Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Vitambulisho vya Machinga sio lazima, acheni uongo

Ivi vitambulisho Kuna wafanyakazi za ofisi za umma walilazimishwa kuchukua na wengine kukatwa kwenye mishara yao , hapo mwaka jana lakini .
 
Leo anakana kila alichokiamuru[emoji23]
Kweli mwanakwetu kashikwa pasipozoeleka kushikwa!
Mkuu umenichekesha Sana na pia umenunikumbusha mbali Sana Bibi mkubwa wangu ni katibu mwenezi wa CCM kata ko ni mwana kada Sasa Kama unataka msielewane ongea vibaya Hawa nyoka wa kijani Sasa siku moja ikatokea skata moja hivi la mashamba wananyang'anya Bibi ambae pia ni mama yake sisi hatuishi huko tupo mikoa mingne na Bibi anaishi sehem nyingne na Mama sehem nyingne Sasa bi mkubwa akatupigia simu Mimi na bro akatuelezea sakata lilivyo Sasa bro yeye ni CDM ni sawa na Mimi tukamwambia Mama tatizo ni hao nyoka wenu wa kijani Mama akaanza kupanic tukasema ngoja Kwanza wamsumbue baadae atajua Sasa mzee yeye ni mtumish wa uuma inajikuta hachangii chochote ila na yeye ni mwana kada ila hajioneshi ko mzee akamsaidia
 
Na mbaya zaidi hela ya kuviuza hatuambiwi ilipatikana kiasi gani na imetumika kwenye nini??? Awamu ya Tano kuna ufisadi sana . Kinachosababisha usisike ni vitisho vya kutekwa, kupewa kesi na kupigwa risasi
May be they do not know that a Country is not a company
 
Ajabu wewe hapa peke yako ndo unamwelewa dikteta katika comments/replies 400, kwa hiyo tuseme katika watu 400, Magu ana kura yake 1, hujishangai?
 
Jana nimesikia mwanancji kuingiza fedha za kigeni nchini ruksa!
Bora tupunguze vipindi vya kufanya uchaguzi iwe kila baada ya miaka miwili ili mateso yasidumu kwa muda mrefu.
 
Nilienda ofisi za manispaa fulani, mkuu wa mkoa amekuja na wapambe wake wakiwemo mapolisi wanawatafuta maafisa biashara wamefunga ofisi wamekimbia, nikarudi mjini nikawakuta nikawambia mkuu anawatafuta wakasema hatuendi hadi aondoke, wakaenda kukopa
Pesa kwa mfanyabiashara fulani mwenye biashara kubwa ya Mpesa ili wakamkabidhi mkuu pesa halafu wakiendelea kuuza vutambulisho ndipo wakalipe deni kwa yule mfanyabiashara. Nikasema kweli kazi za serikali ni zaidi ya utumwa.
 
Ahaa! Lissu amekaba pabaya aisee! Kama vitambulisho hivyo sio lazima, kwanini wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi waliambiwa atakayeshindwa kuvimaliza ajuwe ameshindwa kazi? Tena ni amri hiyo ndio iliyopelekea baadhi wakuu wa mikoa kama yule wa Iringa kuanza kutaja kabisa makundi ya wafanyabiashara ambao lazima wawe navyo wakiwemo madereva wa bajaji ilihali wamiliki wao wameshalipia kodi TRA! Sehemu nyingine za vijijini watendaji walipita fremu moja ya duka hadi nyingine na kuamrisha hata mafundi viatu na washona ndala wanaolipwa TSHs 200 (miam bili) kwamba ni lazima walipe TSH 20,000 kuvinunuwa na kwamba ndio kibali cha shughuli yoyote kiuchumi! Sasa leo tunaambiwa tena haikuwa lazima!
 
Mh hivi vitambulisho vijijini ilifikia hatua hata mtu amebeba debe lake la mahindi kwenda kuuza anaulizwa kitambulisho.
 
Mh hivi vitambulisho vijijini ilifikia hatua hata mtu amebeba debe lake la mahindi kwenda kuuza anaulizwa kitambulisho.
Mimi walinifuata home wakaniambia una kuku zaidi ya 10 wewe ni mjasiriamali lazima uwe nacho. Nilikaza hadi mwisho
 
Vitambulisho ilikuwa ni shs 20,000/=.
Ma-RC na Ma -DC walipewa malengo ya kugawa kila mkoa na ndipo ikawa ni lazima wamachinga wote wawe navyo!
sasa hapo uongo uko wapi!
 
Wakuu wa wilaya na mikoa ufanisi wao unapimwa kwa mauzo ya hivyo vitambulisho pia.
Sijaona kipenger
le kuhusu hizo hela kwenye AG Report tangu vianzishwe au viko kwenye kasima ya Rais isiyokaguliwa????????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…