#COVID19 Dkt. Mollel: Askofu Gwajima ataitwa athibitishe kauli zake, akishindwa tutamshughulikia

Siku za nyuma issue ya Covid ilikuwa na wasemaji wake, nadhani ili tuende sawa ipo haja ya Serikali kuteua wasemaji wa hii issue otherwise tutaendelea kulumbana kila mtu na lwake.
Kama chanjo ni suala la binafsi ya mtu kuamua si sawa kwa yeyote kuvutia upande wake.
Kwa lugha nyepesi ni kuwa Covid sio suala la kakikundi kokote ka watu bali iwe ni National issue kwa kuzingatia takwa la mtu na asitokee yeyote kuwapoteza maboya wenzake.
 
Hapa hakuna dini na 666 niliyongelea labda unaninyatia.
Kwenye hii post yangu uliyo ni qoute sijazungumzia dini wala 666 labda umechanganya mambo wakati unaninyatia.

Muulize DR Mollel nani atawajibika kama ikigundulika watakuwepo Watanzania wamepoteza maisha sababu ya chanjo. Ni mjinga tu asiye jua kwa nini anasanishwa hati ya kujihukumu kifo na jamaa zake wasipate nafasi ya kumuwajibisha yeyote.

Wao hawataki kuwajibika kwa madhara yatokanayo na chanjo lakini wanataka kumuwajibisha mtu angalau anaye jaribu kuwa na roho ya utu, huruma na upendo kuwatahadharisha wanao iendea chanjo yenye walakini mwingi.

Katika chanjo zote zilizowahi kuwepo duniani ipi nyengine ambayo Watanzania walishasainishwa hati ya kujitoa muhanga kwa chanjo? Ili hii ya corona iwe ni muendelezo?
 
Au basi tu nisiandike

#chanjo ni hiari
#waliochanjwa hawataishi milele inabidi wajue hilo.
 
Mollell ni phaller flani, tumesoma naye Minaki high school japo alinitangulia kidato kimoja, amesoma akiwa mzee na alikuwa hajui kiswahili vizuri, huyo ni boya hakuna mfano
Yeye Ni naibu Waziri,we Ni Nani?
 

..Nadhani wamenywea.

..hawana mazoea ya kuchelewa namna hii kuchukua hatua.

..Na jumapili ijayo atawashambulia tena.
 
Hi
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Mollel amesema kuwa mchungaji Gwajima sasa kapitiliza kwa kuwapotosha Watanzania.

Kwa ufupi pitia kwenye bandiko lake hapa chini ili kujionea alicho ongea.

View attachment 1894702
Hivi huyo Mollel ndiyo nani?? Hivi mtu anayebadilisha kauli kulingana na mwelekeo wa awamu husika he is a serous liability to our country!! Anapaswa ajiuzulu kwa sababu hawezi kuyasimamia yale aliyokuwa anayapinga hadharani!! na sasa anajifanya anayaunga mkono!! Yeye na boss wake ni wasanii wa kufa mtu!
 
Kwamba zile chanjo zina chip?
 
Mdahalo uwekwe live najua gwajima atashinda na selikal iweke wazi waliochomwa na waangaliwe kwa miaka 2 akifa hata mmoja tayar kesi closed gwajima anakuwa ameshinda
Na ambao hawajachoma wakifa seikali itakuwa imeshinda? Nani kakwambia chanjo ya Corona Ni kwa ajili ya kuzuia kifo?
 
Naanza kupata mwanga hii sheria na taratibu mpya za kusajili Taasisi za dini kila baada ya miezi 6 nadhani ilimlenga gwajima. Wanataka wamuweke mtu kati gwajima the bold nad brave.
Kanisa lake likitishiwa kutosajiliwa Gwajima ataendelea kuwa strong au atanyoosha mikono ju?
 
Dr. Mollel mpaka hapo, tunaweza kusema kachokonoa nyuki ndani ya mzinga wao wakati wa mchana wa jua kali bila kuwa na kinga ya kujizuia wasimuume...

Nimesikiliza video yake mwanzo mwisho. Kuna mahali kamwita Mch. Gwajima "mjinga pamoja na wajinga wenzie wengine - akimaanisha wanaopinga chanjo na pengine na waumini wote wa kanisa la ufufuo na uzima"...

Na hapa maana yake, katukana jamii yote ya Ufufuo na Uzima na hakika HATABAKI SALAMA huyu...

Sina shaka kuwa, yeye Dr. Mollel na waliomtuma kuchokoza nyuki, watapata majibu yao kesho tu toka kwa Mch. Gwajima maana alishasema, yeye huwa ukimbipu, basi anakupigia hapohapo bila kuchelewa;

Alishasema, ukimchokoza anakufyatua bila kuchelewa...!!

Stay tuned...
 
Your browser is not able to display this video.


Gwajiboy atamfuta kazi Mollel muda si mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…