Pre GE2025 Dkt. Slaa afikishwa mahakamani Kisutu kwa Shtaka la kusambaza taarifa za Uongo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Dr. Slaa kama hana ushahidi wa aliyosema, ataweza kufungwa, ushahidi kwa mambo ya kuambiwa kwa mdomo au kupigiwa simu ni mgumu sana kupeleka kama ushahidi mahakamani na itaweza kumpeleka kifungoni..!!
 
Kwa hiyo walimkamata bila kujua Sheria inasemaje?!!!Duuh kweli tutafika.
 
Natoa ushauri kwa jeshi la polisi ili kutozua taharuki.

Kwa hawa watu maarufu, taarifa iwe inatolewa kabla ya watuhumiwa kupata upenyo. Namaanisha polisi wasiwe wa mwisho kutoa taarifa hasa baada ya kelele kuwa nyingi, wajitahidi kutoa taarifa punde tu kitendo cha ukamataji kinapokamilika.

Kwa sisi kajamba nani, ndugu zetu wapewe taarifa pindi tu tunapohitajika kukamatwa.

Hii itaondoa hisia za polisi kuteka watu hasa baada ya matukio ya karibuni watu kuchukuliwq na wanaodhaniwa kuwa polisi, kisha miili yao kuokotwa wakiwa wafu.
 
Dr Slaa hakutaja usalama wa Taifa wa nchi gani.

Ndio tujue wanasiasa wanacheza na akili zetu.

Hii kesi Dr anashinda asubuhi.
Alimtaja Mwamba. Halafu akafafanua kuwa Mwamba ni Mbowe. Akasema pia kuwa maafisa wamesambazwa nchi nzima. Itabidi afafanue hao ni maafisa usalama wa nchi gani ambao waliweza kusikiliza mazungumzo kati ya Rais na Mbowe.

Ukweli ni kuwa kwenye hili amejitakia mwenyewe. Na baada ya kumalizana na TISS, Mbowe anaweza kumfungulia kesi ya madai ambamo itabidi atoe ushahidi kuwa Mbowe alizungumza na Mkuu wa Nchi, na kuwa kuna pesa zilitoka serikalini kwenda kuwahonga wajumbe wa Baraza Kuu la Chadema. Alitakiwa amuige Lissu ambae anazungumzia pesa za Abduli bila kuwq specific.

Ila nakumbuka nae aliwahi kusema kuwa watu wasikimbilie kumtetea Mbowe kuwa sio gaidi. Sasa na yeye yamemkuta.

Lakini itakuwa vizuri kama DPP atasema hana haja ya kuendelea na hii kesi kama alivyofanya kwenye kesi ya Mbowe.

Amandla...
 
Hoja ipo, mzee wa mihogo alihongwa akapewa na ulinzi kusaliti mabadiliko.

Akapewa na kitumbua kbs ili asife njaa. Acha wamshughulikie. Mtu unakuwa afisa mwandamizi wa serikali afu unakuwa mzushi mzushi tu.
 
Wazee hawa walioshika imani za kikatoliki, vizuri sana ukimuweka ndani, endapo kama hana kosa ( ikosala ya kilatini haikopeshi) albadir cha mtoto!
--"Vermes, Cancer, et Vermes penetrant animam tuam".
Kisha wanapata Cancer ♋️ ???! Au ?
 
Nitasikitika sana kama Dk. Slaa atashinda kesi au kesi yake kufutwa.
 
Babu Mzee Slaa. Learn how to guide your mouth. Kumzushia kiongozi wa nchi ni mambo ya kishamba
 

Sheria zingeruhusu mtuhumiwa asipofikwa na hatia, alipwe gharama za usumbufu........
 
Wazee hawa walioshika imani za kikatoliki, vizuri sana ukimuweka ndani, endapo kama hana kosa ( ikosala ya kilatini haikopeshi) albadir cha mtoto!
--"Vermes, Cancer, et Vermes penetrant animam tuam".
Hahaha....mbona unawatisha watoa amri za kukamata
 
Na hizo sheria zingesimamiwa vizuri wasingemgusa
Upo sahihi, mara kadhaa watu wanakamatwa wanawekwa mahabusu muda mrefu then hawakutwi na hatia, haya ni mambo ya ajabu... Wengine mahabusu upelelezi unaendelea, mara uchunguzi unaendelea...... Pia hata feedback ya kuendelea kwa uchunguzi hakuna au upo haueleweki....... Ingawaje mambo yanabadilika, ya sasa si ya zamani......
 
Muosha huoshwa!!alihama chadema kwa dharau akaenda ccm akapewa ubalozi,sasa hvi wanamgeuka!karma ipo kazini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…