Dkt. Slaa anadaiwa kusafirishwa Usiku huu (August 14, 2023) kuelekea Mbeya

Wanawapeleka Mbeya kuwatumia majaji wale wale waliotupa kesi.....
 
Safi sana, akaungane na watuhumiwa wenzake wa uhaini.
 
Unaweza weka ushahidi wa hili hapa jukwaani?
Samia siyo Magufuli alyewasamehe kina Nape na kundi lake la kina Mzee kinana! Kina Dr Slaha ndiyo by by hiyo!! "Ukinizingua,tunazinguwana" by Samia!! ndiyo maana yake hiyo!!
 
Maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga
 
Rais Samia rais aliyefanikiwa kugawanya Tanzania kwa misingi ya UDINI akishirikiana na waarabu. Rais aliyefanikiwa kuporomosha misingi yote aliyoiacha baba wa taifa. Laana imtafune
Hiyo misingi alioiacha huyo baba wa taifa ndio hiyo hiyo anayoifata huyo Raisi aliepo Mamlaka Makubwa ya Raisi na kumpa kinga ya kutoshitakiwa ni matokea ya Katika aliotuachia huyo baba wa taifa katiba tunayo tumia ni ile ile toka enzi za nyerere au wewe hufahamu
 
Polisi kazi yao ni kukamata tu, DPP ataamuwa kama wana kesi ya kufikishwa mahakamani au hapana. Mahakama itaamuwa kama ni wahaini kweli au la.

Sisi kwa sasa tusubiri shria zifate mkondo wake.
Nakazia hapo kwa police! Police anakamata na kupeleleza shauri lote pamoja na kukusanya ushahidi wote wa shauri,na Kisha hupeleka taarifa zake zote kwa DPP, na DPP akiwa Kama Wakili wa Jamuhuri atapitiaa kazi yote ya uchunguzi uliofanywa na police,na akiona Kama upelelezi una mashiko Jalada linapelekwa Mahakamani kwa Mashitaka tayari!!
 
Maisha ya Wilbroad Slaa kisiasa na kiuzalendo yalifika Kikomo pale ambapo aliwakana wapinzani wenzake enzi za Rais John Magufuli na kukimbilia mkate wa kuwa balozi huko Canada.

Wilbroad Slaa, wakati wapinzani wanapambania demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari na Utawala Bora katika awamu hii iliyopita, yeye aliwageuka na kutugeuka watanzania hadi kufikia hatua ya kusema kwamba hakuna haja ya katiba mpya, Rais JPM aachwe ainyooshe nchi.

Kama hiyo haitoshi, kipindi wenzake wamepewa kesi za kubumba na mwendazake ambapo hata hivyo Mh Rais Samia alikuja kuzifuta yeye aliwasagia kunguni na kusema hao siyo wapinzani,ni wapinga maendeleo.

Leo hii zama zimembadilikia na anaonekana kwenda kuozea selo hakuna hata chama Cha siasa kutoka upinzani kinachohangaika nae, Wilbroad Slaa amepuuzwa kama vile ambavyo yeye aliwapuuza wenzake.

Ama hakika kuimba ni kupokezana,Unafiki,Njaa na Uchu wa madaraka wa Wilbroad Slaa na tamaa zake za fisi zimepelekea awe na mwisho wa fedheha katika siasa za Tanzania...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…