Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Sio hongo, mimi bado ni Rais, natangaza tenda ya barabara za mjini Itigi KM 10

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Sio hongo, mimi bado ni Rais, natangaza tenda ya barabara za mjini Itigi KM 10

Magu ni Raisi siyo waziri, anatoa maagizo popote pale ndo maana anatembea na yule mpambe wake mwanajeshi, ni icon ya nchi!
Na ndio maana hajavaa sare za CCM. Ndio wajue mzee yupo kazini anyatime
 
Nimekuelewa vizuri sana, nimekujibu kizembe kama wewe ulivyouliza kizembe. Mtu mjinga akiuliza swali la kijinga kwa mtu mwenye akili ukimjibu kistaarabu utaonekana wewe mjinga.

Sasa nakujibu alipokuwa kwa akili.

Bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 inaisha lini?
Utekelezaji wa Ilani ya CCM mwakak 2015 hadi 2020 unaisha lini?

Ukishajibu hayo maswali ndio utajua alipokuwa.
Hujanijibu swali langu! Nimekuuliza kama kulikuwa na haja ya kujenga hiyo barabara na alikuwa anajali sana alikuwa wapi mda wote na Mwaka wa fedha umeanza july hadi atoe iyo amri na hayo maagizo leo siku ya kampeni????
 
... tangu lini order ya peleka fedha pale; peleka kule hata kama ni utekelezaji wa bajeti ikatolewa kwenye majukwaa ya kampeni?
Unampangia pa kutolea order? Order ikitolewa mezani ndio inakuwa order?

Ishatoka hiyo, dawa inapenya taratibu mpaka itakolea
 
Nimekuelewa vizuri sana, nimekujibu kizembe kama wewe ulivyouliza kizembe. Mtu mjinga akiuliza swali la kijinga kwa mtu mwenye akili ukimjibu kistaarabu utaonekana wewe mjinga.

Sasa nakujibu alipokuwa kwa akili.

Bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 inaisha lini?
Utekelezaji wa Ilani ya CCM mwakak 2015 hadi 2020 unaisha lini?

Ukishajibu hayo maswali ndio utajua alipokuwa.
Mkuu hawawezi kukuelewa hawa chandimu! Kwa nyongeza hata Lisu akiwa Raisi (ila haiwezekani kabisa) ataendelea kutekeleza bajeti ya serikali ya ccm mpaka tar 31 June 2021!
 
Hujanijibu swali langu! Nimekuuliza kama kulikuwa na haja ya kujenga hiyo barabara na alikuwa anajali sana alikuwa wapi mda wote na Mwaka wa fedha umeanza july hadi atoe iyo amri na hayo maagizo leo siku ya kampeni????
Ikiwa uelewa wako ni mdogo au unajibu lako jaza hilo hilo ujipe tick.

Hiyo imetoka na pesa zitatoka. Tambua alichelewa alikuwa Chato
 
Ni mgombea bado Kama ye bado rais why anafanya kampeni. Raisi hawezi fanya kampeni.
Labda Ni Rahisi
 
Na bado kazi yao ilikua kumsifia tuu oooooo 2020 hakuna kampeni oooooo CDM tushaizika eti oooooooo wanakuja kuunga mkono hoja piga spana mpk wanataharuki
Aliyewapa wazo la kuunga juhudi Ni wazo la kishenzi Sana inatakiwa wamkamate awarudishie pesa yako,hili limekosa tija kabisa kwao halikuzaa matunda kabisa.Zaidi limechochea hasira pande zote kwa ccm na upinzani,cheki waunga juhudi kina katambi,waitara ,mollel walivyosusiwa kampeni na maccm wenzao,
 
Wewe kinakuuma nini,fanya yako jamaa utajiumiza bure na mambo ya siasa huna uwezo wa kumuzuia
 
Kama bado ni Rais, hivi Rais hawezi kutoa au kudai hongo hata ya ngono?
 
Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni na leo yuko Itigi mkoani Singida. Akiwa huko akaongelea uzuri wa nyumba za Singida na kusikitika zinavyopigwa vumbi ndipo ghafla akaitwa meneja wa Tanroad mkoa wa Singida mbele ya hadhara ya kampeni. Mazungumzo yao yalikuwa hivi.
=======


Dkt Magufuli: Ahadi yangu ya mjini ilikuwa kilomita 8 sasa ntatengeneza 10 pamoja na hii barabara niliyokuja nayo, nasema kwa dhati, sisemi kwa sababu ya kura. Nasema kwa sababu hii ni haki yenu.

Huu mji umependeza sana, mmejenga nyumba nzuri sana. Haiwezekani nyumba nzuri nzuri ziwe zinaendelea kupigwa mavumbi, nasema hapana kabisa lazima tutengeneze lami na mimi lazima niwaahidi ukweli. Mheshimiwa mkuu wa mkoa sijui yuko wapi? Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Singida hili ndio liwe la kwanza kushughulikiwa, asante sana.

Na regional manager wa Tanroads yupo au msaidizi wake? Njoo hapa, chukua mic

Dkt. Magufuli: Regional manager

Regional manager: Ndio mheshimiwa

Dkt. Magufuli: Pamoja na wa Tarura, nataka mkae hapa, kuanzia leo sisi tukiondoka.

