Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Dr Salaa ni miongoni mwa watu waliokuwa na heshima sana nchini

Katika siku za karibuni Salaa amekuwa na 'project' ya kuharibu integrity and credibility yake

Kazi ya ubalozi ni kama asali, ameshailamba na sasa anataka kuchonga mzinga.

Dr ana uhuru wa kutoa maoni, kinachosikitisha ni maoni yaliyojengwa juu ya chuki
Chuki imeutawala moyo wake hata kufikia mahali ukweli anauona ni sumu kuliko chuki aliyobeba

Kuhusu TL , swali hilo anaulizwa mara nyingi na kila anapojibu wasomaji wanabaki ''WHAT?
''Waandishi'' humuuliza ku'push agenda bila kujua au kwakujua anafanya kile kilichokusudiwa

Anamsema TL kwa kuonyesha mfano wa 'Chadema walivyowahi kudhuriana'' .
Fact aliyo nayo ni kuambiwa na red brigade aliyekataa kumwambia kabla.

Dr Salaa anamaanisha tukio la TL kupigwa risasa lina utata ''hawezi'' kulizungumzia huku akiwa tayari kalizungumzia kwa tuhuma za red brigade. Nafsi inamsuta na anajificha ficha! anajua anachosema si kweli kina maumivu kwa Tundu Lissu na Rais wema duniani, anazunguka zunguka

Kila mtu anajua nani alifanya nini. CCM wanaomba maridhiano wasiyosema ni ya nini

Dr Slaa anajua masaa machache kabla ya TL kupigwa risasi JPM alisema nini

Mr Slaa anajua Camera zimeondolewa , Walinzi waliondolewa na hakuna uchunguzi
Hata waliojaribu kwenda kumsalimia TL baada ya risasi lukuki mwilini waliona cha mtema kuni.

Anajua matibabu ya TL yalizuiwa kwa makusudi

Badala ya kueleza mfano wa kipuuzi aliokutana nao Padr Slaa ange address controversies ambazo serikali haiwezi kuzieleza.

Tundu Lissu, Mhanga, anasema wazi waliopanga na waliotekeleza. Hakuna anayepinga hilo.

Dr Slaa anaweka doubt kwamba TL alishambuliwa kwa risasa.

Bwana Slaa amefikia kiwango cha chini sana kimaadili '' moral decay' kujidhalilisha

TL ni mlemavu , anaishi kwa maumivu ! Dr Salaa alitoroka kwasababu anawindwa.

TL hakuwindwa bali anaishi majeraha ya kuwindwa. TL ana makovu mwilini ana risasi imebaki

Dr Slaa anaamini kuna ufeki katika hilo, na kwamba, pengine ni wenzake! hatafuti fact tena

Dr Slaa unachokifanya kinakuondolea thamani ya utu., kwamba Uhai wa mwanadamu unautweza na kuuweka katika mizani na matamanio ya nafsi yako! upate mkate kwa kudhalilisha Utu.

Jaribu kuushinda ubinafsi ili uutukuze UTU! Uamini katika ubindamu si nafasi au teuzi!

Dr Slaa ukifungua mdomo jitathmini! sidhani kama umefikia kiwango hicho!


JokaKuu Pascal Mayalla Mag3
 
Siku hizi humu baada ya uzi ni matusi tu. Kwani mnaomtukana huyu mzee mnakosoa hoja ipi? Zamani watu wali quote sentensi na kupangua hoja! Mbona mambo mengi kaongea kwa ushahidi mzuri tu? Au mnataka kusikia yanayowasha masikio yenu tu!
Mnafiki ningeshangaa sana kama usingekuja kutetea huu utopolo wa Dr Mihogo kwa kigezo cha hoja,sasa hapo kuna hoja gani wewe mfuasi wa mungu mfu wa Chato?
 
Hahaha kudadeki ni kama vile slaa karukwa na akili # sio kwa mipumba hiyo 😁
 
Mama Muangalie huyu mzee. Hata ubalozi wa Ukraine ni bora.

