Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mheshimiwa Daktari Mwigulu Lameck Nchemba,Ambaye ni waziri wetu wa Fedha ametumia usafiri wa Treni ya Mwendo kasi kutoka Dar kuelekea Dodoma.ambapo Mheshimiwa Waziri ameonekana akiwa amejaa Tabasamu na furaha kubwa sana katika uso wake akiwa ndani ya usafiri huo.
Ambao ni jitihada ,ndoto na kiu ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan katika kuona anakamilisha ujenzi wa reli hiyo na kuanza kutumika kwa usafiri huo ambao utachochea biashara katika nchi zote za ukanda wa Maziwa Makuu.
Mheshimiwa Waziri ambaye anaongoza Wizara ambayo ndio kitovu na tegemeo la wizara zote kujiendesha , ameonekana kuwakosha watu wengi sana kwa uamuzi wake wa kutumia usafiri huo , ambao umepongezwa na kusifiwa na watu wengi sana walioonja na kuutumia kusafiri tangia kuzinduliwa kwake.
Kwa hakika Mheshimiwa Waziri au waweza kumwita Mr Clean kama ambavyo wengi hupenda kumwita ,ameonyesha mfano mzuri wa kuigwa kwa viongozi mbalimbali na watumishi na watendaji mbalimbali wa serikali kuutumia usafiri huo badala ya kukimbizana na magari barabarani,ambapo unakuta wakati mwingine gari la kifahari lililojazwa full tank limebeba watu wawili tu yaani dereva na Bossi wake.
Kwa hiyo itakuwa vyema kama viongozi wengine wataamua kuutumia usafiri huo kwa safari zao za Dar kwenda Dodoma au Dodoma kwenda Dar.hii ni katika kubana matumizi ya pesa za serikali ambazo ni jasho la watanzania wanyonge wanaolipa kodi.
Kikubwa ni kuendelea kuboresha usafiri huu kila panapo onekana kuwa na dosari ,lakini pia kuhakikisha kuwa ratiba inazingatiwa na kufuatwa vyema.kusudi mtu awe na uhakika wa kusafiri kuliko mtu anakuwa na ratiba ya kusafiri siku fulani na muda fulani halafu anasikia ratiba imebadilika ghafla na hakuna usafiri wa treni kwa muda huo.
Kuhakikisha Huduma ziwe nzuri ndani ya treni,wafanyakazi wawe wakarimu,washeshi, wanyenyekevu,wavumilivu ,wenye lugha nzuri kwa wateja na wasikivu sana.hasa kwa kuzingatia kuwa abiria wanakuwa ni watu wenye tabia tofauti tofauti ambapo inahitaji wakati mwingine moyo wa uvumilivu na Upendo.
Wasimamizi wa mradi ni lazima wawe makini , wazalendo,wenye akili na mawazo ya kibiashara na wenye ubunifu na usimamizi mzuri ili mradi ujiendeshe kwa faida na siyo hasara. Kwa sababu haiwezekani unakuta watu binafsi wanaweza kuendesha kampuni yenye magari zaidi ya 20 bila hasara halafu unakuta watu wa serikali wanashindwa kuendesha na kusimamia mradi kama huu wa Treni ya Mwendo kasi .inakuwa inaumiza sana kusikia hasara za mashirika na taasisi za Umma kila mwaka kutoka katika ripoti ya CAG.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.