Consigliere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 12,037
- 24,637
Inawwzekana aiseeinategemea wewe unamuonaje,pengine wewe ndo hauko sawa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inawwzekana aiseeinategemea wewe unamuonaje,pengine wewe ndo hauko sawa.
Kwa kweli...Inawezekana ww unayemfatilia ndio umechanganyikiwa....!
Huyu mzee amechanganyikiwa hajui hata anachoongea na hana msimamo na anachoongea,yeye mwenyewe ndo anagawa watanzania .
Tumwogope sana hafai kabisa
Hatumtaki Rais anayetegemea kupewa huruma kwa kuwa kapigwa risasi atauza nchi maana keshapata advance ili auze nchiHahahahah! Huruma yako haimsaidii lolote.
Dkt. Magufuli asubuhi hii amefanya mkutano wa kampeni katika jimbo la Misungwi jijini Mwanza na kuwataka Watanzania tupendane.
Dkt. Magufuli amewasihi wananchi kutobaguana kwa misingi ya chama cha siasa, dini au kabila kwa mustakabali mwema wa taifa letu.
Kadhalika Dkt. Magufuli amewataka wanamisungwi kuchagua Rais, mbunge na diwani kutoka CCM ili waendeleze maendeleo yaliyo katika ilani ya uchaguzi.
Source: Channel Ten
Maendeleo hayana vyama!
==============
Rais Magufuli leo Jumanne anaendelea na kampeni za kuwania Urais na kuwanadi Wabunge na Madiwani wa chama anachokiongoza. Amepita Misungwi jimbo lilikuwa linaongozwa na waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Charles Kitwanga ambalo kwa sasa CCM ilimpitisha ndugu Mnyeti, Hii ni sehemu ya hotuba yake fupi.
DKT MAGUFULI: Ninachowaambia mimi niko nyumbani, ninawashukuru sana watu wa Misungwi mmepitisha mbunge bila kupingwa, mmepitisha madiwani bila kupingwa, hongereni sana. Nimebaki mimi tu kwa sababu hamnipendi, hamjanipitisha bila kupingwa, wangapi mtanipitisha bila Kupingwa? Asanteni sana.
Nataka nieleze ukweli, mlikuwa na mbunge hapa, Kitwanga alikuwa ananisumbua sana baadhi ya miradi. Ni lazima tujue historia ilikotoka, mahali tulipo na tunapoenda na Mnyeti atakuwa Mbunge.
Katika mipango ambayo imefanyika hapa ni mingi, hata hili barabara halikuwepo, katika kipindi cha miaka mitano tulilifanya na alienisumbua ni Kitwanga, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Nataka niyazungumze haya, bahati nzuri katika kazi zetu huwa sio za maisha. Palikuwa na Nyerere akamaliza muda wake, akaja Mwinyi akamaliza miaka yake kumi, akaja Mkapa akamaliza miaka yake kumi, akaja Kikwete miaka yake kumi na mimi mkitipisha hapa imebaki miaka mitano tu watakuja na wengine.
Hapa tuna mradi mkubwa wa maji ambao utagharimu bilioni 12 utakaonufaisha watu zaidi ya sitini na nne elfu.
Tumeanza vizuri, naomba mtuamini, naomba muendelee kuiamini CCM na hasa mnaona kazi nyingine ambayo inafanyika hapo Kigongo-Busisi, tunatengeneza daraja ambalo halijawahi kuonekana Tanzania na Afrika mashariki, daraja la kilomita 3.2.
Sasa msiache mkanichagua, yakaja mengine yakafuta haya mamiradi kwa sababu gharama ya daraja hili ni bilioni 699, bilioni 700 tunaziweka hapa. Ninachowaomba ndugu zangu wa Usagara na Misungwi endeleeni kushikamana, muwe wamoja. Haya mambo ya siasa yaliyokuwa yanawatenganisha myaache na bahati nzuri ndoa ya Mnyeti, alieiandaa ni Kitwanga.
MNYETI: Mheshimiwa Rais ni kweli kama ulivyosema, ndoa yangu aliiandaa mzee Kitwanga, namheshimu sana, nampenda sana siku zote.
MAGUFULI: Nampongeza Mnyeti kwa kushinda, nawapongeza waheshimiwa madiwani. Ninafahamu kuna appeal zitatokea tokea lakini tusubiri hilo ni kazi la tume pia nawapongeza wananchi wa hapa kwa kushikamana, maendeleo hayana chama.
Nina mke wangu nae nilimuoa Misungwi, mke wa Kitwanga hebu njoo hapa bwana.
MAMA JANETH MAGUFULI: Tunamuombea kura Rais, wabunge, madiwani, mtawachagua? Basi tunawashukuru sana asanteni.
MAGUFULI: Jamani nawapenda, nitakuja siku moja tufanye mkutano hapa.
Hajakuomba huruma kwani hakukutuma ukampige risasi ukizani atakufa kisha urejeshe mfumo wa chama kimoja, CCM wakienda ulaya kuomba omba misaada kwa wazungu huwaita wafadhili wahisani lakini hao hao wazungu wakikataa upumbavu wao hugeuka na kuwaita wanaume wenzenu mabeberu utazani nyinyi CCM ni mbuzi jike.Hatumtaki Rais anayetegemea kupewa huruma kwa kuwa kapigwa risasi atauza nchi maana keshapata advance ili auze nchi
Walipa kodi ndiyo reference yenyewe kama ulikuwa hujui kwani wapinzani na wananchi wasio na vyama ndiyo walipa kodi wazuri, wanaccm siyo walipa kodi bali wapo ni wafujaji wa pesa za walipa kodi, kuchukua pesa za viwanda kwenda kujenga chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge ni mojawapo ya matumizi mabaya ya kodi za wananchi.Replica, Magufuli anajua pa kuanzia kampeni zake mfano katika miradi mikubwa aliyotekeleza na maendeleo kwa ujumla Sasa sijui wenzetu huwa wanaanzia wapi manake hawana reference.
Kupita bila kupingwa ndiyo ushetani Hatari kwa usitawi wa demokrasia TanzaniaMission ya bila kupingwa kaianzisha yeye mwenyewe
Hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu atawapigia kura CCMWatumishi wapo na Lissu ataelewa tu.Na kuna watu wengi nyuma yao
Laana ya uonevu kwa wapinzani inamtafuna ndiyo maana kapagawaHuyu Baba la Baba kachanganyikiwa.
Juzi jumapili kawafokea watu kwamba wakichagua upinzani watakoma. Hadi kabadilisha lugha ili wamuelewe.
Leo ana sema tusibaguane. Huyu mzee ana ndimi ngapi? Ni mtu wa kumuogopa sana
Nilijisikia hasira siku ile nimemsikia akiwatishia wapigakura kwamba wakichagua mpinzani watakiona, nilijiuliza hivi ni akina nani waliompigia yeye mpaka akawa rais 2015 ?, huyu jamaa hajui kabisa kuongea na hana sifa za kuwa kiongozi wa watu, kwa sababu uongozi wa watu unapaswa kureflect discipline na UtuKampeni zimemuelemea, ifahamike hata alipokuwa mbunge alikuwa anapita bila kupingwa, hivyo hana uzoefu wa kushindana.