Wandugu kushindia Mihogo sio kazi ndogo
Dr Slaa hawezi kushindia mihogo wewe.
Ana hela nyingi tu hata kuwalisha wewe na ukoo wako wote miaka yenu yote.
 
Dr. Slaa ni mkatoliki wa hovyo .
Ni Mdini sana.
kumpenda Kiongozi yeyote asiye mkatoliki. Na ndio ugomvi wake na Lowasa. Lowasa sio fisadi ni mtu aliyewekeza kutoka na fursa alizozipata kuanzia kwenye familia yake ,jeshini,kwenye Chama na serikali mpaka kufikia Waziri Mkuu. Ulitegemea awe maskini.

Slaa na Genge la wahuni wanaojificha nyuma ya Udini walimhofia sana Lowasa Mluteri kuwa huenda akaukwa uraisa mana jamii nzima ilikua inamkubali ndo waliotengeneza Mchongo na kumpaka matope.

Ndio maana awamu hii ya mama Samia Slaa anajitahidi kujitutumua ili aonyeshe kuwa serikali ya awamu ya SITA sio Bora kama ya awamu ya Tano. Tumemshtukia na kumpuuza. 2025 ni Mama Samia TU mpaka 2035 ,hivyo kama Slaa anaota urais anajidanganya kama kula chakula ndotoni.
 
Hizi ndio hoja za kumuuliza atoe maoni. Walau wewe umeibuka na hoja ya msingi. Dr Slaa kwa principles zake za kusimamia ukweli, hili la Lissu hajalisemea kwa viwango tunavyotegemea kwa levels zake.
Principles zipi anasimamia au zile za human rights sio kipaumbele cha Watanzania?
 
Hizi ndio hoja za kumuuliza atoe maoni. Walau wewe umeibuka na hoja ya msingi. Dr Slaa kwa principles zake za kusimamia ukweli, hili la Lissu hajalisemea kwa viwango tunavyotegemea kwa levels zake.
Alafu huyu alikuwa padre ila ndio hivyo muongo muongo.Ata sijui kama huwa anatubu dhambi zake
 
Ile kesi ya mwenyekiti ya Ugaidi jamaa hakuwa ameaingiziwa. Ilikua kweli. Ila hakukua tu na water tight evidence.

Hii ni kashfa kubwa kwa chadema kuwa kuna mambo wanayafanya kwa ajili ya kuichafua serikali.

Chama cha hatari sana hiki.
 
Siku hizi humu baada ya uzi ni matusi tu. Kwani mnaomtukana huyu mzee mnakosoa hoja ipi? Zamani watu wali quote sentensi na kupangua hoja! Mbona mambo mengi kaongea kwa ushahidi mzuri tu? Au mnataka kusikia yanayowasha masikio yenu tu!
Washamba,wajinga wamevamia jukwaa mkuu enzi za kina kibunango, mzee mwanakijiji, spiderman, na wengine akiwemo le mutuz field Marshal ungeona huu upuuzi?
 
Wewe ndo mdini na si Dr.slaa
Ukiweka akili sawa na kuondoa mind set ya dini utamuelewa vizuri tu.
Nitarudi badae baada ya kula daku
 
Utekaji,mauaji,utesaji ulikuepo Tangu nchi hii inapata uhuru na hata Sasa.Labda wewe muhamiaji tu ndo unaona mpya.

Nakukumbusha tu,Dr Slaa anasimamia msimamo uleule.Hakuna kumung'unya maneno mbele ya fisadi na Sasa kasema wazi umerudi na CDM pia hupokea mafisadi.Mbona Yuko wazi sanaaa,Tatzo nchi hii mnaona KILA mtu ni mfia vyama
 
Udini kusema ufisadi umerudi au?We ni mgeni nchii hii kushangaa Dr.Slaa kuongelea ufisadi?Wewe ndo mdini ulokosa hoja,unafikiri KWA kutumia mgongo wa dini
 
..lakini huko nyuma walikuwa wakifanya kwa kujificha-ficha.

