Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Bunda walijichanganya wenyewe, Utawapelekeaje Barabara watu wanaokutukana?

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Bunda walijichanganya wenyewe, Utawapelekeaje Barabara watu wanaokutukana?

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
“Bunda walijichanganya wenyewe, Ilani hii lengo kutengeneza Barabara kutoka kwa Lugola kule tukaunganishe na ukerewe kuja hadi Bunda baadaye tunaipasua hadi Serengeti lakini utawapelekeaje Watu wanaokutukana?, hata kama ni Malaika utagoma kidogo”

"Lakini utawapelekeaje watu wanaokutukana hata kama ni malaika utagoma kidogo. Mimi sio malaika nina roho na moyo na hata ukiwa na chakula kizuri huwezi ukampelekea mtoto wa jirani utampelekea mtoto wako wa kuzaa kama ana njaa" - Magufuli

Huyu jamaa asipoangalia anaweza kosa kura hata za wajinga anaowategemea

Maana sasa watu wanaanza kuona rangi zake halisi kuwa ni mtu Mwenye roho mbaya, chuki na visasi visivyo vya kawaida
 
Halafu utashangaa hao watu wanamlisha kwa kodi ya jasho lao.
Ukweli JPM amewakosea wana Mara, Amemkosea Mungu pia.

Pesa anazojengea barabara, kuleta maji, umeme nk hazitoki mfukoni mwake. Ni kodi ya wana Mara na Watanzania wote.

HAKI HUINUA TAIFA
 
View attachment 1559749
Huyu jamaa asipoangalia anaweza kosa kura hata za wajinga anaowategemea

Maana sasa watu wanaanza kuona rangi zake Hamisi kuwa ni mtu Mwenye roho mbaya, chuki na visasi visivyo vya kawaida
Ndie rais alie apa kuilinda katiba. Ana onyesha sura yake. Kwamba ana wa kifuani na wa mgongoni. Ni kiongozi wa Ccm huyu..
 
Sehemu pekee nchini Tanzania ambapo waweza kudhani Lissu atakuwa Raisi wa nchi hii ni Jamii Forums tu. Ila ukweli na uhalisia ni kwamba Lissu hatakaa awe Raisi wa Tanzania. Sio 2020 tu, ni NEVER (KAMWE)
 
Naona mnatumia JF kujipa moyo.Yaan hata kura mil 2 hampati.Pole sana ndugu

Umeona wanaongelea idadi ya kura hapo?
Hayo ni maneno ya kusemwa na kiongozi wa nchi? Kwanini kujitoa ufaham unaleta habari isiyohusika?

Nikikuuliza uchaguzi uliopita wapiga kura wangapi walijiandikisha, wangapi walipiga kura, idadi ya waliopata kila mgombea unaweza kuziweka kwa mlinganyo sawa ukapata majibu ya kueleweka? Ikiwa mwenyekiti wa tume mwenyewe alikiri makosa kwenye idadi wewe unaanzaje kuongelea kura 2M wakati hata sio hoja kwenye huu mjadala?
 
View attachment 1559749
Huyu jamaa asipoangalia anaweza kosa kura hata za wajinga anaowategemea

Maana sasa watu wanaanza kuona rangi zake Hamisi kuwa ni mtu Mwenye roho mbaya, chuki na visasi visivyo vya kawaida
Kweli ana hali mbaya ina maana hajui kama analishwa na kulishwa na kodi za watanzania wote ikiwemo hao anaosema watoto wa jirani naamini kweli hao anawahutubia ni mazuzu vinginevyo huwezi kuongea such a nonsense kwenye jamii ya watu wanaojitambua na wakaendelea kukushangilia.
 
Sehemu pekee nchini Tanzania ambapo waweza kudhani Lissu atakuwa Raisi wa nchi hii ni Jamii Forums tu. Ila ukweli na uhalisia ni kwamba Lissu hatakaa awe Raisi wa Tanzania. Sio 2020 tu, ni NEVER (KAMWE)
Huyo mgombea wenu sasa anawafanya hata wale wajinga waliokuwa wanam support kumgeuka.

Kwa haya maneno nawaambia mtashangazwa hiyo October 2020 mkiona Lissu anampiga vibaya huyu mtu wenu kwenye Sanduku la kura!!
 
Back
Top Bottom