Dkt Mwigulu Nchemba Atumia Usafiri Wa Treni ya Mwendokasi kutoka Dar hadi Dodoma

Dkt Mwigulu Nchemba Atumia Usafiri Wa Treni ya Mwendokasi kutoka Dar hadi Dodoma

How
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Daktari Mwigulu Lameck Nchemba,Ambaye ni waziri wetu wa Fedha ametumia usafiri wa Treni ya Mwendo kasi kutoka Dar kuelekea Dodoma.ambapo Mheshimiwa Waziri ameonekana akiwa amejaa Tabasamu na furaha kubwa sana katika uso wake akiwa ndani ya usafiri huo.

Ambao ni jitihada ,ndoto na kiu ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan katika kuona anakamilisha ujenzi wa reli hiyo na kuanza kutumika kwa usafiri huo ambao utachochea biashara katika nchi zote za ukanda wa Maziwa Makuu.

Mheshimiwa Waziri ambaye anaongoza Wizara ambayo ndio kitovu na tegemeo la wizara zote kujiendesha , ameonekana kuwakosha watu wengi sana kwa uamuzi wake wa kutumia usafiri huo , ambao umepongezwa na kusifiwa na watu wengi sana walioonja na kuutumia kusafiri tangia kuzinduliwa kwake.

Kwa hakika Mheshimiwa Waziri au waweza kumwita Mr Clean kama ambavyo wengi hupenda kumwita ,ameonyesha mfano mzuri wa kuigwa kwa viongozi mbalimbali na watumishi na watendaji mbalimbali wa serikali kuutumia usafiri huo badala ya kukimbizana na magari barabarani,ambapo unakuta wakati mwingine gari la kifahari lililojazwa full tank limebeba watu wawili tu yaani dereva na Bossi wake.

Kwa hiyo itakuwa vyema kama viongozi wengine wataamua kuutumia usafiri huo kwa safari zao za Dar kwenda Dodoma au Dodoma kwenda Dar.hii ni katika kubana matumizi ya pesa za serikali ambazo ni jasho la watanzania wanyonge wanaolipa kodi.

Kikubwa ni kuendelea kuboresha usafiri huu kila panapo onekana kuwa na dosari ,lakini pia kuhakikisha kuwa ratiba inazingatiwa na kufuatwa vyema.kusudi mtu awe na uhakika wa kusafiri kuliko mtu anakuwa na ratiba ya kusafiri siku fulani na muda fulani halafu anasikia ratiba imebadilika ghafla na hakuna usafiri wa treni kwa muda huo.

Kuhakikisha Huduma ziwe nzuri ndani ya treni,wafanyakazi wawe wakarimu,washeshi, wanyenyekevu,wavumilivu ,wenye lugha nzuri kwa wateja na wasikivu sana.hasa kwa kuzingatia kuwa abiria wanakuwa ni watu wenye tabia tofauti tofauti ambapo inahitaji wakati mwingine moyo wa uvumilivu na Upendo.

Wasimamizi wa mradi ni lazima wawe makini , wazalendo,wenye akili na mawazo ya kibiashara na wenye ubunifu na usimamizi mzuri ili mradi ujiendeshe kwa faida na siyo hasara. Kwa sababu haiwezekani unakuta watu binafsi wanaweza kuendesha kampuni yenye magari zaidi ya 20 bila hasara halafu unakuta watu wa serikali wanashindwa kuendesha na kusimamia mradi kama huu wa Treni ya Mwendo kasi .inakuwa inaumiza sana kusikia hasara za mashirika na taasisi za Umma kila mwaka kutoka katika ripoti ya CAG.
View attachment 3075853

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
How did you get to be this dumb? In a civilised world, a minister taking public transport is not something to be shocked about. Many leaders today do not really care whether they are leaders as long as they fulfil their purpose.
 
Ilikuwa Bonge Moja ya Hotuba maana nilimsikilizaga vizuri sana siku ile .Mimi namuunga mkono na naomba Mheshimiwa Rais aendelee kumuamini kuendelea kuwepo katika Baraza la mawaziri,maana naamini atamsaidia sana Mheshimiwa Rais.
Jamaa anajitahidi kwa kuendesha ile Wizara ambayo ni ngumu kiukweli kuliko Wizara nyingine zote, na inalawama nyingi maana unapaswa ukusanye na utoe mgao ambavyo ni kazi ngumu kwa chumi ndogo kama za nchi zetu. Ama kweli Mzigo Mzito Mbebeshe Mnyamwezi ( Mnyiramba).
 
Kuhusu Treni, chawa acheni kufifisha mbeba maono JPM. Yaani mna jitahidi sana kufuta jina hili kwenye kumbukumbu. Mama mama mama kitu gani.
 
Ndio maana Mheshimiwa Rais anaendelea kumuamini Mr Clean Daktari Mwigulu Lameck Nchemba kuendelea kuongoza Wizara hiyo nyeti.
 
Kuhusu Treni, chawa acheni kufifisha mbeba maono JPM. Yaani mna jitahidi sana kufuta jina hili kwenye kumbukumbu. Mama mama mama kitu gani.
Katika hili uko sahihi, huu mradi pamoja na miradi yote mikubwa ya kimkakati ilikuwa ni maono na uthubutu wa Jiwe ( RIP), hili halina ubishi na litabakia kuwa hivyo katika Historia. Kumbuka Historia haifutiki hata kama kuna namna inataka kufutwa ,Jamaa pamoja na mapungufu yake katika kuimarisha Demokrasia, kwnigine kote hasa katika kuitakia maendelea nchi yetu alikuwa Kiongozi kwa vitendo, na Mzalendo wa kweli. Mengine mapungufu yaliyokuwepo tumsamehe kama binadamu.
 
Legacy huwezi kuifuta. Naamni juko mbeleni kuna wazalendo watweka kumbukumbu vuzuri na kuzitunza kwa vizaji vijavyo wajue mchango wake katika Taifa hili kama Viongozi wengine wakuu waliopita katika Bara la Africa of his Calibre.
 
Mbona bibi tako anasafirigi na fisi kutoka mbeya mpaka dar na huleti ushuhuda humu
 
Ni jambo la ajabu Waziri kupanda Train?
Ni watu wa aina gani wanaostahili kupanda train na wa aina gani wasiostahili kupanda train?
Inaonyesha namna ulivyo muumini wa social discrimination...
 
Back
Top Bottom