..awamu ya 5 ikawa ndio kama sera yao wakawa wanafanya kwa kutamba kwenye majukwaa.

..hivi ktk hizo awamu zilizopita uliwahi kumsikia kiongozi wa Ccm akibwatuka kauli za kikatili kama alivyokuwa akifanya Kheri James?
 
Nakukumbusha tu maana umesahau hata juzi juzi tu mwangosi ulikuaje?Dr ulimboka unajua nani alimng'oa kucha?Abson kibanda?Mwakyembe?wafanya biashara wa madini?Mashekhe wa uamsho?,bomu la mkutano wa CDM Arusha?Unajua Ulemavu wa mkono wa Dr.Slaa ameupata wap?Na wengine wengi?Walikua wamejificha?

WaTZ wepesi kusahau sanaaa,Juzi mwezi wa12 tu hapa vijana wa4 hawajaonekana Hadi leo,na wengine wanazidi kupotea lakini Mnaleta hoja nyepesi tu.Nyinyi mmeimbishwa hoja na mafisadi na mmeipokea na kucheza Ngoma msiyo ijua,na Sasa mnaona aibu
 
Mimi kila nikiwaza kuwa ni Kwa Nini Tundu alipigwa risasi nakosa jibu kabisa , alikua na kosa Gani la kustahili kupigwa risasi nyingi vile ? Ni unyama wa Hali ya juu.

Dr. Slaa kumbe ni kati ya watu katili sana sana Duniani . Nimemchukia sana !
.
Kufurahia na kushabikia BINADAM Mwenzake kupigwa risasi na Majambazi( potelea mbali kama sio state mission ) Hata kama alipigwa na Wenzake wa Chadema hakustahili kupigwa na hakuwa na Madhara yoyote Kwa Chadema mpaka apigwe risasi.
Ni kweli kabisa kuwa kama uchaguzi 2020 ungefanyika Kwa uhuru kidogo kama ule wa 2010 alipogombea yeye basi Tundu angemgalagaza sana mgombea wa CCM.

Mihogo na PhD yake amesahau jinsi Lisu alivyokua ananyimea mpaka kutumia Helkopta kwenye kampeni na kutishiwa kuuawa wakati wa kampeni na kuchonwa sindano ya sumu huku akifungiwa asifanye kampeni . Lisu alimuacha mbali sana Slaa kwenye kampeni 2020. Hata Zanzibar alipokelewa Kwa shamrashamra kubwa ukilinganisha na mihogo 2010.

Ingetosha TU Kwa Slaa kusema kuwa suala la Lisu lilikua na utata hivyo uchunguzi huru ufanyike ili ukweli ubainike na wahusika wachukuliwe hatua
 
Kwani ndiyo yule og,au wa baada ya kuungana na Wana chukua chako mapema.
 
Slaa ameongelea kuhusu CAG report na kusema kuwa sababu moja ya kutaka kuwa isiwe public mpaka itakapojadiliwa na Bunge ni kuepuka vitu kama risiti iliyohojiwa kupatikana baadae.
Huu ni upotoshaji mkubwa na unaweza kuzungumzwa tu na mtu asiyejua taratibu za pesa za umma. CAG anapokagua hesabu anawaambia wahusika dosari alizoziona katika kikao chake cha mwisho na aliowakagua. Baada ya hapo anaandika formal report ambapo anaainisha mapungufu yote alioyaona. Hizo zinaitwa Audit Queries. Audit queries zinajibiwa na accounting officer, ambae anamuandikia CAG. Kama ana risiti anaziambatanisha. Accounting Officer hata siku moja hajibu Bunge moja kwa moja. Bunge wanachoweza kufanya ni kumtaka Accounting Officer atoe majibu haraka kwa CAG.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…