WASIFU MFUPI (CV) WA MKURUGENZI MKUU MPYA WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA, TANZANIA (TISS), DKT MODESTUS KIPILIMBA
Jina kamili ni Modestus Francis Kipilimba
Dini ni Mkristo
Ni mzaliwa wa Morogoro, Tanzania
Alifunga ndoa mwaka 1988, na ana watoto watatu.
Kuanzia Januari mwaka 1973 hadi Novemba mwana 1976 amesoma Shule ya Sekondari Kingonsera iliyopo Mbinga mkoani Ruvuma. Kidato cha 5 na 6 amesoma Mkwawa High School iliyopo mkoani Iringa. Shahada ya kwanza amesoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika masuala ya Kompyuta.
Shahada ya Uzamili (Masters Degree) alisoma nchini Uingereza katika chuo Salford, Manchester ambapo alisomea masuala la Kompyuta tangu Septemba 1992 hadi Novemba 1994.
Shahada ya Uzamivu (PhD) alisoma katika chuo hicho hicho cha Salford kilichopo Manchester Uingereza, kutoka Februari 2002 hadi Septemba 2005.
Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Tarehe 15 Februari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Dkt. Kipilimba alijaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dickson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Tarehe 24 Agosti, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Chanzo: Swahili Times