Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Huyo joseph kiongozi temeke ndo yule joseph yona kada wa CCM waliyemuokota ununio??? Km ndo huyo inawezekana ikawa kweli coz huyo jamaa mwaka wa sita huu analalamika ingawaje kesi yake ilikuwa kutembea na mke wa mchadema mwenzake
 
Mzee Dishi limeyumba.
200 (13).gif
 
Hajielewi vuguvugu Moto au baridi!?
Angekuwa balozi huko alikokuwa wala asingeongea haya!

Eti wafanyabiashara wengi wakirudi nchini, atutajie Nani Kwa mfano!!?

Utasikia maslahi mapana ya nchi! My foot!
So angeshinda uraisi angeongea haya Leo!! Si ajabu angewapa hao red brigade kazi za kumlinda Ikulu?!

Sometimes huhitaji kubwabwaja ovyo, kukaa kimya nayo ni heshima!
Tukuulize wafanyabiashara gani walikimbia na sasa wamerudi? Saizi Uber na Bolt wamekimbia! Nitajie kipindi cha Magu mfanyabiashara gani alikimbia kama sio kwamba wewe ndo unabwabwaja?
 
  • Thanks
Reactions: nao
Mdini sana huyu Mzee.
Kila akitokea Kiongozi Muislam Dr. Slaa anapanua mdomo Kama Chai Jaba.

Hivi haoni kuwa uhuru wa kisiasa ndio unampa fursa ya kuzungumza na kutetea Chama chake Cha UP.!!
Hatapata wanachama ndio atajua kuwa yeye SI chochote si lolote ndani ya CCM Wala Chadema.

Hawezi kupata wanachama hata laki Moja.
Kama anabisha 2025 achukue fomu agombee aone kuwa Watanzania sio wajinga.

Yani mpumbavu sana huyu Slaha mihogo ,amesahau watu walivyopoteza maisha Kwa maandamano aliyokua anayaratibu akiwa Katibu mkuu wa Chadema.? Amesahau kuwa Kuna watu walikua wanafungwa Kwa sababu ya kutaka haki hasa wakati wa uchaguzi ?

Hivi huyo Slaa haoni kuwa Afrika hakuna mtu anayetegemea serikali kula? Hata kabla ya hizi takataka za kikoloni zinazoitwa serikali na maendeleo kuja Afrika waafrika walikua wanatafuta chakula Chao wenyewe. Sasa kusema kuwa Katiba haimpi mtu chakula mezani ni kuwadharau watanzania. Yeye ndiye anayepewa chakula mezani lakini wanyonge wanajitafutia wenyewe hawahitaji serikali iwape chakula. Hata somalia pasipo na serikali watu wanaishi. Watu wanataka haki tuu. Watu wanataka wapate haki sawa mbele ya vyombo vya dola lakini haki ya kupanda na kufikia ndoto zao za kisiasa bila kuzuia na Dola Kwa sababu ya kulinda CCM pekee. Watu wanataka CCM iwekwe madarakani kihalali na waonyesha hayo waliyofanya sio Kwa kubebwa na Polisi na Tume.

Kama Dr. Slaa hajui ugumu wa kuendesha shughuli za kisiasa chini ya Katiba iliyopo basi Hana tofauti na mtoto wa kishetani anayemtoa baba yake kafara ili apate Mali.
Afrika Ina laana mbaya sana kuwa na wanasiasa wanafiki wanaojali matumbo yao.

Waafrika wanapigania mtu badala ya falsafa.
Kwa nchi yetu na Katiba iliyopo ni Bora TU Dr. Slaa akae kimya ale alichopewa na serikali ya CCM mana kama ana ndoto za Urais basi anajidanganya. Haiwezekani hii nchi akabidhiwe padri muasi. Mtu aliyemuasi Mungu hawezi kuwa mwaminifu Kwa wanadamu ndio maana hazungumzii haki. Kazi ya serikali ni kutenda haki.
Maendeleo ni Kodi za Wananchi wenyewe sio hisani. Haki ndiyo itakayowafanya Watanzania wapate mrejesho wa Kodi yao.

