Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Duuh mkuu una roho ngumu sana
Sio roho ngumu mkuu, ukweli MCHUNGU lakini ndio hivyo.. Mapafu yamechakazwa na Coona, hamna mtu humo, ni maiti hiyo mjianandae wapendwa wake.
 
..Dr.Mpango anasema alikaa na mtungi wa oksijen nyumbani kwake kwa muda wa wiki mbili, baadae ikaamuliwa apelekwe hospitali.
 
Amezungumza na waandishi wa habari akiwa hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma leo tarehe 23 Febr 2021, live kupitia TBC.

Amesema alikuja hapo hospitalini akiwa na mtungi wa Oxygen. Amekuwapo kwa zaidi ya wiki mbili. Na leo ni siku ya 3 hajagusa mtungi wa Oxygen, anapumua mwenyewe.

Tunafurahi sana kuona amepona.

Binafsi nafurahi zaidi kwa ushuhuda wake wa kwamba amepona kwa tiba rasmi za hospitali, na si kwa mambo ya kujifukiza na kupiga nyungu. Huu ni ushuhuda kwamba hizi ndizo huduma tunazopaswa kuzieneza kwa wote na kuhimiza wananchi wazitumie, na siyo kutupoteza kwa mambo ya nyungu.

Amesifu excellent professionalism ya madaktari wetu. Naomba ujumbe huu uwafikie wale wanasiasa wote wanaobeza madaktari wetu na kuwadhalilisha, na ujumbe uwafikie pia wale wanaohimiza uganga wa jadi. Mheshimiwa amekiri kuwa hii sekta inastahili kupewa kipaumbele zaidi.
Usisahau professionals hao hao ndio waliogundua Covidor, nyungu na ndio zinazotumiwa sasa hivi kila hospital. Ndio wanaoshauri Physiotherapy ambayo unaweza kuifanyia nyumbani na ni ukweli kwamba Hakuna TIBA rasmi ya COVID19 duniani kwa sasa.
 
Amezungumza na waandishi wa habari akiwa hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma leo tarehe 23 Febr 2021, live kupitia TBC...
Tunakutuma ukienda bungeni uwe mpigaji wa kerere kuongezwa kwa bajeti ya wizara ya afya
 
Kulikuwa kuna ulazima gani wa kuwaleta wagonjwa wa corona hadharani tena bila tahadhari? angalieni hao watumishi wa afya wanaotegemewa kuhudumia wagonjwa wengine mbele ya waandishi wa habari namna wamekuwa exposed bila hata mask ili tu kum please mtu mmoja tu anayeitwa jiwe.
 
Ningekuwa mimi nisingeishia kufurahia kuvushwa pekee bali ningejiongeza na kujitafakari kwa upya ni kwa nini haswa watu walikuwa wafurahie kuugua kwangu na baadhi actually hata kutaka nife kabisa?
Great Thinking, Hafahamu tungo za rohoni.Alitakiwa aangalie hili suala kutokea angle hiyo lakini anaogopa kutumbuliwa kuliko kifo.Ajabu&Aibu kwa wasomi wetu.
 
Ni bora mngemshauri apumzike co kwa kumlazimisha kule kuitisha press.huku akikohoa kohoa
 
Kulikuwa na ulazima wa yeye kuzungumza mbele ya umma?
 
Back
Top Bottom