Dkt. Mpango awataka watumishi fedha kujihadhari na Corona

Dkt. Mpango awataka watumishi fedha kujihadhari na Corona

10126120311.jpg
 
Yaani hao Jamaa wameleta Ndege kuchukua raia mmoja?
Uhai wa mtu unathamani kwa wenzetu...haijalishi nafasi yako au cheo chako..Norway walituma ndege Kenya kumchukuwa raia wao tena ni msomali ilimradi tu ana passport yao. Sisi kazi kupenda viongozi wetu na wao hawatupendi wanapenda familia zao.
 
Kama hakuna tahadhari ya nini?
Hii Corona lazima itaondoka na mtu hivi karibuni .....

Boss kesha sema hakuna Corona wao wanang'ang'ania kila siku kuwaogopesha wananchi.

Boss alishasema hofu ni mbaya kuliko Corona yenyewe .... sasa sijui kwa nini wanatutisha wananchi!!
 
Kama sisi hatuna na wote waliotuzunguka, wanao anataka watumishi wake wachukue tahadhari zipi zaidi ya yeye na serikali yake kuhakikisha ulinzi wa mipakani ili isiingie ?

Au ni mimi ndio sio mwelewa ?
 
Inatakiwa wajikinge maana wanapokea wageni kutoka nje ya nchi
 

Dk Mpango ataka watumishi fedha kujihadhari na corona​

TUESDAY JANUARY 26 2021​


mpangopic

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango


By Habel Chidawali

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango, amewataka watumishi wa wizara hiyo kuchukua tahadhari zote kuhusu ugonjwa wa corona, licha ya kukiri kuwa Tanzania haina maambukizi ya virusi hivyo kwa sasa.


Dk Mpango alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Mkutano huo ulifanyika jana katika ukumbi wa Kambarage uliopo jijini Dodoma.

Waziri Mpango alisema ugonjwa huo haupo nchini, lakini umeendelea kuitikisa dunia na kuyumbisha uchumi wa nchi nyingi.

“Tumshukuru Mungu ugonjwa huu umetupisha mbali hapa nchini kwetu, lakini niwasihi watumishi tuendelee kuchukua tahadhari zote kama tunavyoelekezwa na wataalamu wetu wa Wizara ya afya,” alisema.

Awafunda wafanyakazi

Aidha, Dk Mpango aliwagiza viongozi wa baraza hilo kufikisha ujumbe kwa wanaowaongoza, watende kazi kwa kufuata miongozo na kutotoa siri za Serikali.

Alisema watashughulika na watendaji watakaobainika kuvujisha siri za Serikali.

Katika hatua nyingine Dk Mpango aliwaagiza watumishi katika wizara hiyo kutobweteka kutokana na Tanzania kuingia katika uchumi wa kati.

Alisema wanapaswa kutambua kuwa bado wana safari ndefu ya kuipeleka nchi katika mafanikio zaidi.

‘‘ Hakuna maana kwa wizara kuwa na msururu wa wafanyakazi ambao hawatimizi wajibu wao bali kila mmoja ajione kuwa na thamani mahali pake na watenge muda wa kusikiliza matatizo ya walio chini yao,’’ alisema.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, alitaja lengo la mkutano huo ni kuchagua viongozi na kujadili namna ya kuboresha utendaji kazi.

James alisema maboresho ya mazingira ya watumishi yataendana na kuboresha mazingira ya kazi ili kufanya watu wawe na afya njema na kuendelea kuchapa kazi inavyotakiwa.

Akitoa neno la shukrani, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mary Maganga aliahidi kuwa maagizo ya Waziri yatazingatiwa na kwamba watayashusha kwa watendaji wa ngazi ya chini ili utekelezaji uanze mara moja.
 
Mfano hai ni huu kuwa Covid-19 imeingia tena awamu ya pili kivingine, kuficha na kuhadaa watu ni jambo baya.

Ona bandeji ktk mkono wa mgonjwa anayepandishwa ndege maalum ya ambulance baada ya kutundikiwa drip kibao za madawa apate nafuu akaendelee na matibabu zaidi Turkey.

Maana Covid19 inaandamana na "ulemavu" wa kila aina hata mgonjwa akipona ikiwa hakupatiwa matibabu maalum na ya kisasa.

Corona ipo tujihadhari kwa kufuata miongozo mizuri iliyokwisha tolewa na wataalamu wa wizara ya Afya.
 
Back
Top Bottom