Leo Slaa amesahau kuwa wabunge na kamati zao wamekua wakihongwa ili watetee wezi ? Amesahau Sakata la Jairo. Leo anamfunga mdomo Zito wakati Kuna utata. Alikufa ni Magufuli Sasa Kuna dhambi Gani kuwajibishwa wasaidizi wake walioiba wakati wapo.? Hofu yao Nini kama sio kweli wezi wapo. ?
Magufuli alikua ni Rais lakini alikua na wasaidizi ambao ndio walioipaka matope serikali yake , wawajibishwe wao sio hayati. Aliwaamini wakamwangusha na kumpa ripoti za uongo.

Tunajua Slaa ni lile kundi lisilomkubali Mama Samia ndio maana anazunguka zunguka TU na vijembe vyake akidhani kuwa mama naye anaipenda hii katiba mbovu. Mama ni Mpenda haki na Demokrasia. Hakuna mpenda haki anayeamini katika katiba inayowafanya watawala kuwa miungu. Rais anakua na mamlaka makubwa kuliko Mungu kwenye nchi iliyoumbwa na Mungu . Haya maisha ni ya kupita TU hakuna haja ya kujisahau kama hao wazee wanavyojisahau wakidhani wataishi milele.
Na wewe ni pimbi tu kama pimbi wengine! Kwa hiyo kwa kuwa wewe unamshabikia mama Samia kwa kuwa muislam wenzako ndo Unafikiri watu wote wanaomkosoa ni kwa kuwa wanachuki za kidini?
 
  • Thanks
Reactions: nao
Kupigwa risasi Lisu sio jambo la ajabu Bwana tuacheni! Kila siku jambo lile lile!
Mimi kila nikiwaza kuwa ni Kwa Nini Tundu alipigwa risasi nakosa jibu kabisa , alikua na kosa Gani la kustahili kupigwa risasi nyingi vile ? Ni unyama wa Hali ya juu.

Dr. Slaa kumbe ni kati ya watu katili sana sana Duniani . Nimemchukia sana !
.
Kufurahia na kushabikia BINADAM Mwenzake kupigwa risasi na Majambazi( potelea mbali kama sio state mission ) Hata kama alipigwa na Wenzake wa Chadema hakustahili kupigwa na hakuwa na Madhara yoyote Kwa Chadema mpaka apigwe risasi.
Ni kweli kabisa kuwa kama uchaguzi 2020 ungefanyika Kwa uhuru kidogo kama ule wa 2010 alipogombea yeye basi Tundu angemgalagaza sana mgombea wa CCM.

Mihogo na PhD yake amesahau jinsi Lisu alivyokua ananyimea mpaka kutumia Helkopta kwenye kampeni na kutishiwa kuuawa wakati wa kampeni na kuchonwa sindano ya sumu huku akifungiwa asifanye kampeni . Lisu alimuacha mbali sana Slaa kwenye kampeni 2020. Hata Zanzibar alipokelewa Kwa shamrashamra kubwa ukilinganisha na mihogo 2010.

Ingetosha TU Kwa Slaa kusema kuwa suala la Lisu lilikua na utata hivyo uchunguzi huru ufanyike ili ukweli ubainike na wahusika wachukuliwe hatua
 
..Dr hazungumzii tena kuhusu mke wake kujeruhiwa na polisi, ameungana na Ccm waliotuma Polisi kumshambulia.

..lakini kuna tofauti kati ya awamu ya 4 na ya 5 ktk mambo haya ya ukatili. Hoja yangu ni kwamba awamu ya 5 walikuwa wanafanya waziwazi na ndio maana nasema walivuka mpaka ukiwalinganisha na wenzao huko nyuma.

..kuhusu Mwakyembe kwanini hakufuatilia suala lake la kuwekewa sumu? Mwakyembe si alikuwa waziri wa sheria nini kilimzuia?

..Magufuli naye anadai alilishwa sumu kwanini hakuwakamata wahusika alipokuwa Raisi? Hivi inawezekana Magufuli awashughulikie wapinzani na kuwaacha waliomlisha sumu?