Regional manager: Ndio mheshimiwa

Dkt. Magufuli: Mchague baadhi ya barabara zitakazotosha kwenye KM 10(Regional manager: Ndio mheshimiwa Rais).

Dkt Magufuli: Tangaza tenda mwezi huu, pesa usiulize, mimi nitatoa pesa kwa ajili ya kutengeza barabara hii. Itigi Oyee, (Wananchi: Oyee kwa shangwe). Kwa hiyo mjulishe chief executive wa Tanroard, mjulishe na waziri wa ujenzi, tunaanza mara moja, wala tusichelewe na hii wala sio hongo, mimi bado ni Rais kwa hiyo natoa maagizo. Tangaza tenda ya barabara za mjini Itigi kilomita 10, zitengenezwe kwa kiwango cha lami.

Regional manager: Ndio mheshimiwa Rais.

Dkt. Magufuli alifunga suala hilo na kuendelea na kampeni kwa kuelezea ubaya wa kugawa nchi katika majimbo na kuwataka wana-Itigi wawafundishe kwa kuwanyima kura wanaotaka kufanya hivyo.
Watanzania ni lazima wajifunze kuhusu kufanya uamuzi sahihi wa kumchagua kiongozi wa nchi aliye muadilifu na mwenye kuzingatia maadili. Haiwezekani ndani ya kipindi cha kampeni za uchaguzi zikiwa bado zinaendelea, mgombea kwa makusudi hataki kutofautisha kati ya majukumu yake ya uraisi na yale ya kupeperusha bendera ya chama chake.

Hiki si kitu kingine bali ni kiburi cha uzima na ulevi wa madaraka. Ndiyo! Haiwezekani mtu anakiuka kwa makusudi kanuni za uchaguzi zilizowekwa kisheria. Fedha za umma zina utaratibu rasmi wa kupangiwa matumizi yake, katiba haimpi Rais kuzitumia vile kama atakavyo, tena ili kujenga ushawishi wa kupata kura.

Nchi inaendeshwa kwa MBWA (Management By Walking Around) na wala si kwa MBO (Management By Objectives). Haya ndiyo mambo yaliyotupeleka ktk maamuzi tata ya fedha za umma mathalani ununuzi wa ndege kwa fedha taslimu, ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato, tenda ya Mayanga Construction na uozo mwingine kama huo.

Hapa ndipo hoja ya kuanzishwa kwa serikali za majimbo inapopata mashiko. Mathalani, tungelikuwa na Jimbo la Kiserikali la Nyanza, ni lazima bunge la jimbo lisingelikubali uwanja wa ndege ujengwe Chato. Inaelekea hii ndiyo sababu kubwa Mheshimiwa ya kuishikilia hoja ya muundo wa serikali za majimbo kuliko hoja nyingine yoyote ile.

Hapo yameguswa maslahi binafsi kwa kisingizio cha uzalendo. Anatambua uwepo wa serikali za majimbo utamfanya akose meno juu ya fuko la taifa la hazina ambalo anaamini yeye tu ndiye anao uhuru wa kulitumia kama mali yake binafsi.
 
Magufuli akishinda,hiyo miaka 5 ijayo tutalia na kusaga meno
 
Nimekuelewa vizuri sana, nimekujibu kizembe kama wewe ulivyouliza kizembe. Mtu mjinga akiuliza swali la kijinga kwa mtu mwenye akili ukimjibu kistaarabu utaonekana wewe mjinga.

Sasa nakujibu alipokuwa kwa akili.

Bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 inaisha lini?
Utekelezaji wa Ilani ya CCM mwakak 2015 hadi 2020 unaisha lini?

Ukishajibu hayo maswali ndio utajua alipokuwa.
Mkuu unataka haya maswali yako yajibiwe na huyu uliyemquote au tume ya uchaguzi na serikali waliotunga kanuni na sheria ya uchaguzi? Je unadhani waliotunga sheria na kanuni za uchaguzi unadhani hawakujua kuwa wakati wa kampeni kuna mtu atakuwa bado rais? Kama sasa hajui hizi sheria na kanuni zilitungwa ili mtu asitumie nafasi yake kuhararisha rushwa ili kugiribu wapiga kura.This incompetent individual inajificha kwenye urais ili kujustify uvunjaji wa sheria, kanuni na taratibu
 
Kwa hiyo unataka kazi za uraisi zisimame hadi uchaguzi upite? Katiba inamruhusu kuendelea na majukumu yake ya kiraisi hadi mpya atakapoapishwa
Acha kutetea mjinga,kazi za rais ni kuidhinisha pesa za ujenzi wa barabara au kupiga simu Tanroad wewe ni hovyo kama unae mtetea alivyo wa hovyo pia
 
Huyu mzee kwenye kujenga tu nampa salute angejirekebisha matatizo yake angekuwa rais bora sana
 
Sio rushwa ni utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu nliyopitishwa na bunge la june mwaka huu

Utekelezaji wa bajeti huwa hausimami kwa sababu ya uchaguzi

Hata bajeti ya tume ya mwaka huu wanayotumia ni iliyoidhinishwa na bunge la June
Sikiliza hii!

 
Back
Top Bottom