Dkt. Mpango awataka watumishi fedha kujihadhari na Corona

Dkt. Mpango awataka watumishi fedha kujihadhari na Corona

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango, amewataka watumishi wa wizara hiyo kuchukua tahadhari zote kuhusu ugonjwa wa corona, licha ya kukiri kuwa Tanzania haina maambukizi ya virusi hivyo kwa sasa.

Dk Mpango alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Mkutano huo ulifanyika jana katika ukumbi wa Kambarage uliopo jijini Dodoma.

Waziri Mpango alisema ugonjwa huo haupo nchini, lakini umeendelea kuitikisa dunia na kuyumbisha uchumi wa nchi nyingi.

“Tumshukuru Mungu ugonjwa huu umetupisha mbali hapa nchini kwetu, lakini niwasihi watumishi tuendelee kuchukua tahadhari zote kama tunavyoelekezwa na wataalamu wetu wa Wizara ya afya,” alisema.

Awafunda wafanyakazi

Aidha, Dk Mpango aliwagiza viongozi wa baraza hilo kufikisha ujumbe kwa wanaowaongoza, watende kazi kwa kufuata miongozo na kutotoa siri za Serikali.

Alisema watashughulika na watendaji watakaobainika kuvujisha siri za Serikali.

Katika hatua nyingine Dk Mpango aliwaagiza watumishi katika wizara hiyo kutobweteka kutokana na Tanzania kuingia katika uchumi wa kati.

Alisema wanapaswa kutambua kuwa bado wana safari ndefu ya kuipeleka nchi katika mafanikio zaidi.

‘‘ Hakuna maana kwa wizara kuwa na msururu wa wafanyakazi ambao hawatimizi wajibu wao bali kila mmoja ajione kuwa na thamani mahali pake na watenge muda wa kusikiliza matatizo ya walio chini yao,’’ alisema.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, alitaja lengo la mkutano huo ni kuchagua viongozi na kujadili namna ya kuboresha utendaji kazi.

James alisema maboresho ya mazingira ya watumishi yataendana na kuboresha mazingira ya kazi ili kufanya watu wawe na afya njema na kuendelea kuchapa kazi inavyotakiwa.

Akitoa neno la shukrani, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mary Maganga aliahidi kuwa maagizo ya Waziri yatazingatiwa na kwamba watayashusha kwa watendaji wa ngazi ya chini ili utekelezaji uanze mara moja.

Source Mwananchi
1611669221037.png

Muda utaongea tu
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewataka watumishi wa Wizara ya hiyo kuchukua tahadhari za ugonjwa wa korona, licha ya kukiri kuwa Tanzania haina maambukizi ya virusi hivyo kwa sasa.

7E6A56FF-8DE8-4A80-B902-C5E3123206DE.jpeg
 
Hii corona mbona ilikuwa imesahaulika kabisa toka may 2020 ni kipi kimeiibua kwa speed kiasi hiki au kuna aina mpya ya kirus imetua bongo.

Ngoja tusubiri tuone kama Jiwe atakaa Chato miezi miwili kama kipindi kile cha mpaka papai lina Corona aah kaka tuchati
 
Hii corona mbona ilikuwa imesahaulika kabisa toka may 2020 ni kipi kimeiibua kwa speed kiasi hiki au kuna aina mpya ya kirus imetua bongo.Ngoja tusubiri tuone kama Jiwe atakaa Chato miezi miwili kama kipindi kile cha mpaka papai lina Corona aah kaka tuchati
Mwezi wa 12 Ndege zimeleta wageni wengi Tanzania tokea Nchi zenye maambukizi makubwa ndiyo maana corona imepamba moto zaidi mpaka mtukufu akaamua kukimbilia chato kujificha huko
 
Siku sio nyingi wote watanena lugha moja, hongera kwake kaamua kutoka ndotoni, intellectuals wa kweli ndio wanatakiwa kuwa hivyo.

Bosi wao mwenyewe kahamishia makazi Chato sidhani kama amependa kufanya hivyo, hali hairuhusu..

Tujihadharini wajomba.
 
Eheeee we mpango wewe utatumbuliwa wewe.... nani kakuambia kuna korona bongo
We haya tu
 
Waziri wa fedha kauli yake hubeba uzito mkubwa.

Huyu aliapishwa siku moja na wakati mmoja na sehemu mija na waziri mkuu!
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewataka watumishi wa Wizara ya hiyo kuchukua tahadhari za ugonjwa wa korona, licha ya kukiri kuwa Tanzania haina maambukizi ya virusi hivyo kwa sasa.

View attachment 1686394
Huyu anatuchanganya Kama hakuna ugonjwa huo kwa Nini anatahadharisha.hapa anamainisha Nini wadau wenzangu?
 
Back
Top Bottom