Dkt. Modestus Francis Kipilimba: Wasifu wake

Dkt. Modestus Francis Kipilimba: Wasifu wake

Mbona sijaona uzoefu wake WA KI TISS TISS? au nitaitwa mchochezi? ACHA niishie Hapo nisije nikazolewa hapa nyuma ya kibodi, upepo umesha chafuka
Rais wako ni amiri jeshi mkuu, mbona hana hata 'rank' moja ya JW?
Unavijua vigezo vinavyoangaliwa kumpata 'MKURUGENZI' wa usalama wa taifa? Unajua advantage ya IT kama moja ya vigezo? Karne ya 21 usalama wa taifa sio mitulinga peke yake na nimefurahi sana rais wetu kuling'amua hilo!
 
Bosi wa usalama anapsswa kuwa mwanajeshi aliyebobes kwenye mbinu mbalimbali za medani na usalama wa nchi!
Hivi wewe kwa akili yako unafikiri mbinu za medani kitaaluma inafikia hata muhula mmoja wa kozi yeyote ya sayansi kwa ngazi ya chuo kikuu?
NB: Pamoja na kuzisoma darasani, mbinu za medani zinatungwa kila siku na watu wenye maarifa wanaoajiriwa jeshini ambao hugundua madhaifu ya mbinu zilizopo!
 
Mara nyingi bigboss wa usalama sio lazima awe anatokana na wanausalama,wanaomenyeka ni kuanzia madeputy,hao ndo lazima awe anajua na amesomea hasa hiyo kazi,
Director huwa ni uteuzi wa kisiasa zaidi kama sikosei
 
Condoleeza Rice aliwahi kuwa mshauri wa mambo ya usalama wa Rais wa marekani (Kipindi cha kwanza cha Bush mdogo) ilhali hajawahi kuwa mtu wa ujasusi au mtu aliyepitia jeshii...

Kilichompa kiki sana ni uelewa wake mkubwa sana wa mambo ya soviet ambayo ndiyo aliyafanyia masomo yake ya shahada ya uzamivu. Huyu mwanama walimtumia sana katika kuelewa jinsi ya ku deal au kunegotiate na warusi mpaka ikafikia hatua ya kuumaliza ukomunisti USSR.

Usalama unahusu sera, mipango, mikakati, maamuzi, jiographia ya siasa za kikanda, na mambo mengine..Kwa hiyo tuache porojo porojoo tuangelee tunayoyayeelewa zaidi tusijifanye wajuaji kwenye yale tusiyoyaelewaa..

Chukua clip moja umuone mkurugenzi wa usalama wa kwa Zuma umsikie vitu anavyoongea ndo utafahamu bosi wa usalam kwenye karne ya ishirini na moja anapaswa awe vipi..

Anaongelea mambo ya kushauri kuhusu sera na mahusiano na nchi zingine na pia fursa za kiuchumi kwa nchi n.k. Wengi wakisikia usalama wanapata tu picha za james bond. Kumbe hayo mambo ni ya field tu wakati wa kukusanya taarifa.

Taarifa zikikusanywa zinapaswa kuchambuliwa na watu ambao wapo vizuri kichwani. Na katika uchambuzi IT inaweza kuwa na msaada mkubwa sana...
 
Sijaelewa Lengo la Kamwaga kuandika kwa kirefu hivi bola kuonyesha mapungufu hata kidogo..... Waandish wa Tanzania hapo ndipo wanapoitwa "waandish njaa"
Anyway, tusubiri tuone utendaji kazi wa kisasa na kizalendo kwa manufaa ya nchi bila kumuonea mtu.
 
Tunashukuru sana na upo sahihi,Sasa huyu Dr Kipi tumuombee kwa Mungu afanye kazi yake kwa weledi.

Pia sisi watanzania tuwe kama Israel,kila mtu awe TISS wa kujitegemea.
Ukiona adui ripoti polisi,kwa mjumbe,balozi nyumba kumie etc
 
Kila Zama na kitabu chase, kila Masika na Mbu wake!

Othman Rashid Mkurugenzi Mstaafu alifanana sana na Dr. Kikwete kwa umjini mjini na Mambo ya ujana ujana na ndio sababu walivushana salama October 25, 2015 Ngoja tuone hii chemistry ya Dr Magu na Dr Kipilimba
 
Naomba kuuliza: Hivi kuandika personal info za mtu bila written permission siyo kosa?

Kama maofisini kutoa numba ya simu ya mtu bila ruksa yake ni kosa hao waliokupa details zake zidhani kama wamefanya vyema haijalishi mna mahusiano nao kiasi gani, hapo kuna tatizo.

Tatizo kila mtu siku hizi eti anajua mambo ya usalama kisa kuna materials online, kama yamewekwa online inamanisha mambo yamebadilika kuna techniques nyingine. Haujui unawarahisishia kazi wanaotafuta info from "open source"?

Tujifunze kuchuja kabla ya kuandika, watanzania tupunguze kuongea ongea hata tunapotakiwa kukaa kimya. Kama unajua mambo ya usalama naamini unajua kwamba haichukui siku kulocate ulipo na kukupata.

"Learn to use the power of being silent".
 
Kulingana na maelezo yako The guy looks smart! kila la heri
 
Back
Top Bottom