..Ni kweli awamu ya 4 walifanya ukatili, lakini wao walikuwa tofauti na awamu ya 5 kwasababu walifanya kwa kificho. Awamu ya 5 walifanya waziwazi na walihalalisha ukatili wakidai wanashughulikia wasaliti.
Dr Ulimboka alitekwa!,Mwangosi aliuawa,Dr Mvungi aliuawa,Chacha Wangwe aliuawa kuna usiri wowote hapo wewe kichwa panzi? Utakuwa umezaliwa juzi?
 
Watu badala wa mjibu Dr kwa hoja wanaanza mkejeli hii inatafsiri gani kwa wanasiasa wetu hasa vijan?
 
Hakuna aliyejua hili ! maandishi na matamshi yake yanaondoa shaka kuhusu uadilifu wake

D Slaa bado anashaka kama kweli TL alipigwa risasi! Slaa kapatwa na nini?

Mwangosi (pumzika kwa amani) alipigwa risasi mbele ya Dr Slaa na Polisi.
Hadi leo haki haijatendeka kwa aliyefanya unyama ule
Mkewe Dr Slaa alipigwa na Polisi na kuvuja damu.

Leo Padre Slaa ana shaka kama kweli TL alipigwa risasi na kama alipigwa pengine ni chama chake.

Bila haya hata kidogo anadiriki kutoka mfano wa kipuuzi!! mfano wa kitoto na kijinga sana alioutengeneza ili kuhalalisha mauaji au maumivu anayopitia TL.

Slaa hana chembe ya Utu anatafuta mkate kwa kushabikia uvujaji damu, ana push agenda kwamba TL hakushambuliwa na 'wasiojulikana''. Huyu aliyelalamika kuwekewa vinasa sauti Dodoma leo haamini mwenzake anayetembea kwa kuchechemea kwamba kadhulumiwa!

Dr Slaa kapoteza utu, ubinadamu , integrity and credibility yake, anaonekana msema hovyo

Acha kushabikia mauaji , kusukuma agenda uteuliwa katika bodi! Teuzi na vyeo ni mapito tu.

Wewe na mwendazake nani wa kumsaidia mwenzake?
Huenda Slaa ameamua kiusafisha awamu ya 5 dhidi ya hizo tuhuma maana alikuwa mtumishi wake.
 
Tukuulize wafanyabiashara gani walikimbia na sasa wamerudi? Saizi Uber na Bolt wamekimbia! Nitajie kipindi cha Magu mfanyabiashara gani alikimbia kama sio kwamba wewe ndo unabwabwaja?
We mlinda legacy ya mzimu niambie wapi nimeandika kuna wafanyabiashara waliondoka sasa wamerudi!?

Mwambie huyo Slaa atutajie hao wafanyabiashara ni kina nani? Waliondoka lini? Walirudi lini?

Slaa aache njaa! Ubongo wake sasa unakoelekea, atapoteza heshima aliyokuwa nayo miungoni mwa jamii kitaifa na kimataifa!

Polisi wamkamate achunguzwe na ikibidi afunguliwe mashtaka. Kujua uhalifu na kuficha ushahidi juu ya uhalifu ni kosa kisheria!
 

Mwanasiasa Willbrod Peter Slaa amefanya mahojiano na kuzungumza mambo mengi kuhusu siasa, mahojiano haya ni mwendelezo ya interview aliyofanya wiki iliyopita.

TAARIFA YA CAG INAPOTOSHWA
“Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zito Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu.

“Moja ya maelezo ya ile sheria inasema baada ya CAG kukabidhi ripoti yake kwa Rais kisha kuifikisha Bungeni siku saba baadaye, ripoti hiyo haitakiwi kuwa public discussion, kwa kuwa ni kama mhtasari tu wa ripoti.

“Inatakiwa Kamati ya Bunge ndiyo iifanyie kazi, mfano kuna sehemu unaweza kukuta risiti haikuonekana wakati wa ukaguzi lakini hiyo ikapitishwa na kuonekana ni wizi, tumepotosha maana ya ile taarifa ya CAG.

