Dkt. Slaa anadaiwa kusafirishwa Usiku huu (August 14, 2023) kuelekea Mbeya

Dkt. Slaa anadaiwa kusafirishwa Usiku huu (August 14, 2023) kuelekea Mbeya

Nchi inaendeshwa kihuni sasa.
FB_IMG_1692047468444.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Balozi Hana kinga ya kutoshitakiwa?
Uhaini hauna kinga,unazani Mama yuko kama Magufuli aliwapuuza kina kinana na kundi lake,angeaamua angewapa kesi ya Uhaini bila shida na ushahidi uko ubaoni, unazani Nape mjinga kupiga magoti kwenye viwanja vya Ikulu kuomba msamaha kutoka kwa Mwendazake!? Kinana mwenyewe alikimbia Nchi kwa muda baada ya ule upuuzi wao wa Waraka!!
 
Hii ndio Taarifa ya sasa tunayokunong'oneza kutoka kwenye vyanzo vyetu vya Uhakika zinadai Kwamba Balozi Dkt. Wilbrod Slaa ambaye ni miongoni mwa Watetezi wa Bandari za Tanganyika, anasafirishwa Usiku huu kuelekea Mbeya, kwa lengo la kuunganishwa na 'wahaini' wenzake ili wafikishwe Mahakamani .

Utetezi wake wa Mali za Tanganyika umempa kesi ya Uhaini .

View attachment 2717521
Hii nchi imeanza kuzeeka kwann hatuna unit wananchi hofu tunazopewa ndizo zinafanya kukosa umakini wa mafikirio zaidi jeshi la polisi Lima ukubwa gani wakuzidi wananchi kutuzuia tutapoamua jambo nchi ni ya wananchi sio viongozi wazalendo wa nchi kufikishwa mahakamani sio jmbo jema. Sana
 
Hii mbinu wanayotumia polisi kumlinda msaliti wa rasillimali za Tanganyika ni ya kijinga sana..

Hivi hawa polisi wataendelea mpaka lini kukubali kutumika kwenye kukandamiza haki za wanaolalamika wanapotendewa uovu?

Hili jeshi la polisi kuna wakati nikilitazama kwa jicho la pembeni, naliona sasa limegeuka kabisa na kuwa jeshi la kuwalinda majambazi wa rasilimali za Tanganyika...

Wala sio tena lile jeshi la mwanzo la kumlinda mtanganyika na mali zake, hawa jamaa bahati mbaya zaidi, wanatumia sheria zetu bila vidhibiti ili kutimiza malengo yao ovu dhidi yetu.

Dr. Slaa ni mwanasiasa mkomavu, anayezijua mbinu zao zote, mbivu na mbichi, kujaribu tendo lolote la kumtisha huyu, mtu mwenye uelewa wa juu kabisa wa sheria, sio za kanisani pekee, na za nchi hii, naona kabisa hawa polisi wetu wanaendelea kujidhalilisha bila kujua, kwa maslahi yake yule mjinga aliyetusaliti.
mapolisi utayalaumu bure! yenyewe ni kupewa maelekezo tu na hutekeleza bila kuruhusiwa kuhoji. The police force is there to protect the interests of the ruling class. ni mambumbumbu flani ndio maana hata Huwa hawawezi kudai masilahi yao.

adui mkuu wa taifa letu ni wanasiasa ma puppet ambao huwa na masilahi binafsi, wanatumiwa na mataifa ya nje kuhujumu taifa.

ma nchi ya kijinga haya yanakaribia kufanana na kuzimu

JESUS IS LORD
 
Ila huyu mzee acha ccm wamsomeshe namba hayo ni malipo ya kile alichokifanya yeye na mwenzake Lipu-mbaa 2020
 
Sio mole anapandikizwa huko?

Kama nakumbuka alituaminisha kwamba aliagizwa na maafisa usalama wengi aseme yale aliyokua anayasema... au mm sikumuelewa.
Wewe mwongo.

Alisema kuna watu 18 viongozi wa Serikali na CCM wamemuwa wakimpigia simu kumwambia kuwa watu waendelee kudai bandari zao, wao kutokana na nafasi zao Serikalini, hawawezi kutamka chochote.
 
Watanganyika wako wapi? Na Tanganyika ni eneo gani? Mnajijazia jazba zisizo na maana tu.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, idadi ya Watanzania ni kama 61 Milioni. Kati ya hao ni chini ya 3 Milioni tu ndiyo walizaliwa kabla ya mwaka 1964 nchi iliyokuwa inaitwa Tanganyika.

Ina maana watu 58 Milioni vyeti vyao vya kuzaliwa vimeandikwa Tanzania.

Wewe unayedai Tanganyika ni nani unayetaka kumuweka kwenye hiyo nchi?

Pili aliyetoa jina la Tanganyika ni Mkoloni Mjerumani na Mwingereza akalirithi, ila Mwl Nyerere akaobatiza nchi Tanzania baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mnajazwa UJINGA na nyinyi MNAJAA
kwanza nijibu Zanzibar ni nchi au NI mkoa!?
KAMA ukijibu ni nchi Basi Tanganyika ipo , na Kama ww sio mzanzibar Basi mm na ww ni watanganyika , tuungane kulinda raslimali za Tanganyika yetu. Hiyo Tanzania unayoisema ipo ki ceremonial tu .
 
Maguvu ya nini kwenye mambo ya kutumia akili?.ila slaa analipa malipo ya usaliti
 
Uhaini hauna kinga,unazani Mama yuko kama Magufuli aliwapuuza kina kinana na kundi lake,angeaamua angewapa kesi ya Uhaini bila shida na ushahidi uko ubaoni, unazani Nape mjinga kupiga magoti kwenye viwanja vya Ikulu kuomba msamaha kutoka kwa Mwendazake!? Kinana mwenyewe alikimbia Nchi kwa muda baada ya ule upuuzi wao wa Waraka!!
Kupigania mali za Taifa ndio Uhaini ?
 
Haya yanayoendelea kufanyika Tanzania Wajukuu zetu watakuja kuyakojolea makaburi yetu,Kila kiongozi anajiuliza atapata lini nafasi ya juu zaidi ili aendelee kutunisha mfuko wake...Ugumu wa maisha tulio nao hadi sasa umesababishwa na mikataba ya Ovyo iliyosainiwa na viongozi waliopita kabla..

Rasilimali zetu ngapi zinachukuliwa na kusafirishwa moja kwa moja bila kuleta pato kwa Taifa na hatusemi kitu,,,Watu husema jambazi mwenye silaha akikuvamia,wewe fanya tu anachosema ili uyanusuru maisha yako,Tukubali tu kwamba tayari tumefeli kuitetea Nchi yetu,asilimia karibu 98 ya Raslimali zilizopo nchini sio zetu(Zimebinafsishwa),Tukae tu kimya kunusuru maisha yetu,mifano ndo kama hii tunayoiona,kila anayejaribu kusimama kutetea taifa anakatwa Miguu ili kututisha tulioko nyuma yake...

Nchi yetu hii kujifanya Hero(Shujaa) wa Taifa,,unapotea na hauchukui muda unasahaulika.....na kweli Tunamkumbuka mzee
 
Nenda kafie mbali, watu wa aina yenu ndio watumwa mnaotafutwa karne hii.

Hovyo Kabisa.
 
Back
Top Bottom