Dkt. Slaa ahutubia mkutano wa CHADEMA. Asema sasa imekomaa kuongoza nchi

Dkt. Slaa ahutubia mkutano wa CHADEMA. Asema sasa imekomaa kuongoza nchi

Je, amerejea CHADEMA? Tusubiri tuone

View attachment 2531371
View attachment 2531436

Aliyewahi kuwa Katibu wa CHADEMA Taifa na baadaye Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbrod Slaa kwa mara ya kwanza jana Jumapili amehudhuria mkutano wa Chadema Wilaya ya Karatu na kuahidi atashirikiana na chama hicho kudai Katiba mpya.

Dkt. Slaa aliondoka CHADEMA akiwa Katibu Mkuu wakati wa mchakato wa uchaguzi Mkuu mwaka 2015 baada ya chama hicho, kumteua Edward Lowassa kugombea urais kupitia chama hicho.

Dkt. Willibrod Peter Slaa anasema:
“Mimi sina chama, nawaambia CCM ili kuwasaidia, kuna sababu gani ya kuchagua kama hawajirekebishi, lakini kwa sasa twende na chama ambacho angalau kinaonesha kina wafikiria na kuwajali Watanzania hiyo ni katika uchaguzi unaoakuja, maandalizi yaanza ndani ya chama

“Hatua ya pili twende katika mikutano ya Katiba, CCM wanasema Katiba itakuletea Uji, Wali au chakula kingine chochote nyumbani kwako? Niwaambie Katiba ni kila kitu.

“Ugali unaoupata maamuzi ya huo bei ya ugali na chakula kingine unachopata inatokana na Katiba.

“Katiba ya sasa imetoa mamlaka yote kwa Rais, simlaumu Rais peke yake bali nalaumu mfumo uliotengeneza Katiba.”

SLAA NI PROFESA
Mimi ni Profesa wa Siasa, kazi yangu ni kutoa ushauri na nitawaelekeza, Profesa amepita mengi na magumu ana uzoefu

Ndio maana naongea kwa uhuru kabisa katika Nchi yangu najua Sheria najua haki zangu na hakuna wa kuniuliza kwanini nazungumza na CHADEMA, nitasema bila kumung’unya maneno

Bei ya Mchele inapanda licha ya kuwa tunalima hapahapa Nchini, bei ya nyama ya ng’ombe nayo inazidi kupanda
hiki kibabu kinahangaika kweli
 
Siasa ni dynamic. Hakuna rafiki wa kudumu na adui wa kudumu

Kama CCM walimpokea tena Lowasa tena kwa mbwembwe, kwa nini Chadema wasimpokee tena katibu wao mkuu bora wa wakati wote?

Chadema ya leo ni mti ambao Mzee Slaa alishiriki kuupanda.
Hilo halina ubishi mchango wake hauwezi kupuuzwa. Imank yake imebaki kugombea ubunge tu sio level ya Urais tena
 
Je, amerejea CHADEMA? Tusubiri tuone

View attachment 2531371
View attachment 2531436

Aliyewahi kuwa Katibu wa CHADEMA Taifa na baadaye Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbrod Slaa kwa mara ya kwanza jana Jumapili amehudhuria mkutano wa Chadema Wilaya ya Karatu na kuahidi atashirikiana na chama hicho kudai Katiba mpya.

Dkt. Slaa aliondoka CHADEMA akiwa Katibu Mkuu wakati wa mchakato wa uchaguzi Mkuu mwaka 2015 baada ya chama hicho, kumteua Edward Lowassa kugombea urais kupitia chama hicho.

Dkt. Willibrod Peter Slaa anasema:
“Mimi sina chama, nawaambia CCM ili kuwasaidia, kuna sababu gani ya kuchagua kama hawajirekebishi, lakini kwa sasa twende na chama ambacho angalau kinaonesha kina wafikiria na kuwajali Watanzania hiyo ni katika uchaguzi unaoakuja, maandalizi yaanza ndani ya chama

“Hatua ya pili twende katika mikutano ya Katiba, CCM wanasema Katiba itakuletea Uji, Wali au chakula kingine chochote nyumbani kwako? Niwaambie Katiba ni kila kitu.

“Ugali unaoupata maamuzi ya huo bei ya ugali na chakula kingine unachopata inatokana na Katiba.

“Katiba ya sasa imetoa mamlaka yote kwa Rais, simlaumu Rais peke yake bali nalaumu mfumo uliotengeneza Katiba.”

SLAA NI PROFESA
Mimi ni Profesa wa Siasa, kazi yangu ni kutoa ushauri na nitawaelekeza, Profesa amepita mengi na magumu ana uzoefu

Ndio maana naongea kwa uhuru kabisa katika Nchi yangu najua Sheria najua haki zangu na hakuna wa kuniuliza kwanini nazungumza na CHADEMA, nitasema bila kumung’unya maneno

Bei ya Mchele inapanda licha ya kuwa tunalima hapahapa Nchini, bei ya nyama ya ng’ombe nayo inazidi kupanda
Tuache fitna Dr Slaa ndio CHADEMA na CHADEMA ndio Dr. Slaa.
 
