Dkt. John Pima aliyekuwa DED Arusha na wenzake wahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Dkt. John Pima aliyekuwa DED Arusha na wenzake wahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Miaka 20, maana yake watatumikia theluthi mbili ya miaka yao.

Mantiki hiyo ni kuwa Watatumikia miaka 13 na miezi kadhaa. Kwa kuwa wameshatumikia mwaka na miezi minne basi bado miaka 12 au chini ya hapo.

2023+12, watatoka 2035.

Ila hapo katikati wanaweza kuchomoka kwa msamaha wa Rais.

Kuna makosa hayana msamaha
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na makosa ya uhujumu uchumi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Agost 31, 2023 na Hakimu Seraphin Nsana, katika kesi namba 5/2023 ya uhujumu uchumi, iliyokuwa inawakabili Dk. Pima, aliyekuwa Mweka Hazina wa jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi namba 5/2023, mbele ya mahakama hiyo, Hakima Nsana amesema kuwa baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, mahakama imewatia hatiani washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili.

"Kwa kuzingatia maombi ya mawakili wa upande wa washtakiwa, ikiwemo kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, utegemezi wa familia na ushirikiano mlioutoa katika kipindi chote cha uendeshaji wa kesi hii, mahakama inawapa adhabu ya kutumikia miaka 20 jela huku miezi 14 mliokuwa kizuizini ukizingatiwa," amesema

Mbali na hilo, washtakiwa wana haki na nafasi ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu endapo hawajaridhika na hukumu hiyo.

Mwananchi
Fagio la chuma la Rais Mwinyi? Kuna watu bado wanadai tumehuru, ya nini kama mambo yako swafi kama hivi majambazi wanafungwa?
 
Halafu hizi du ova zako zinaboa hazikupi umaarufu jamiiforum mwanzo nilikuwa nakuona wa maana mtoto wa mjini ila umezidisha duova hadi unaboa maana huna constructive contribution yoyote ile kwasasa otherwise umaarufu umekufikisha kwenye Peter Principal huna jipya.
 
Kila kitu kila post wewe ni du ova du ova huu ni ushamba YANI ushajiona star jf
 
Mzee wa Kino ni kwamba huyo jamaa alikuwa kwenye inner circle ya JPM. Kiburi chake sio poa. Kwa Afrika lazima utawala mpya unapoingia madarakani ishughulikie baadhi ya watu. Hata Gambo bungeni harudi. Yule Gambo alishawahi waweka ndani watu waliokuwa wamejichanga kwenda kupeleka rambirambi kwenye msiba wa watoto wa Lucky Vicent. Aliweka utaratibu kuwa rambirambi zote zipitie kwake. Na katika aliowatia ndani kwa sasa baadhi ni vigogo wa awamu ya 6.
Duh!...Ila Ccm wanaweza kumpa tu cheo hata kama akikosa ubunge.
 
Duh!...Ila Ccm wanaweza kumpa tu cheo hata kama akikosa ubunge.
Kwenye siasa lolote linawezekana. Uliwahi kuota CHADEMA wangemteua mtuhumiwa wao mkuu wa ufisadi kuwa mgombea wao wa urais?
 
Halafu hizi du ova zako zinaboa hazikupi umaarufu jamiiforum mwanzo nilikuwa nakuona wa maana mtoto wa mjini ila umezidisha duova hadi unaboa maana huna constructive contribution yoyote ile kwasasa otherwise umaarufu umekufikisha kwenye Peter Principal huna jipya.
Jomba mbona unalialia sana? Hizo Ova zinakupunguzia nini kwenye maisha yako?
 
Back
Top Bottom