Dkt. Slaa arudishwa kituo cha Polisi Oysterbay kutoka Mbeya. Wakili wake aambiwa akashughulikie dhamana

Dkt. Slaa arudishwa kituo cha Polisi Oysterbay kutoka Mbeya. Wakili wake aambiwa akashughulikie dhamana

Kama unasaga kunguni halafu harufu inakurudia mwenyewe, saga tu, ila Bandari lazima itabinafsishwa tu!
Harufu ya kunguni imeonekana kuwarudia zaidi nyie ndio mana mmechanganyokiwa hajui mfanyeje na muda unakwenda IGA inaexpire October 😁😁😁😁

Mnarukaruka mara mseme mnataka kupinduliwa ni aibu kwa serikali yenye jeshi kulialia kwenye vyombo vya habari kwamba mnataka kupinduliwa
 
Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!

Jana baada ya ku-file maombi ya kulitaka jeshi la Polisi kuwapeleka Dr. Slaa na wenzake mahakamani ambapo leo tungepangiwa jaji atakayesikiliza maombi yetu na kupewa wito wa mahakama (Summons) ili kuwaita wajibu maombi yetu .

Mimi nilisafiri kurudi Dar kwa ndege na kufika majira ya saa tano usiku.Hivyo kazi ya kufatilia tararibu nilizoeleza hapo juu nilimwachia wakili Jebra Kambore akishiikiana na Chengula na wenzake.

Muda huu nimepigiwa simu na uongozi wa Polisi Oysterbay -Dar es Salaam wakinijulisha kuwa Dr. Willibrod Peter Slaa wamemtoa Mbeya usiku na wako naye kituoni hapo. Hivyo nifike kwa ajili ya kufanya utaratibu wa dhamana yake.

Wakili Dickson Matata
18/8/2023 saa 10:07 Asubuhi

Pia soma
- Dkt. Slaa anadaiwa kusafirishwa Usiku huu (August 14, 2023) kuelekea Mbeya
Tungeona unafiki wa utawala huu wa saa100 na waziri wake wa habari wanaojinasibu eti wanajali haki za binadamu na uhuru wa habari huku wanamfungulia mzee Slaa kesi ya uhaini bandia. Ingekua aibu tupu kwa upande wao. Hata huo uchochezi hakuna kesi hapo. Ukweli wamebaki kutega masikio yao kama popo kusikiliza wanachosema wale wenye kupinga mkataba wa kuipa dubai umiliki wa bandari zetu kama himaya yao ili kkuweza kuwatupa lupango.
 
Harufu ya kunguni imeonekana kuwarudia zaidi nyie ndio mana mmechanganyokiwa hajui mfanyeje na muda unakwenda IGA inaexpire October 😁😁😁😁

Mnarukaruka mara mseme mnataka kupinduliwa ni aibu kwa serikali yenye jeshi kulialia kwenye vyombo vya habari kwamba mnataka kupinduliwa
Kuna kauli yoyote ya Serikali kwamba wanapitia upya Mkataba wa Bandari? Kwa taarifa yako, baada ya Bunge kuupitisha Mkataba wa Bandari, Sasa hivi taratibu zingine zinaendelea kama kawaida. Kumbuka, kelele za chura hazimzuii tembo kunywa Maji!
 
Maana neno "Habeas Corpus"
The “Great Writ” of habeas corpus is a fundamental right in the Constitution that protects against unlawful and indefinite imprisonment. Translated from Latin it means “show me the body.” Habeas corpus has historically been an important instrument to safeguard individual freedom against arbitrary executive power.
 
Wajaribu waone kwa Katibu mstaafu wa TEC 😁watajua idadi ya mzunguko wa Dunia
Mtu kanyea debe takribani wiki Sasa,pengine moyo na sukari vimeleta shida wameamua kumuachia,umri ule kupekuliwa makalio na vijana na kulala kwenye zege ni mateso tosha
 
#HABARI Wakili wa mwanasiasa mkongwe Balozi Dr. Willibrod Peter Slaa amesema mteja wake ametolewa jijini Mbeya na kufikishwa Jijini Dar es salaam kwa ajili ya taratibu za kupewa dhamana

Wakili Dickson Matata amesema tayari amepigiwa simu kutoka kwa uongozi wa Polisi Oysterbay - Dar es Salaam wakimtaka afike kwa ajili ya taratibu hizo

"Muda huu nimepigiwa simu na uongozi wa Polisi Oysterbay -Dar es Salaam wakinijulisha kuwa Dr. Willibrod Peter Slaa wamemtoa Mbeya usiku na wako naye kituoni hapo. Hivyo nifike kwa ajili ya kufanya utaratibu wa dhamana yake" amesema wakili Dickson Matata #EastAfricaRadio
FB_IMG_1692353070534.jpg
 
Prof Tibajuka na wengineo waliliolifikisha jambo hili kwenye ngazi za kimataifa, washukuriwe sana. Shinikizo kutoka ngazi za kimataifa ndizo zimefanya watuhumiwa hawa wa uhaini waachiwe kama ambavyo ilitokea kwa wale watuhumiwa wa ugaidi, Mbowe na wenzake.

Utetezi wa akina Nape in broken english haukuwa na mashiko kwenye ngazi za kimataifa, sana sana ulikuwa ni kujiaibisha tu na ni heri wangekaa kimya. Baada ya kuachiwa haitashangaza Dr Slaa kumuona Ikulu kama tulivyomwona Mr Mbowe mara tu baada ya kuachiwa. Siasa za Tanzania ni ka mchezo katamu. Hatima ya hili sakata la bandari iko ukingoni. Mama kawasikia na kuwaelewa. Kazi iendelee!
 
Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!

Jana baada ya ku-file maombi ya kulitaka jeshi la Polisi kuwapeleka Dr. Slaa na wenzake mahakamani ambapo leo tungepangiwa jaji atakayesikiliza maombi yetu na kupewa wito wa mahakama (Summons) ili kuwaita wajibu maombi yetu .

Mimi nilisafiri kurudi Dar kwa ndege na kufika majira ya saa tano usiku.Hivyo kazi ya kufatilia tararibu nilizoeleza hapo juu nilimwachia wakili Jebra Kambore akishiikiana na Chengula na wenzake.

Muda huu nimepigiwa simu na uongozi wa Polisi Oysterbay -Dar es Salaam wakinijulisha kuwa Dr. Willibrod Peter Slaa wamemtoa Mbeya usiku na wako naye kituoni hapo. Hivyo nifike kwa ajili ya kufanya utaratibu wa dhamana yake.

Wakili Dickson Matata
18/8/2023 saa 10:07 Asubuhi

Pia soma
- Dkt. Slaa anadaiwa kusafirishwa Usiku huu (August 14, 2023) kuelekea Mbeya
Hii nchi inahitaji reforms kila eneo
 
Back
Top Bottom