CAG AMESABABISHA TAHARUKI KWA RIPOTI YAKE
“Kwanza hata CAG mwenyewe amechangia kuleta hii taaruki kwa kuwa huwa ni ya awali tu na analijua hilo, inatakiwa irudi kwa akaunti ofisa wa Serikali ijadiliwe, pia CAG wakati anatoa taarifa zake hadharani hatakiwi kuingia ndani kutoa ufafanuzi zaidi kama anavyofanya.

“Unaweza kukuta ripoti hiyo ikifika kwenye Kamati ya Bunge vitu vingi vikawekwa sawa, mfano labda kulikuwa na upotevu fulani wa mambo madogomadogo ambayo kwa nje yanaonekana kama ni wizi lakini details zikiwekwa sawa kunakuwa hakuna tatizo.

UBUNGE WA KINA MDEE SPIKA HANA KOSA, NITAZUNGUMZA CHADEMA WAKISHAKAA KIKAO
“Nimeona kwenye vyombo vya habari kuwa watajadiliwa na chama chao katika rufaa yao, naona lawama zimepelekwa kwa mtu ambaye hausiki (Spika).

“Chama kilitakiwa kufungua kesi Mahakamani kuhoji Tume ya Uchaguzi kwa kupitisha majina hayo lakini sijaona kesi. Mimi nitazungumza baada ya rufaa yao kupitiwa na CHADEMA, nimesikia wanakaribia kuwajadili kwenye kikao chao.

HOJA YA KATIBA SIYO MAHITAJI MUHIMU YA WANANCHI
“Mabosi wa vyama vya siasa ni wananchi, wanatakiwa kujiuliza wanayoyafanya yanawagusa vipi wananchi, kwa sasa kuna mambo mengi ya muhimu lakini hivyo vyama vimekuwa bize kuzungumza habari za ajenda ya Katiba.

“Hawana ajenda ambazo mwananchi anaweza kujiuliza kama inaweza kuweka chakula mezani, hakuna katiba ambayo inaweza kuzungumzia kila kitu.

“Katiba yetu ina vipengele vingi vya muhimu lakini havitekelezwi, japo sijasema kuwa katiba siyo muhimu.

“Mimi ni kati ya watu waliozunguka Tanzania kukusanya maoni lakini tusipotoshe kuwa katiba ndiyo jibu la kila kitu, siyo kweli.

“Leo hii Marekani ina katiba tunayoisifu lakini Donald Trump si alishutumiwa anataka kufanya mageuzi.

KATIBA PENDEKEZWA NI MBOVU KULIKO KATIBA YA SASA
Sisi tuna maoni ya Jaji Warioba, licha ya kuwa kulikuwa kuna mambo yamekosekana lakini yapo mazuri ambayo tunaweza kuyatumia.

“Baada ya maoni hayo kupelekwa Bungeni ikachujwa ikatoka inayoitwa Katiba Pendekezwa, ni mbovu kuliko hata katiba tuliyonayo sasa hivi.

SIZUNGUMZII SUALA LA LISSU KUPIGWA RISASI SABABU UTEKAJI ULIKUWEPOA CHADEMA
“Kuna watu wananiuliza kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, kuwa sipendi kulizungumzia hilo kwa kuwa sita taarifa zake za uhakika.

“Nitoe mfano iliwahi kutokea huko nyuma nikiwa Katibu Mkuu CHADEMA, nililetewa taarifa za mtu wangu anaitwa Joseph, huyu alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, alitekwa saa sita usiku. Kesho yake saa sita mchana nikahitisha mkutano na waandishi wa habari nikaisema sana Serikali na Usalama wa Taifa.

“Saa nane mchana siku hiyohiyo Joseph akapatikana, alikutwa ametupwa maeneo ya Ununio ameumia sana usoni.

“Mwezi mmoja baadaye kijana wangu wa Red Brigade anakuja kwangu kuniambia yeye ndiye aliongoza kukosi cha kwenda kumteka nyara huyo mwenyekiti huyo.

