Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Waziri wa fedha na mipango Dkt. Philp Mpango amesema anarudi kuchapa kazi baada ya mkono wa Mungu kumvusha na ugonjwa uliomkumba mpaka akalazwa.

Waziri Mpango amesema haya (Nukuu) - Narudi kazini na kazi ndogondogo nimekwishaanza za kulitumikia Taifa. Watanzania tuendelee kumwomba Mungu kwa kila mmoja na imani yake na atatuvusha. Amenivusha mimi na wengine ninaowaacha hapa atawavusha.

Nilikuwa nafungua mitandao, ni mambo ya ajabu sana. Nimeonja upendo mkubwa sana kwa wananchi wa Tanzania na wananchi wenzangu wa Buhigwe, wawe na amani na muda si mrefu nitakwenda kuwatembelea

Madaktari, manesi, wataalamu wa viungo, mpaka wahudumu nawashukuru sana kwa huduma nzuri mlizonipa katika kipindi chote. Ni vijana lakini wanafanya kazi kubwa sana"

Natoa pole sana kwa familia zilizopoteza wapendwa kwa wiki mbili nilizokuwa hapa na nyumbani. Ningeshiriki msiba wa Maalim Seif, Balozi John Kijazi na jana nimempoteza mwalimu wangu wa pekee, Profesa Benno Ndulu na mdogo wangu Atashasta Nditiye"

Kulikuwa na vishawishi, hamia Dar es Salaam, hamia huku nikasema hapana, hospitali ni nzuri kabisa na wataalamu walioiva. Sababu ya kukimbilia Ulaya, haipo. Tuboreshe vya kwetu na kwa nafasi aliyonipa Rais, nitamshauri kuboresha zaidi



Ikumbukwe watu wasio wema walizua taarifa za uongo kuwa amefariki baada ya kulazwa. Na tarifa hizo za uongo zilidai amefariki kwa ugonjwa wa Covid 19.

Dkt. Mpango alituma sms kwa mkuu wa nchi yetu kuwa amewasamehe waliomzushia uongo kuwa amekufa.Sasa wakimuona sijui watajisikia vipi. Aibu kubwa kwa wanafiki. Zaidi soma Dkt. Philip Mpango: Mimi ni mzima, walionizushia kifo nimewasamehe
Kaongea vizuri sana
 
1614096634729.png
 
Bado hajapona,sema ICU wanaamini siku 21 mtu tokea awe positive,hawezi ambukiza tena. Hiyo ni theory tu. Hao Ma Dr wanajiaona vijana hata wakipata hawatakuwa na hatari ya kuzidiwa. Sema wanasahau wanaweza ambukiza baba zao,mama zao. Too sad.
 
Bado hajapona,sema ICU wanaamini siku 21 mtu tokea awe positive,hawezi ambukiza tena. Hiyo ni theory tu. Hao Ma Dr wanajiaona vijana hata wakipata hawatakuwa na hatari ya kuzidiwa. Sema wanasahau wanaweza ambukiza baba zao,mama zao. Too sad.
hapo ndio tunaanza kuishutumu serikali,wangeanza kuelimisha watu mapema ujinga kama huu usingekuwepo,hao wanaenda kuambukiza watu wengine familia zao na wagonjwa wa hapo hosptali
 
Back
Top Bottom