Dkt. Sule: Kutumia Majini kupata Mali si dhambi/ haramu

Hakuna malaika walioasi, malaika wameumbwa kwa nuru na majini wameumbwa kwa giza la kivuli cha moto, majini ni majini na malaika ni malaika, na wao wameumbwa kuwa watiifu na majini wamepewa utashi kama sisi, ukitaka tii ukitaka asi na moto uko mbele yako.
 
Acheni unafiki mizimu ni majini.....sasa km sio makabila yote yanaamin mizimu sasa kwann muogope majini
 
Mbona kama story zako tu unamwagika hapa bila hata ushahidi wa aya
 
Na ni bora umeandika Allah anajua zaidi umetokea hapo. Vinginevyo unahitaji kujifunza dini zaidi na zaidi kuna vitu vingi hujui, japo alhamdulillah kwa iliyonayo ili kabla kupinga jifunze zaidi.

Huyo Sule huwezi kumpangua kwa hoja na kwambia wewe hapa umeonyesha kumdharau lakini kahifadhi Quran nzima moyoni na kichwani pia kahifadhi biblia nzima kichwani iweje umbeze jana kwamba hana kitu? Acha kabisa hilo

Kuhusu majini Dkt Sule yuko sahihi Kama muislam ana elimu kuhusu nayo pasi na kumshirikisha Allah basi anaweza kufanya nayo kazi kwani Nabii Suleiman majini na binadamu ndio waliojenga hekalu alikua akiwasimamia na alikua na akiwapangia kazi mbalimbali kwa jinsi anavyotaka na Allah ametwambia Nabii hakukufuru.

Aya nitakuwekea inshaallah
 
Ona huyu mwingine anaropoka uongo.
Katika uislam majini ni viumbe walioumbwa kwa moto,malaika ni viumbe walioumbwa kwa nuru/nyota.
Hawafanani kamwe.
Mtume ufunuo aliletewa na malaika/kiumbe kilichoumbwa kwa nuru ama nyota.
Majini wapo wema na wapo wabaya.
Majini wabaya ndio hao mashetani au mapepo.
Usiokoteze uongo kutoka kanisani kwenu na kuleta hapa.
Matako yako.
 
Ukifutwa uislam,hao walio baki hawatumii majini? Jiulize aliechora dunia bila hata darubini au kuwa Nga za mbali aliwezaje?,
Tunachojua ni kwamba jini lilimchorea ramani na yye kafanya uhakiki kama ni kweli.
 
Naona wagalatia wanakuja mbio na matusi pasi na kujua Sule kazungumza nini.
Mleta mada ungeweka video watu wasikilize sio kuleta maneno baadhi yenye mkanganyiko.
Sule alichosema ni kuwa kuwatumia majini wenye mali kupata mali sio haramu.
Ila katika kuwatumia huko ni kwa kumuomba Mungu hao majini watii kwa kupitia neno la Mungu.
Kuna majini wanashikilia mali za dhahabu,almasi,ruby.
Unawafanyaje watii wakugaie mali?
Ni kupitia visomo vitakaowafanya wanyeyekee kwa jina la Mungu.
Na Sule alitanabaisha kuwa sio kwa kutumia makafara kutoka kwa waganga na ukapewa mapepo ya kafara laa hasha huo ushirikina.
Ila kwa kutumia kumuomba Mungu ili uwanyenyekeshe majini hilo ni sawa.
Kama Nabii Suleyman alikua akiwanyenyekesha majini kwa kumtaja Mungu maana Mungu ndio kaumba hao majini.
Narudia Sule hakukusudia kutumia mashetani ya kafara.
Kuna kitu katika uislam tunakiita Khadiim,maana yake mtumishi wa kiroho.
Hao watumishi wa kiroho wapo malaika na majini wasafi ambao huwezi kuwaona abadan mpaka ufanye utajo wa Mungu.
Na ukiwa mtu wa ibada sana katika masiku meupe hawa viumbe wanaweza kukutembelea pasi na wewe hata kuwaita ukashangaa wamekutembelea.
Niishie tu hapa ila kiufupi Dr Sule hajakusudia mashetani ya kafara.

Cha kuongezea,hao khudaam huwezi kuwafuga hawafugiki ng'oo.
Bali unawanyenyekesha na wakitimiza ulichoomba wanaondoka na mpaka warudi tena aisee ufanye kazi uache kazi.
Yani khadim ni sawa na nyota ya jaa.
 
kwa hiyo sule kuokoka inawezekana. Basi na iwe hivyo atoke kwenye giza na udanganyifu
 
Hao ni Majahili(Wajinga/Wapumbavu) tu wa Uislamu.

Amesema Mtume Wa Allah" Umeanza Uislamu ukiwa mgeni na utaendelea/rejea kuwa mgeni basi hongera kwa wageni"

Hao wanachanganya mila zao za mizimu kama Yericko Nyerere na Uislamu.

Huyo Sule ni mfanyabiashara wa dini (Tijaru dini) kama walivyo akina Mwamposa tu. Anatajirika kwa jina la dini, amekuwa mchawi(mfuga majini) mwenye jina la kiislamu.
 
Ukifutwa uislam,hao walio baki hawatumii majini? Jiulize aliechora dunia bila hata darubini au kuwa Nga za mbali aliwezaje?,
Tunachojua ni kwamba jini lilimchorea ramani na yye kafanya uhakiki kama ni kweli.
Mafala hao,hawajui kitu
Wakatafute kitabu/biblia iitwayo"CODEX GIGAS".
Iliandikwa karne ya 17 na warumi ina agano jipya na kale na ina sehemu ya kuwatiisha majini wazuri na kuwafukuza mapepo wabaya na kuwafunga.
 
Quran 27:17 Na alikusanyiwa Suleiman majeshi yake ya majini, na watu na ndege nayo yakapangwa kwa nidhamu.

Msingi wa wakuyatumia majini uko hapo binadamu mwenye elimu juu ya anachokifanya bila kumshirikisha Mwenyezi Mungu majini ni kama mbwa unatuma anakufanyia kazi zako sema wasio kuwa na elimu ni waoga kwakua hawana elimu na kuzusha vitu someni mjue
 
Ni Dkt 😄😄

Sema nyie na wanazuoni wenu hua mnachekesha sana. Yani huyo Sulle ukimsikia tu anavyoongea na jinsi anavyoelezea mambo unajua tu kichwani hamna kitu. Yani alichonacho ni confidence lkn kichwani ni patupu aisee
Dkt ..ukiwa na maana ya Medical doctor au Phd?
 
Na hao majini wa kuwatiisha hawafugiki mkuu.
Hao ukiwaita unaweza ukachukua hata miezi sita mpaka wanakuja.
Na wakija masharti yake huyawezi.
Na wakiondoka hawarudi tena labda uwe aswhaabul akhdaam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…