Ni mnafiki👇🐒🐒🐒
 
Kama ni kweli basi mbowe na wahuni wenzie wamekubali kuwa chadema ipo shimoni sasa wanatafuta mtu wa kukitoa chama shimoni.

Wakumbuke huyo jamaa alikuwa mfuasi wa siasa za magufuli [emoji1787]tuliwaambia chadema siku nyingi kuwa kumpinga mzalendo ni kujichimbia shimo wenyewe wakabisha.

Chadema washukuru kuwa sasa hivi hakuna chama chochote cha upinzani chenye kubeba legasi ya nyerere wala magufuli vinginevyo wangebaki mdomo wazi maana kifo cha hicho chama kinge vunja rekodi ya vifo vyote
Wewe kweli ni mpumbavu. Hivi unamuonaga magu ni Mungu au? Wengine tulimchukulia kitu cha kawaida sana
 
Ukweli ni kuwa MaCHADEMA hawana tena mvuto wala sera zaidi ya matusi. Gaidi ameamua kubadili tena Gia angani kwa kumrudisha Halima Mdee team na Babu mzinzi mwizi wa wake za watu Slaa kuwa front line. Babu Mzinzi hajawahi rudisha kadi ya CCM tangu achukue 1989. Chiba Lissu hakubaliani na hiyo move kaamua kurudi kulelewa na hawara kule BEJIAMU. Sasa sasa in Chiba voice. MaCHADEMA yanajipaka matapishi kwa sababu hayana watu wengine zaidi ya hao wahuni. CCM tu narudi tena kuiendesha MaCHADEMA taka yasitake. Yees matusi ya MaCHADEMA yaendelee.
 
CHADEMA, msipuuze Dr. Slaa hata wale waliomponda Dr.Slaa wakati anasusa Leo wapo CCM wanalamba asali. Siasa ni upepo siasa ni watu, anaweza kuja Leo Kwa nia ovu, lakini akatamani akawa shujaa wa chama, mpokeeni siasa ichangamke na adui yenu hamuwezi kumjua kamwe mpaka siku atakapowaumiza.
 
Hatimaye CDM wamesikiza ushauri,

Binafsi nimekuwa nikishaauri wazi umuhimu wa Slaa CDM,

Nashauri arudi nafasi ya Katibu mkuu wa chama, chama kitaimarika sana kimkakati na kisera kuepuka siasa za matusi ,ushabiki na kuvizia matukio.

Dr Slaa anaweza kuwajibu Kwa HOJA wazee wa CCM kama wassira na PINDA kuelekea kupata njia ya kuandika KATIBA mpya.

Ni kwema mbeleni, ni kwema mbeleni.

Mungu ibariki TANZANIA,

Mungu ibariki CDM.

Aamen
Nashauri Chadema iunde kitengo Cha Sera na mipango ambacho litakua na Mkurugenzi wake,ambaye atakua ni Dr. Slaa.

Ukisema arudi kwenye Ukatibu mkuu pataibuka Mgogoro mana Kuna mtu ambaye Kwa hakika ni Mtiifu sana Kwa Chama yaani John Mnyika.

Au kama Mwenyekiti atabadilika na kuja Chadema asili ya Kupiga vita Ufisadi ikiongozwa na Mwenyekiti kama Lisu au Heche au Msigwa basi Dr. Slaa atafiti sana kwenye Ukatibu mkuu.

Dr. Slaa anafaa sana kuwa kwenye nafasi za juu ili arejeshe heshima ya Chadema kupambana na CCM na mafisadi wake
 
Lowassa was not a traitor lakini
Ila alikuwa kama adui wa taifa kwa jinsi chadema walivyowahi kumtangaza kwa ufisadi, haikuwa rahisi mtu kudhani kwamba ipo siku Lowasa atakuja kuwa mwana chadema achilia mbali kuwa mgombea wao wa urais. Halikuwa jambo la kawaida hata kidogo.
 
Nashauri Chadema iunde kitengo Cha Sera na mipango ambacho litakua na Mkurugenzi wake,ambaye atakua ni Dr. Slaa.

Ukisema arudi kwenye Ukatibu mkuu pataibuka Mgogoro mana Kuna mtu ambaye Kwa hakika ni Mtiifu sana Kwa Chama yaani John Mnyika.

Au kama Mwenyekiti atabadilika na kuja Chadema asili ya Kupiga vita Ufisadi ikiongozwa na Mwenyekiti kama Lisu au Heche au Msigwa basi Dr. Slaa atafiti sana kwenye Ukatibu mkuu.

Dr. Slaa anafaa sana kuwa kwenye nafasi za juu ili arejeshe heshima ya Chadema kupambana na CCM na mafisadi wake
Mnyika ni dhaifu na mwoga sana. Hafai hiyo nafasi. Mrudisheni Slaa.
 
Back
Top Bottom