Kuna tatizo gani asipokuwa rais? Nchi hii ina miaka 60 toka uhuru, na raia 59m+, idadi yote hiyo ya watu, ni watu watano tu wamekuwa marais. Hivyo hakuna tatizo kwani kwa ratio hiyo kuwa rais sio uwezo bali ni bahati. Tunachotaka ni ashindwe kihalali tu basi. Na uzuri kampeni hizi zimeonyesha kuwa ccm haina uwezo wa kushinda kihalali kwa kura zaidi vya 55%, na zama za ccm kuwa chama pekee zimeshapita na hazitakaa zirudi tena. Kinachofuata ni ccm kutolewa madarakani kwa amani, au kinyume chake muda si mrefu.