Huo ushindi wa kupewa na system Lisu hahitaji, Magufuli ndio anauhitaji ushindi wa mezani, maana hana ushawishi wala mvuto kwa wapiga kura. Tutampa Lisu kura zetu, yeye Magufuli angojee kutangazwa kwa mbeleko ya system. Ila hata hao system watajua kuwa enzi za ccm kutawala nchi hii zimeshapita. Na hao system waendelee kuomba wananchi kuwa makondoo, vinginevyo wakiamua kukaza kutatokea machafuko na mauji ya kutosha.
Ukitaka kujua ccm sio chama cha kizazi hiki, angalia ccm imefanya siasa miaka mitano peke yake, kila uchaguzi wameunajisi, lakini ndani ya mwezi tu, tayari watu wamerudi kwenye uhitaji wao wa mabadiliko. Peleka ujumbe huu kwenye vikao vya mboga mboga kuwa kila kitu kina kizazi chake, na ccm sio chama cha kizazi hiki bali cha kizazi kilichopita, ndio maana kinatumia nguvu kubwa kubaki madarakani, kuliko ushawishi wa kisiasa.