Halafu enzi Ile akiwa MEWATA yeye ndio alikuwa msimamizi wa Ile kampeni ya kupima kansa ya matiti. Kweli mganga hajigangi.
Mimi nilikuwa naishi Houston, Texas miaka kama 10 imepita. Kuna Dr mmoja wa Pharmacy nilikuwa nacheza naye Tennis alikuwa ametokea Nigeria. Siku mmoja akaja kucheza Tennis akafa kwa stroke uwanjani pale. Kumbe alikuwa hatumia hata dawa ambazo madaktari walimpa za pressure. Madaktari wengi wanajiamini sana na hii sio nzuri. Lakini simuongelei huyu Mama maana sina habari za uhakika huu ni mfano tu
Mama yangu ni ya ziwa na iligundulika stage 2 ila hakuna tulichoambulia. Usinidanganye. Hizo tafiti zao possibility ya error ni kubwa au walikutana na sample yenye same feature...
Kila binadamu ni tofauti , aina ya cancer lakini ilevile matibabu mfano kwenye cancer za maziwa washauri ni ukipata kuyatoa yote hata kama ni stage 1 and 2 wengi wanatoa moja au wanafanya matibabu halafu hawatoi. Hivyo huwezi kutumia mtu mmoja na kusema cancer ndiyo hivyo tena. Mimi naongelea mamilioni ya watu na data. Mimi binafsi hapa nimepoteza mgojwa kwa cancer ya tumbo hii ilinifanya nijue cancer na matibabu yake. Mtu akipata cancer ya ziwa mshauri atoe yote. Cancer ya maziwa inamtindo wa kurudi baada ya miaka michache. Ina wezekana vilevile mama yako alipata aggressive cancer ambayo haikubali chemo.