Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Pole nyingi kwake, shukrani pia kwa Mwenyezi Mungu! Namshauri ajitathmini sana namna nz mazingira alivyo upata ugonjwa huo ili asijekanyaga tena mahala pale!
 
Najisikia aibu kuwa mmoja wa wasomi nchi hii, Dr Mpango acha ujinga pigania afya yako... la sivyo punde mkeo atapewa raha na wengine.

Cheo ni dhamama.
 
Nimeiona hii footage,,nikasikitika sana,,huyo ni mtu mkubwa sana,,anataabika vile,,,je sisi wa chini itakuaje..?.
Ana kila kitu at his disposal...

Ninyi wa chini haliwafiki, Mungu fundi bwana.
 
Uko sahihi kiasi chake mkuu.

Lakini kumuona qualified Daktari yupo na mgonjwa anayekohoa bila hata mask. Na anajua kabisa huyu mgonjwa ana COVID ambayo haijapona….... Imenifanya niwaze huyu bwana elimu yake inamsaidia vipi.... Nimeogopa sana.....
Afu wakitoka hapo wanaipigia kelele serikali haiwapi PPEs..
 
Mi nadhani angestaafu tu Kiongozi wetu, akabidhi kijiti kwa wengine.
 
TRUE, he is not out of the woods yet!! Amewahi sana kushukuru!!! Aachane na tabia ya kujipendekeza kwa JIWE; anatakiwa achukue likizo akapumzike badala ya kujifanya yeye ni mzalendo at the expense of his health. Akifanya mchezo ataondoka!!!
Ha Ha ha,

nadhani amesoma Biblia Waebrania 11. Kwamba ukiamini bila hata kuona basi matokeo yatakuwa chanya.
 
Mmmh nahisi kama kuna kitu nahisi hivi ila sijui kama atatoboa Nimuombee kheri tu maana mwaka huu hiiiii mmmmm
Ngoja nikae kimya nisijeitwa mchawi nikala kejeri bure narudia tena huu mwaka huu tutaona mengi sana.
 
Bado hajapona,sema ICU wanaamini siku 21 mtu tokea awe positive,hawezi ambukiza tena. Hiyo ni theory tu. Hao Ma Dr wanajiaona vijana hata wakipata hawatakuwa na hatari ya kuzidiwa. Sema wanasahau wanaweza ambukiza baba zao,mama zao. Too sad.
Jamani dakika 20 tu zimepita nimepata taarifa za msiba. Na umri ni 35. Aliumwa na akapata nafuu lkn ghafla hali ilibadilika na ameaga dunia leo. COVID-19 variant ni unpredictable na inachukua aspect tofauti kwa kila anayeipata. Watoto tu ndio inafahamika symptoms sio severe lakini very good carriers of the C-19.
 
COVID-19 IPO NA NI REAL. Si ugonjwa wa kwanza na wala hautakuwa wa mwisho. La muhimu ni Serikali kuutangaza rasmi na kufanya kampeni ya dhati katika kuelimisha wananchi jinsi ya kupunguza maambukizi na wenyewe kujikinga.

Ukimwi tulifanya hivyo mpaka ukaeleweka Tanzania nzima, mjini kwa vijijini sielewi kwanini iwe shida kufanya hivyo kwa COVID-19.

Lock down si muhimu pengine katika mazingira yetu lakini kuwaeleza wananchi kuwa na nafasi ya mita 1 kati ya mtu na mtu, kujiepusha na mikusanyiko ya watu (Harusi, maziko, makanisani, misikitini n.k) ni elimu tosha. Ni juu ya kila mmoja kupanga na kuchagua, na tutaokoa maisha ya wengi. Hatujachelewa tuanze leo!
 
Back
Top Bottom