Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli akiwa Misungwi; Nimebaki mimi tu kwa sababu hamnipendi, hamjanipitisha bila kupingwa

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli akiwa Misungwi; Nimebaki mimi tu kwa sababu hamnipendi, hamjanipitisha bila kupingwa

Huyu mzee amechanganyikiwa hajui hata anachoongea na hana msimamo na anachoongea,yeye mwenyewe ndo anagawa watanzania .

Tumwogope sana hafai kabisa

1599554931899.png
 
Psychopath.....kichaa chake hakiponi.

Ewe Mwenye Enzi Mungu twakuomba hili dubwana usilipe nafasi ya kutwaa tena madaraka..Mimi huyu bwana nimemkataa na kamwe hatoweza pata kura yangu.

Mtu mzima akiwa MUONGO haipendizi,huyu mzee angekuwa uswahili wangewita mtu mzima hovyo.
 
Dkt. Magufuli asubuhi hii amefanya mkutano wa kampeni katika jimbo la Misungwi jijini Mwanza na kuwataka Watanzania tupendane.

Dkt. Magufuli amewasihi wananchi kutobaguana kwa misingi ya chama cha siasa, dini au kabila kwa mustakabali mwema wa taifa letu.

Kadhalika Dkt. Magufuli amewataka wanamisungwi kuchagua Rais, mbunge na diwani kutoka CCM ili waendeleze maendeleo yaliyo katika ilani ya uchaguzi.

Source: Channel Ten

Maendeleo hayana vyama!

==============

Rais Magufuli leo Jumanne anaendelea na kampeni za kuwania Urais na kuwanadi Wabunge na Madiwani wa chama anachokiongoza. Amepita Misungwi jimbo lilikuwa linaongozwa na waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Charles Kitwanga ambalo kwa sasa CCM ilimpitisha ndugu Mnyeti, Hii ni sehemu ya hotuba yake fupi.

DKT MAGUFULI: Ninachowaambia mimi niko nyumbani, ninawashukuru sana watu wa Misungwi mmepitisha mbunge bila kupingwa, mmepitisha madiwani bila kupingwa, hongereni sana. Nimebaki mimi tu kwa sababu hamnipendi, hamjanipitisha bila kupingwa, wangapi mtanipitisha bila Kupingwa? Asanteni sana.

Nataka nieleze ukweli, mlikuwa na mbunge hapa, Kitwanga alikuwa ananisumbua sana baadhi ya miradi. Ni lazima tujue historia ilikotoka, mahali tulipo na tunapoenda na Mnyeti atakuwa Mbunge.

Katika mipango ambayo imefanyika hapa ni mingi, hata hili barabara halikuwepo, katika kipindi cha miaka mitano tulilifanya na alienisumbua ni Kitwanga, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Nataka niyazungumze haya, bahati nzuri katika kazi zetu huwa sio za maisha. Palikuwa na Nyerere akamaliza muda wake, akaja Mwinyi akamaliza miaka yake kumi, akaja Mkapa akamaliza miaka yake kumi, akaja Kikwete miaka yake kumi na mimi mkitipisha hapa imebaki miaka mitano tu watakuja na wengine.

Hapa tuna mradi mkubwa wa maji ambao utagharimu bilioni 12 utakaonufaisha watu zaidi ya sitini na nne elfu.

Tumeanza vizuri, naomba mtuamini, naomba muendelee kuiamini CCM na hasa mnaona kazi nyingine ambayo inafanyika hapo Kigongo-Busisi, tunatengeneza daraja ambalo halijawahi kuonekana Tanzania na Afrika mashariki, daraja la kilomita 3.2.

Sasa msiache mkanichagua, yakaja mengine yakafuta haya mamiradi kwa sababu gharama ya daraja hili ni bilioni 699, bilioni 700 tunaziweka hapa. Ninachowaomba ndugu zangu wa Usagara na Misungwi endeleeni kushikamana, muwe wamoja. Haya mambo ya siasa yaliyokuwa yanawatenganisha myaache na bahati nzuri ndoa ya Mnyeti, alieiandaa ni Kitwanga.

MNYETI: Mheshimiwa Rais ni kweli kama ulivyosema, ndoa yangu aliiandaa mzee Kitwanga, namheshimu sana, nampenda sana siku zote.

