Dkt. Mollel: Ni ujinga Waziri kutoa Data za Walioathiriwa na Corona kila siku. Bei ya chanjo ni Tsh 400,000

Dkt. Mollel: Ni ujinga Waziri kutoa Data za Walioathiriwa na Corona kila siku. Bei ya chanjo ni Tsh 400,000

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Jinsia Wazee na Watoto amesema watu wengi wanasema Tanzania haitoi data, ambapo amesema data haina haja ya kutangazwa kila siku na Waziri, utakuwa ni ujinga mtupu.

Amesema Data huwa inataka uchakataji ili kujua tatizo ya magonjwa yanayosababisha vifo na kujua namna ya kuyakabili.

Kwa kipindi cha karibuni kumekuwa na taharuki ambayo imesababisha kila anayefariki kupakaziwa amekufa kwa #CoronaVirus hivyo inahitajika uchakataji kujua waliopakaziwa

Amesema ili kutoua watu, mtu akienda hospitali huwa wanasema ana matatizo ya kupumua ili kwanza kujua kama anashindwa kupumua kwa tatizo la presha, nimonia, sukari au bakteria.

Msikilize:

 
Yuko sahihi, kwani kuto kutanganza data hadharani pia ni mbinu mojawapo ya kupambana na matatizo ya Corona.

Sio kila mtu mwenye changamoto ya upumuaji basi ana zushiwa kuwa anaumwa corona, bali matatizo ya upumuaji yanaweza pia kusababishwa na magonjwa ya moyo, pumu, nimonia, sukari, n.k.

ni vyema wagonjwa wote wenye magonjwa sugu na ambao wanapaswa kuhudhuria kliniki wafanye hivyo badala ya kubaki nyumbani.

Lengo ni kuokoa maisha ya watu wote na haswa wenye changamoto sugu za kiafya na sio kuwatisha kwa matangazo ya vifo.
 
Walipoenda kusaini mikataba na WHO kuhusu takwa la ku-share data inapotokea ugonjwa wa mlipuko unaotishia maisha ya watu hayo hawakuyajua.

Au WHO wanahimiza vitu ambavyo hawana uhakika navyo?

Tangu mwezi wa tano wao wanachakata tu?

Epidemiology alisoma peke yake tu?
 
Yuko sahihi, kwani kuto kutanganza data hadharani. sio kila mtu mwenye changamoto ya upumuaji basi ana zushiwa kuwa anaumwa corona, bali matatizo ya upumuaji yanaweza pia kusababishwa na magonjwa ya moyo, pumu, nimonia, sukari, n.k.
Kipindi kile wanatoa daily data as per global SOPs za kupambana na maradhi ya milipuko walikuwa wanatangaza idadi ya watu waliothibitika kuugua corona baada ya vipimo.

Hawakuwa wanajitangazia figures tu za kila mtu aliyeenda hospital akikohoa au kuumwa kichwa au kubanwa pumzi.
 
Comedians!

90876541.jpg
 
Statistics zinasaidia kujua ukubwa wa janga, umri gani wameathirika zaidi na walindwe vipi. Kama ugonjwa utaendelea basi litakua na ukubwa gani na watu wangapi wanakadiriwa kuupata na Serikali isaidie vipi. Hili ni janga la dunia we owe this to the world. Lazma ije isemwe this tragedy claimed how many lives, dunia ilijikingaje na inaelekea kuumaliza vipi.

Je unadhani zile chanjo za polio na kifua kikuu zinakuja kiholela? Wanakadiria nchi kwa mwaka wanazaliwa wangapi, wangapi wanakadiriwa kupata chanjo na ugonjwa umeshuka kwa kiasi gani??

Kwani statistics za waliokufa kwa malaria mamilioni kwa dunia nzima kuna mtu anaamka tu halafu anaitaja??? In general statictics zinakusaidia pia wewe na Serikali yenu mtapewa msaada wa chanjo kwa kiasi gani.
 
Walipoenda kusaini mikataba na WHO kuhusu takwa la ku-share data inapotokea ugonjwa wa mlipuko unaotishia maisha ya watu hayo hawakuyajua.

Au WHO wanahimiza vitu ambavyo hawana uhakika navyo?
Mbowe na genge lake ndio waliosaini mkataba wa WHO.
 
Back
Top Bottom