Dkt. Mpango awataka watumishi fedha kujihadhari na Corona

Dkt. Mpango awataka watumishi fedha kujihadhari na Corona

Kama hakuna tahadhari ya nini?
Kila mmoja anajua hupo, pia hayuko alie tayari kubainisha uwepo wa Covid-19, woga, kutojihamini, hivyo wanasema kimtindo, ila waziri wa fedha aruhuwi kuzungumzia Covid-19!
 
Ukitaka kujua umuhimu wa kuvaa barakoa, nunua Juis au matunda, kesho upite ward 3 na 4 pale Mwaisela Muhimbili. Walinzi wakikuuliza waambie Kuna mgonjwa unampelekea chakula. Trust me utamuelewa Dr Mpango na utazingatia ushauri wa Baraza la Maaskofu katoliki.
R.I.P Paroko wa Mwananyamala.
 
Umepiga mule mule Mkuu.
Mwezi wa 12 Ndege zimeleta wageni wengi Tanzania tokea Nchi zenye maambukizi makubwa ndiyo maana corona imepamba moto zaidi mpaka mtukufu akaamua kukimbilia chato kujificha huko
 
....., licha ya kukiri kuwa Tanzania haina maambukizi ya virusi hivyo kwa sasa....

Hawa watu ni waongo Mpka shetani (Lucifer) anawashangaa.
 
Yaani hao Jamaa wameleta Ndege kuchukua raia mmoja?
Wanajali uhai kuliko mali. Sisi tunajali mali kuliko uhai, ndio maana tunasisitizwa kuchapa kazi hata kama tupo kwenye lindi la maambukizi.
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango, amewataka watumishi wa wizara hiyo kuchukua tahadhari zote kuhusu ugonjwa wa corona, licha ya kukiri kuwa Tanzania haina maambukizi ya virusi hivyo kwa sasa.

Dk Mpango alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Mkutano huo ulifanyika jana katika ukumbi wa Kambarage uliopo jijini Dodoma.

Waziri Mpango alisema ugonjwa huo haupo nchini, lakini umeendelea kuitikisa dunia na kuyumbisha uchumi wa nchi nyingi.

“Tumshukuru Mungu ugonjwa huu umetupisha mbali hapa nchini kwetu, lakini niwasihi watumishi tuendelee kuchukua tahadhari zote kama tunavyoelekezwa na wataalamu wetu wa Wizara ya afya,” alisema.

Awafunda wafanyakazi

Aidha, Dk Mpango aliwagiza viongozi wa baraza hilo kufikisha ujumbe kwa wanaowaongoza, watende kazi kwa kufuata miongozo na kutotoa siri za Serikali.

Alisema watashughulika na watendaji watakaobainika kuvujisha siri za Serikali.

Katika hatua nyingine Dk Mpango aliwaagiza watumishi katika wizara hiyo kutobweteka kutokana na Tanzania kuingia katika uchumi wa kati.

Alisema wanapaswa kutambua kuwa bado wana safari ndefu ya kuipeleka nchi katika mafanikio zaidi.

‘‘ Hakuna maana kwa wizara kuwa na msururu wa wafanyakazi ambao hawatimizi wajibu wao bali kila mmoja ajione kuwa na thamani mahali pake na watenge muda wa kusikiliza matatizo ya walio chini yao,’’ alisema.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, alitaja lengo la mkutano huo ni kuchagua viongozi na kujadili namna ya kuboresha utendaji kazi.

James alisema maboresho ya mazingira ya watumishi yataendana na kuboresha mazingira ya kazi ili kufanya watu wawe na afya njema na kuendelea kuchapa kazi inavyotakiwa.

Akitoa neno la shukrani, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mary Maganga aliahidi kuwa maagizo ya Waziri yatazingatiwa na kwamba watayashusha kwa watendaji wa ngazi ya chini ili utekelezaji uanze mara moja.

Source Mwananchi
View attachment 1686739

Muda utaongea tu

Inasikitisha Phd holder anapoongea upumbavu
 
Mie Niko tofauti na wengine.

Why watumishi Wa fedhaa pekee INA mana ndo anaowapenda Sie tusio watumishi Wa fedha inakuwa je ivi,tusio na ajira tumekaa tu home ni kuchati inakuwa je ivi.
Haya labda wao ndo wako covid prone alone
Jiongeze hapo sio kila kitu uambiwe!
 
Back
Top Bottom