Kwa ufupi mtu huyu alikuwa Ofisa wa Juu wa Usalama wa Taifa , DG wa TISS , kabla ya hapo alitokea kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Kwa sasa ni Balozi , kimsingi balozi ni mtumishi wa Umma kama mabalozi wengine akina Dr Slaa , Polepole na Mwanaidi Majaar .
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania si kosa kutaka kumfahamu mtumishi yeyote wa Umma , kwa lengo la kutaka kujua uaminifu wake na kutaka kujua kote alikopita na hata shule alizosoma , elimu yake , uhusiano wake na jamii na mengine lukuki .
Alianza lini kazi usalama wa Taifa , aliletwa na nani , kwanini aliletwa Tume ya Uchaguzi dakika za mwisho kabla ya uchaguzi mkuu 2015 , alisaidia nini hadi kutunukiwa U DG wa TISS ?
Naomba kuwasilisha .