“Nikauliza kwa nini hakuja kwangu akasema ‘wapo viongozi wanaojua’, nikaamua kunyamaza, ndiyo maana ninapoulizwa suala la Lissu ninasema hapana, CHADEMA kwanza wajiangalie wao ndani.

“Huyo kijana (Joseph) walivyomtupa ufukweni walijua amekufa, kumbe alikuwa hajafa labda upepo ulimpiga akaamka. Miaka kadhaa baadaye tukaanza kusikia watu wanaokotwa wamekufa ufukweni, unadhani inatoa pcha gani!

“Ukiwa kiongozi lazima uwe kunasema ukweli hata kama unaona watu wako wanakosea.

SINA TATIZO LA LOWASSA
“Mimi na Lowassa tulipishana kwenye principal siyo maisha, mimi niliwahi kufanya fund rising na Jakaya Kikwete siku moja baada ya kupanda jukwaani na kumsema tena kwa mambo mazito.

“Nimeishi Ulaya, nimeona mambo ya kwenye mabunge, kuna muda inafika hatua wabunge wanapigana ngumi lakini wakitoka wanaenda kunywa bia. Unatakiwa kutofautisha maisha binafsi na siasa. Hivyo sikuwa na tatizo binafsi na Lowassa.

AWAMU YA TANO HAIKUFELI DIPLOMASIA YA KIMATAIFA
“Watanzania tuwe wakweli, tumefeli wapi, mimi nimekutana na wafanyabiashara wengi, wapo walioniambia wamchoshwa na Tanzania yenye ufisadi.

“Wapo walioamua kuondoa biashara zao huko nyuma lakini katika awamu ya tano waliamua kurejesha biashara hapa nchini, kwa nini? Ni kwa sababu kulikuwa kuna mambo mengi yanaenda vizuri, nazungumza kwa kuwa najua zaidi kilichokuwa kinaendelea.”



Chanzo: Dar24
Wenye akili tulijua kuwa Lissu alitaka kuadhibiwa na Mbowe.
 
Rudi huko zamani
Siku hizi humu baada ya uzi ni matusi tu. Kwani mnaomtukana huyu mzee mnakosoa hoja ipi? Zamani watu wali quote sentensi na kupangua hoja! Mbona mambo mengi kaongea kwa ushahidi mzuri tu? Au mnataka kusikia yanayowasha masikio yenu tu!
 
..Dr.Slaa amesema nini kuhusu ubaguzi, utesaji, utekaji, na mauaji, ktk awamu ya 5 ?

..Umesahau kwamba Dr.Slaa aliwahi kusema kuwa akipata madaraka atamfunga Dr.John Magufuli?

..Dr alitakiwa kuanzisha chama au kujiunga na chama kingine cha upinzani lakini sio kujiegemeza Ccm.
Kesi za kubambikiwa,
Malipo yaliyokuwa hayaendi serikalini,

Njaa na hana maisha, Yule ya kujitetea apate ugali kamuacha yatima!
Angejua angebakia Canada akipiga box. Hadhi yake ingeendana na haya anayoyaropoka sasa!

Ana kinyongo hakuwa mgombea wa urais, mamvi alimpiku!

Sikutegemea huyu babu aweza kuficha uhalifu mkubwa na wahalifu!
 
Siku hizi humu baada ya uzi ni matusi tu. Kwani mnaomtukana huyu mzee mnakosoa hoja ipi? Zamani watu wali quote sentensi na kupangua hoja! Mbona mambo mengi kaongea kwa ushahidi mzuri tu? Au mnataka kusikia yanayowasha masikio yenu tu!
Ushahidi uko wapi hapo?
 
Tunakushukuru sana Mungu kwa kutuondolea huyu Mamluki Chadema
Hao ndio walikuwa wenye chama lakini tamaa ya mwenyekiti na shekeli ,ikapoteza Dira ya chama.
Ingekuwa uongo asingeweka hadharani,ila kama mnabisha nyinyi kina Erythrocyte nendeni mahakamani mumfungulie kesi ya kuwaharibia image ya chama.

Kisha muone atakavyowaadhirisha kwa evidence.

Slaa ni mtunza Documents mzuri.
 
Back
Top Bottom