MAGUFULI: Nampongeza Mnyeti kwa kushinda, nawapongeza waheshimiwa madiwani. Ninafahamu kuna appeal zitatokea tokea lakini tusubiri hilo ni kazi la tume pia nawapongeza wananchi wa hapa kwa kushikamana, maendeleo hayana chama.

Nina mke wangu nae nilimuoa Misungwi, mke wa Kitwanga hebu njoo hapa bwana.

MAMA JANETH MAGUFULI: Tunamuombea kura Rais, wabunge, madiwani, mtawachagua? Basi tunawashukuru sana asanteni.

MAGUFULI: Jamani nawapenda, nitakuja siku moja tufanye mkutano hapa.


Mbunge na Diwani hapo misungwi hawajapita kupingwa, wamepingwa sana tena mno hakuna mfano, huu utamaduni wa kishetani wa kupita bila kupingwa kwa njia haramu za hovyo ndiyo huzalisha wabunge wa CCM wagonga meza wa ndiyoo ndiyo kupitisha miswada ya hovyo, Sheria mbovu, mikataba ya hovyo hovyo kwa wingi wao Bungeni.
 
Hatumtaki Rais anayetegemea kupewa huruma kwa kuwa kapigwa risasi atauza nchi maana keshapata advance ili auze nchi
Hajakuomba huruma kwani hakukutuma ukampige risasi ukizani atakufa kisha urejeshe mfumo wa chama kimoja, CCM wakienda ulaya kuomba omba misaada kwa wazungu huwaita wafadhili wahisani lakini hao hao wazungu wakikataa upumbavu wao hugeuka na kuwaita wanaume wenzenu mabeberu utazani nyinyi CCM ni mbuzi jike.
 
Replica, Magufuli anajua pa kuanzia kampeni zake mfano katika miradi mikubwa aliyotekeleza na maendeleo kwa ujumla Sasa sijui wenzetu huwa wanaanzia wapi manake hawana reference.
Walipa kodi ndiyo reference yenyewe kama ulikuwa hujui kwani wapinzani na wananchi wasio na vyama ndiyo walipa kodi wazuri, wanaccm siyo walipa kodi bali wapo ni wafujaji wa pesa za walipa kodi, kuchukua pesa za viwanda kwenda kujenga chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge ni mojawapo ya matumizi mabaya ya kodi za wananchi.
 
Nchi ina miaka 59 haina maendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani, pesa nyingi inapotelea kwenye kudidimiza demokrasia kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi wapinzani na sasa kituko kipya cha kupita bila kupingwa ili wapate wabunge wengi waende kubadili katiba warejeshe mfumo wa chama kimoja ili mwenyekiti wa CCM atawale milele, CCM ya kishetani imejaa mbinu haramu zisizo na tija kwa Taifa, kuwapeleka wabunge huko Bungeni huku ukijua siyo chaguo la wapiga kura ni ushetani ulioje, mungu hapendi mtu akajiite ajibatize ni mwakilishi wa jimbo wakati hana ridhaa wala baraka za wapiga kura, tunaenda kuwa na wabunge wa ajabu Duniani ni vigumu kupiga hatua kimaendeleo katika mfumo huo haramu
 
Watumishi wapo na Lissu ataelewa tu.Na kuna watu wengi nyuma yao
 
Huyu Baba la Baba kachanganyikiwa.
Juzi jumapili kawafokea watu kwamba wakichagua upinzani watakoma. Hadi kabadilisha lugha ili wamuelewe.
Leo ana sema tusibaguane. Huyu mzee ana ndimi ngapi? Ni mtu wa kumuogopa sana
Laana ya uonevu kwa wapinzani inamtafuna ndiyo maana kapagawa
 
Wanaccm siyo walipa kodi bali wao ni wafujaji wa pesa za walipa kodi inayolipwa na wapinzani na watanzania wasio na vyama
 
Kampeni zimemuelemea, ifahamike hata alipokuwa mbunge alikuwa anapita bila kupingwa, hivyo hana uzoefu wa kushindana.
Nilijisikia hasira siku ile nimemsikia akiwatishia wapigakura kwamba wakichagua mpinzani watakiona, nilijiuliza hivi ni akina nani waliompigia yeye mpaka akawa rais 2015 ?, huyu jamaa hajui kabisa kuongea na hana sifa za kuwa kiongozi wa watu, kwa sababu uongozi wa watu unapaswa kureflect discipline na Utu
 
Back
Top Bottom