Dkt. Slaa: Nitaendelea kusema ninachoamini, asema hajutii kuondolewa hadhi ya balozi

Dkt. Slaa: Nitaendelea kusema ninachoamini, asema hajutii kuondolewa hadhi ya balozi

Dkt. Slaa ameongea na mwananchi baada kuondolewa hadhi ya ubalozi, Slaa amesema taarifa hizo nae ameziona kwenye mtandao lakini hajutii chochote na nchi alizotumikia wanajua walikuwa na balozi wa aina gani.

Amesema alipewa ubalozi na sasa wamechukua, hawezi kuhoji lolote. Alipoulizwa na mwandishi endapo kuondolewa ubalozi kama umehusiana na ukosoaji kwenye mkataba wa bandari, Dkt. Slaa amesema anajitambua na ataendelea kusema kweli na kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria.

Pia, Soma => Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa

Hata sisi watuondolee uraia wetu tuone na wachukue vyeti vya kuzaliwa tuone .
 
Ila Mama Abdul ameji expose sana kwa watu wenye akili timamu...ni mtu wa visasi sana & mnafki, tukumbuke pia yalianzia kwa Ndugai.
Ye anataka kusifiwa tu hata pale anapoboronga...ndio maana wahuni wamejua mapungufu yake wanamsifia kijinga anawapa vyeo kama asante.
Jinga kabisa!.
Kwa hiki Rais alicho fanya, kina tufanya tuamini ile kesi ya uhaini, ili asisiwa Ikulu.
Huwezi kumfutia mtu hadhi yake ati kisa ana sema ukweli.
Hii nchi ina vitu vya ajabu sana.
 
Kwenye siasa hakuna adui au rafiki wa kudumu...

Hata CCM wapo watu kibao ambao nyuma walishawahi kuondoka CCM kwa mbwembwe na sasa wapo CCM wakiwa na vyeo au hadhi kubwa tu...
mfano ni mwenezi dar, marioo binamu
 
Kumuondolea ubalozi imethihilisha kuwa,ukiwa serikalini hata kama kuna mambo ya kipuuzi hutakiwi kusema kuwa serikaliimekosea.wanataka wasifiwe tu
Karejee kiapo chake aliapaje. Lkn haishangazi alivyunja kiapo cha upadri, akavunja cha chadema, akavunja cha Rozi Kamili, akavunja cha mshumbusi, sasa cha ubalozi.
 
Kuna mambo ya ajabu sana yanaendelea kwenye hili Taifa
 
Tuache udhaifu wa Dkt. Slaa. BW. Rostam, katika dhana ya uwekezaji wengi kama sio watu wote wanakubaliana nawe. Kitu kimoja tu umejitahidi kutokukiwekea uzito pamoja na kujaribu kukigusia juu juu, nacho ni vifungu vya mkataba vinavyoibana zaidi nchi. IGA ndio msingi wa mikataba mingine. Kama msingi ni dhaifu, yatayofuata yote hayatakuwa na tija. Hii ndiyo hoja iliyoko mezani na sio DPW kama mwekezaji.
 
Dkt. Slaa ameongea na mwananchi baada kuondolewa hadhi ya ubalozi, Slaa amesema taarifa hizo nae ameziona kwenye mtandao lakini hajutii chochote na nchi alizotumikia wanajua walikuwa na balozi wa aina gani.

Amesema alipewa ubalozi na sasa wamechukua, hawezi kuhoji lolote. Alipoulizwa na mwandishi endapo kuondolewa ubalozi kama umehusiana na ukosoaji kwenye mkataba wa bandari, Dkt. Slaa amesema anajitambua na ataendelea kusema kweli na kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria.

Pia, Soma => Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa

Angekuwa hajutii angekaa kimya.Ujuwe hapo anajutia.Kachezea ahilingi chooni.
 
Unafiki sio kitu kizuri.
Mzee slaa aliwasaliti CHADEMA mbele ya JPM kwajili ya tumbo lake, leo hii tena wapo pamoja kwenye jukwaa la kisiasa.
Mbowe na Lema wanapaswa kujitafakari sana, sio kwamba wanachadema wamesahau ila ...
Chadema hawakumsaliti slaa kwa kumsimamisha lowassa????
 
Back
Top Bottom