Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Maendeleo aliyoleta Rais Samia kwa miaka 3 Madarakani ni kama miujiza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi ujishtukii Kila mtu anakukataa kwahiyo huyo Samia mazuri unayaona wewe peke yako mzee🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Aliyekwambia bei ya 27,000 ilifutws ni nani? Unajua utaratibu wa kutoza 27,00?

Mwisho Lengo la ubinafsishaji ni kuongeza ufanisi Kwa maslahi ya kizazi Cha Sasa na kijacho.

Mengine ni umeandika porojo zisizo na msingi.
 
Kwani kundi kubwa la wajinga likikataa au kukubali jambo ndio werevi wachache wakubaliane?

Ndio sijistulii,kama wewe huoni usilazimishe na wengine wasione maana sio lazima uone.Unaweza kuona kile unachotaka.
Kweli hata chizi uwa anajiona yupo sawa Kwa anachokifanya wakati watu wanamshangaa chawa kwenye Moja na mbili
 
Aliyekwambia bei ya 27,000 ilifutws ni nani? Unajua utaratibu wa kutoza 27,00?
JPM alibadilisha kila mtu atoe hio na sio vijijini pekee Samia akaja akasema itaendelea baada ya hapo kama yalivyo mambo mengi ya wanasiasa kilichosemwa tofauti na kilichotokea (Januari akapindua Meza)
Mwisho Lengo la ubinafsishaji ni kuongeza ufanisi Kwa maslahi ya kizazi Cha Sasa na kijacho.

Mengine ni umeandika porojo zisizo na msingi.
Pitia hapo Privatisation only serves public interest if and only if kunakuwa na competition...


Na ukimaliza hapo nikupe Case Study ya Privatization na magwiji / mfano ambao wengi huwa wanatoa kwamba walifanikiwa (UK\) na ni kipi kilichowakuta / kinachowakuta
 
Kwa hiyo wewe mjini uliwahi kulipa 27,000 ukapata umeme au siyo? πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†

Unayumba sana mara useme imefufwa mara useme Iko Vijijini yaani hueleweki.

Sasa kwa taarifa Yako miradi ya lea iliyoko pembezoni mwa Miji na vitongoji inalipwa 27,000.

Mwisho tafuta sababu zingine Hilo la umeme limekushinda.
 
Umeongea uhalisia mkuu.
 
Samia akifanya kosa moja litashikiwa bango kulinganisha na mema mia anayoendelea kuyafanya. Sababu haswa ni jinsi yake ya kike, wengi wetu tunaishi na mtazamo duni kwamba mwanamke ni dhaifu na hawezi kufanya kitu.
Mkuu mfumo dume umechangia,walio wengi walidhani Mama Samia ni mtu wa kuendesha tu,hana lolote.Lakini pale alipoanza kuonyesha makali ya kistaarabu katika kubuni na kusimamia mfuko wa COVID,wenye riba karibu sifuri,ndio tukasikia mambo ya nchi imeuzwa wakati huko nyuma kimya kimya tulikuwa tukikopa kwa riba kubwa hata 15% kwa benki za Shailoki"Kausha Damu"tena grace period ya muda mfupi,sababu ya kutozingatia kanuni za Benki hizo za Maendeleo zenye riba nafuu.Miradi ya Mjomba Magu karibu yote ipo hatua nzuri na nyingine imekamilika.
Mama ni msikivu,hana majivuno,na nchi inasonga mbele.
Kilichobaki deni kwa Mama yetu ni katiba mpya ili asije tena mtu wa kutugeuza watumwa ndani ya nchi yetu.
 
Pia walitaka Samia awe anagombana hovyo tu na mataifa makubwa ya wazungu yeye kawa kinyume kabisa.

JPM alikuwa na hulka ya ubishi mpaka kupitiliza.
 
Pia walitaka Samia awe anagombana hovyo tu na mataifa makubwa ya wazungu yeye kawa kinyume kabisa.

JPM alikuwa na hulka ya ubishi mpaka kupitiliza.
Mjomba Magufuli self discipline ilikuwa shida hata akatimuliwa seminary akiwa form 2.
Kuna mambo yalikuwa hayaitaji ugomvi ilitakiwa busara tu, hadi nchi kama Denmark ikafunga ubalozi.
Unagombana na Benki za Maendeleo na Taasisi zake zinazotoa .mikopo mikubwa yenye riba nafuu na grace period ya miaka mingi,na wakati mwingine wanakufutia deni hilo na kuligeuza grant.
Ukisha watukana unakimbilia kwa Benki za Shyilok anayetaka ratili ya nyama karibu na moyo wako.
 
Kugombana na mabalozi akiwa ndio kwanza kaingia ikulu lilikuwa suala la ajabu sana. Kaja kumfukuza kazi yule dada mtaalam wa vipimo na maabara.

Rais ni mtu mkubwa sana haipendezi kuingilia ugomvi mdogo wa kawaida, ni rahisi kumuonea mmoja ukidhani unawafurahisha walio wengi.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘ŒπŸ‘ŠπŸ€πŸ™πŸ“πŸ†’
 
Ushauri mara nyingine ukitaka kubisha kitu anagalau tafuta Data au hata uwe unasoma kilichoandikwa.... Mwanzo Vijijini inapopeleka REA ilikuwa 27k na pengine mpaka kwenye laki tatu na ushee anapopeleka Tanesco Awamu ya tano wakasema wote bei itakuwa hio (27K)..., Samia alivyoingia bei iliendelea kuwa hio 27K na Kalemani alisema itaendelea kuwa hio na katika Ziara za Samia alisikika pia akisema itaendelea kuwa hio.....

Muda si muda ikaja u-turn kwa Samia kusema haya...

Rais Samia Suluhu amesema ni ngumu kwa TANESCO kuwaunganishia umeme Watanzania kwa Tsh. 27,000 hivyo amewataka waunganishe umeme kwa gharama ambazo Wananchi wanaweza kuimudu

Amesema amesikia malalamiko kwa Wananchi ambao wanasema wamelipa Tsh. 27,000 lakini hawajaunganishiwa umeme ambapo TANESCO husema ni kwa kuwa hawana nguzo...

Ameongeza kuwa, kuanzia sasa umeme hautakuwa kwa gharama iliyotajwa awali kwa kuwa TANESCO wanatumia gharama kufikisha umeme


Kwahio Ushauri wa bure unapobisha vitu factual vilivyotokea ndio haya haya nayosema na niliyosema hapo mwanzo....

 
πŸ†’πŸ“πŸ€πŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…