Pre GE2025 Dkt. Mwigulu Nchemba: Ni ushamba kugombana kisa uchaguzi, tuendelee kumuombea Rais Samia

Pre GE2025 Dkt. Mwigulu Nchemba: Ni ushamba kugombana kisa uchaguzi, tuendelee kumuombea Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Usinitafutie Ban nasema tena usinitafutie BAN!!!🤬🤬🤬🤬🤬🤬🤬
Acheni kutengeneza matukio kutafuta umaarufu.mnajificha mafichoni halafu mnaanza kuzusha ujinga wenu hapa.
 
View attachment 3066963
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu amewaasa wananchi kuacha kugombana kwa sababu za siasa kwani kitendo hicho kinasababisha maafa, yatima, wajane na kukosekana kwa amani.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo kwenye kilele cha Makambi alipokuwa akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista (Wasababato) Mjini Katoro, Mkoani Geita.

Dkt. Nchemba amewaasa waumini hao kuepuka kujihusisha na siasa za fujo na vurugu kwa sababu zinaleta madhara makubwa kwa familia moja moja na nchi kwa ujumla hivyo kuathiri uchumi, umoja na mshikamano wa taifa.

Aidha, Dkt. Nchemba amewataka waumini hao kuendelea kumwombea Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili aendeleze kudumisha maelewano, mshikamano na kusikilizana ambazo ndio zimekuwa falsafa zake tangu aingie madarakani

===

Ndugu zangu Watanzania,

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Hiivi yule aliyebandika majina yake kwenye madaraja na miti akiomba kuchaguliwa urais ni nani, si ndiyo ushamba huyo?
 
itafahamika tu chawa sugu
2025 inajongea, mnatamani kuipeleka mbele ila ndio hivyo tena
usiku wa denu hauchelewi kukuchwa
 
itafahamika tu chawa sugu
2025 inajongea, mnatamani kuipeleka mbele ila ndio hivyo tena
usiku wa denu hauchelewi kukuchwa
Mwakani ni kutimiza wajibu tu .maana hakuna wa kushindana na Rais Samia Suluhu Hasssan katika sanduku la kura.
 
Back
Top Bottom