Dkt. John Pima aliyekuwa DED Arusha na wenzake wahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Mama nipewe nafasi yoyote nipo radhi kufanya kazi 14hrs a day, punda mtwike mzigo najua utapitia hii comment ukiwa Zanzibar kwenye tamasha la kizimkazi. Kwenye kitengo tu ndio sichagui ila nachotaka niwe bize
 
Hakika hakuna anaejua kesho itakuwaje.

Godbless Lema huwa anasema sana huu msemo. Kesho ni ndefu sana.
Kesho yako ndiyo ndefu hao jamaa wanabebana kishenzi refer kesi ya sabaya
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na makosa ya uhujumu uchumi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Agost 31, 2023 na Hakimu Seraphin Nsana, katika kesi namba 5/2023 ya uhujumu uchumi, iliyokuwa inawakabili Dk. Pima, aliyekuwa Mweka Hazina wa jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi namba 5/2023, mbele ya mahakama hiyo, Hakima Nsana amesema kuwa baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, mahakama imewatia hatiani washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili.

"Kwa kuzingatia maombi ya mawakili wa upande wa washtakiwa, ikiwemo kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, utegemezi wa familia na ushirikiano mlioutoa katika kipindi chote cha uendeshaji wa kesi hii, mahakama inawapa adhabu ya kutumikia miaka 20 jela huku miezi 14 mliokuwa kizuizini ukizingatiwa," amesema

Mbali na hilo, washtakiwa wana haki na nafasi ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu endapo hawajaridhika na hukumu hiyo.

(Imeandikwa na Bertha Ismail)
#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
Hawatamaliza hata miaka miwili wanatoka baada ya kukata rufaa.
 
Kwa kuzingatia maombi ya mawakili wa upande wa washtakiwa, ikiwemo kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, utegemezi wa familia na ushirikiano mlioutoa katika kipindi chote cha uendeshaji wa kesi hii, mahakama inawapa adhabu ya kutumikia miaka 20 jela huku miezi 14 mliokuwa kizuizini...
Hiyo miezi 14 itapunguzwa kwenye hiyo miaka 20 ?.... anyway Ccm imemzamisha.
 
Hawa jamaa walijenga soko Moja kioja sana pale mbauda kwa gharama ya 1.4B... yaani pale kama walitumia sana pesa ni 200M, siku ya kulizindua... PM majaliwa alifika akapigwa na butwaa, akageuza msafara akagoma kulifungua akasema ni uchafu ule, akaamuru wakamatwe... Ndo kilichowafunga hao.... Ila ile pesa walipiga wengi tu Hawa ni mbuzi wa kafara
Ilikuwa mwaka gani?
 
Haya mambo ya uhujumu uchumi si walisema hayatakuwepo tena baada ya Magu kufa..mbona bado yanaendelea sasa?
Jiwe alifanya kwa uonezi, sema Mungu ndiye aliingilia kati tukanusurika
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na makosa ya uhujumu uchumi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Agost 31, 2023 na Hakimu Seraphin Nsana, katika kesi namba 5/2023 ya uhujumu uchumi, iliyokuwa inawakabili Dk. Pima, aliyekuwa Mweka Hazina wa jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi namba 5/2023, mbele ya mahakama hiyo, Hakima Nsana amesema kuwa baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, mahakama imewatia hatiani washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili.

"Kwa kuzingatia maombi ya mawakili wa upande wa washtakiwa, ikiwemo kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, utegemezi wa familia na ushirikiano mlioutoa katika kipindi chote cha uendeshaji wa kesi hii, mahakama inawapa adhabu ya kutumikia miaka 20 jela huku miezi 14 mliokuwa kizuizini ukizingatiwa," amesema

Mbali na hilo, washtakiwa wana haki na nafasi ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu endapo hawajaridhika na hukumu hiyo.

(Imeandikwa na Bertha Ismail)
#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
Hapakuwa na option ya fain hata ya 5ml
 
Back
Top Bottom