa RC alikuwa hazuiliki. Wanashughulikiwa kimyakimya kisheria.Baada ya kifo Cha jpm, nadhani mwaka Jana mwanzoni
Jiwe alifanya kwa uonezi, sema Mungu ndiye aliingilia kati tukanusurikaHaya mambo ya uhujumu uchumi si walisema hayatakuwepo tena baada ya Magu kufa..mbona bado yanaendelea sasa?
Wamehukumiwa kwenda jela MIAKA 20 lkn wamehudumu MIEZI 14Kwahio ni miezi SITA TU?
Hapakuwa na option ya fain hata ya 5mlMahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na makosa ya uhujumu uchumi.
Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Agost 31, 2023 na Hakimu Seraphin Nsana, katika kesi namba 5/2023 ya uhujumu uchumi, iliyokuwa inawakabili Dk. Pima, aliyekuwa Mweka Hazina wa jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.
Akisoma hukumu hiyo ya kesi namba 5/2023, mbele ya mahakama hiyo, Hakima Nsana amesema kuwa baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, mahakama imewatia hatiani washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili.
"Kwa kuzingatia maombi ya mawakili wa upande wa washtakiwa, ikiwemo kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, utegemezi wa familia na ushirikiano mlioutoa katika kipindi chote cha uendeshaji wa kesi hii, mahakama inawapa adhabu ya kutumikia miaka 20 jela huku miezi 14 mliokuwa kizuizini ukizingatiwa," amesema
Mbali na hilo, washtakiwa wana haki na nafasi ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu endapo hawajaridhika na hukumu hiyo.
(Imeandikwa na Bertha Ismail)
#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
Huyu kama amekomeshwa
Umesoma vizuri? Miaka 20 toa miezi 14Kwahio ni miezi SITA TU?