Pre GE2025 Dkt. Mwigulu Nchemba: Ni ushamba kugombana kisa uchaguzi, tuendelee kumuombea Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Dogo ni wananchi gani hao?
Anawaambia wanaccm wenzio
Wenye uchu wa madaraka wanataka kugombea na mama ndani ya chama

Mi Nafikiri igeni wa chadema
Wagombea wote washiriki mdaharo
Atakayeshinda apitishwe kugombea
 
Hizi ni Pumba kama Pumba nyingine nani amegombana ? Au wananchi kukasirika kwamba wanaibiwa na kodi zao kufujwa ndio Kugombana ?

Hivi huyu jamaa kuna anayemuelewa anisaidia na mimi....
 
Kwa hiyo unataka siasa za risasi? Hivi una akili kweli ndugu yangu?
Siasa za risasi atazileta nani zaidi ya hao wasiokubalika kutaka kung'ang'ania madaraka!?
Waacheni raia waamue muone kama mboga mboga itasalia madarakani.
 
Dogo ni wananchi gani hao?
Anawaambia wanaccm wenzio
Wenye uchu wa madaraka wanataka kugombea na mama ndani ya chama

Mi Nafikiri igeni wa chadema
Wagombea wote washiriki mdaharo
Atakayeshinda apitishwe kugombea
Unaanzia wapi kuifananisha CCM chama kiongozi Barani Afrika na chama kama CHADEMA kilicho dhaifu na cha hovyo?
 
Siasa za risasi atazileta nani zaidi ya hao wasiokubalika kutaka kung'ang'ania madaraka!?
Waacheni raia waamue muone kama mboga mboga itasalia madarakani.
Raia walishaamua kuwa ni CCM pekee yenye uwezo wa kuliongoza Taifa letu na kuliletea maendeleo na kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja pamoja na Taifa zima kwa ujumla wake
 
Raia walishaamua kuwa ni CCM pekee yenye uwezo wa kuliongoza Taifa letu na kuliletea maendeleo na kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja pamoja na Taifa zima kwa ujumla wake
Raia wapi hao? 🤣
Labda wewe na ukoo wako
 
Hizi ni Pumba kama Pumba nyingine nani amegombana ? Au wananchi kukasirika kwamba wanaibiwa na kodi zao kufujwa ndio Kugombana ?

Hivi huyu jamaa kuna anayemuelewa anisaidia na mimi....
Mheshimiwa ameeleweka vyema sana na ndio maana kauli yake imeungwa mkono sana
 
Atubu kwa makosa yapi aliyoyatenda?
1. Kudhulumu Maasai ngorongoro.

2. Kuuza Bandari za Bara ilhali za Zanzibar hazijaguswa.

3. Kupuuzia kuwakamata na kufichua watekaji waliompga risasi sativa nk nk.

4. Kutokukomesha vitendo vya ulawiti Kwa watoto WADOGO.

5. Kutokuchukua hatua dhidi ya waizi waliotajwa Ripoti ya CAG.

6. Kutuletea mabehewa chakavu kutumika sgr Kwa Bei ya mpya.

7. Kutokuwa na uchungu na pesa za umma, Nchi inashtakiwa na kulipa matrilioni Yeye kimya!!
8. Kuhadaa umma juu ya Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi.

Mengine taja mwenyewe, orodha ni ndefu.
 
Unaanzia wapi kuifananisha CCM chama kiongozi Barani Afrika na chama kama CHADEMA kilicho dhaifu na cha hovyo?
Chadema inaogopwa, na maccm

Imagine hazina imekauka na madeni kibao lakini Abdul anachota mihela kuwapelekea vigogo wa chadema kuwabembeleza wawe washikaji
 
Chadema inaogopwa, na maccm

Imagine hazina imekauka na madeni kibao lakini Abdul anachota mihela kuwapelekea vigogo wa chadema kuwabembeleza wawe washikaji
Hazina ipo imara na ndio maana watumishi wa umma wanaendelea kulipwa mishahara yao bila shida,ajira zinaendelea kutolewa, miradi ya maendeleo Inaendelea bila kukwama wala Kusua sua, hosipitalini zinaendelea kufanya kazi vyema huku zikiwa na vifaa tiba vyote,madawa yote muhimu.pesa za maendeleo zinaendelea kupelekwa kila sehemu hapa nchini.
 
Mheshimiwa ameeleweka vyema sana na ndio maana kauli yake imeungwa mkono sana
Mwananchi gani amegombana sababu ya siasa au ndio wanapindisha mambo ili ya Kenya yakifika huku ya kutaka kuwawajibisha wasingizie ni fujo...
 
Dr.Mwigulu yuko sahihi kabisa,

hawa jamaa wa mihemko na kuporomosha mitusi wajifunze kuzuia ghadhabu na hasira zao za baada ya kushindwa uchaguzi, mbona ni kawaaida tu na ndio demokrasia ilivyo 🐒
 
Dr.Mwigulu yuko sahihi kabisa,

hawa jamaa wa mihemko na kuporomosha mitusi wajifunze kuzuia ghadhabu na hasira zao za baada ya kushindwa uchaguzi, mbona ni kawaaida tu na ndio demokrasia ilivyo 🐒
Upinzani wa nchi umefirisika kiasi kwamba unataka kutumia vurugu kupata madaraka.hata hivyo watanzania wamegoma kuwaunga mkono wasaka Tonge na wachumia tumbo wa upinzani hasa CHADEMA wanaozurura tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…