Dkt. Modestus Francis Kipilimba: Wasifu wake

Dkt. Modestus Francis Kipilimba: Wasifu wake

Angesomea intelligensia,cuba,usa uingereza na israel angekuwa na mauzoefu ya mosad,fbi na cia mi 6 and mi 5,ma kgb mwanawane ningemuona willy gamba lakin hapa mmmhh
Ila inawezekana ikawa alikuwa usalama toka mwanzo maana wapo watu wa usalama wanaofanyakazi kwenye taasisi mbalimbali
 
Nahisi uyu mkuu mpya nimemuona kwenye ile video ya kutangaza nia walikuwa wanaongelea mambo madini
 
Ni kweli usemayo lakini kwa upeo wangu mdogo alifaa ateuliwe miongoni mwa waliokaa kwenye idara hiyo na waliokubuhu ktk masuala ya upelelezi hasa ktk nyanja za kimataifa
Unajuaje kama hakuwa kwenye hayo majukumu?...TISS INA majukumu mengi
Ni kweli usemayo lakini kwa upeo wangu mdogo alifaa ateuliwe miongoni mwa waliokaa kwenye idara hiyo na waliokubuhu ktk masuala ya upelelezi hasa ktk nyanja za kimataifa
 
WASIFU MFUPI (CV) WA MKURUGENZI MKUU MPYA WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA, TANZANIA (TISS), DKT MODESTUS KIPILIMBA

Jina kamili ni Modestus Francis Kipilimba

Dini ni Mkristo

Ni mzaliwa wa Morogoro, Tanzania

Alifunga ndoa mwaka 1988, na ana watoto watatu.

Kuanzia Januari mwaka 1973 hadi Novemba mwana 1976 amesoma Shule ya Sekondari Kingonsera iliyopo Mbinga mkoani Ruvuma. Kidato cha 5 na 6 amesoma Mkwawa High School iliyopo mkoani Iringa. Shahada ya kwanza amesoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika masuala ya Kompyuta.

Shahada ya Uzamili (Masters Degree) alisoma nchini Uingereza katika chuo Salford, Manchester ambapo alisomea masuala la Kompyuta tangu Septemba 1992 hadi Novemba 1994.

Shahada ya Uzamivu (PhD) alisoma katika chuo hicho hicho cha Salford kilichopo Manchester Uingereza, kutoka Februari 2002 hadi Septemba 2005.

Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Tarehe 15 Februari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Dkt. Kipilimba alijaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dickson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Tarehe 24 Agosti, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Chanzo: Swahili Times
Duh! Nami nisome tuu huenda nikapata fursa
 
Hahaha, yaani hili jukwaa burudani kwelikweli! By thevway inakuwaje bosi usalama wa taifa hana mafunzo ya kijeshi, na kiusalsma kwa ubobezi kabisa? Au kuwa na utaalamu wa usalama wa computer dystems inatosha?
Mpaka kuchaguliwa ni kwamba ana mafunzo ya jwtz..jkt au kule chuoni kwao!!!
Na mengine yanafichwa kwa ethics za kazi yao!!!

Kwa nafasi kama iyo huwezi pewa tu...unapoongelea TISS ni zaid ya polis au jwtz!!!! Na inasemekana huyu jamaa ni pastor
Mtaalamu wa Computer na mambo ya usalama wapi na wapi
 
Back
Top Bottom