1. Uislamu una taratibu zake.
2. Dhambi kwenye uislamu Zina madaraja tofauti.
3. Kuwa muislamu ni kuwa na shahada mbili. Kwa maana yake halisi. Kwamba jambo lolote la ibada hutamfanyia mwingine yeyote ispokuwa Allaah. Na lazima uamini Muhammad ni mja na mtume wa Allaah. Si mwana wa Allaah wala mshauri wa Allaah. Yeye ni mwanadamu kama wengine. Ila yeye aliletewa ufunuo. Hivyo, kwakuwa yeye aliletewa ufunuo ndiye aliyetufundisha ibada,na jinsi ya kuitekeleza. Maana ya shahada ya pili ni kuwa,sitafanya ibada yeyote ila Kwa muongozo na kumuiga Muhammad.
Kwa maana hiyo muislamu ni yule anayeyafuata hayo kikamilifu.
Kinyume na hivyo unaweza ukatoka kwenye uislamu au ukahukumiwa kuwa si muisla. Na hili la kuhukumiwa lina taratibu zake. Na wanaoweza kutoa hukumu hiyo ni wanachuoni wakubwa waliobobea kwenye ilmu.(Kwa maana hiyo, Sule amekosea kutoa hukumu wakati yeye si mwanachuoni)
Wasio wanachuoni nafasi yao ni kukumbisha,kunasihi na kufundisha.
Harmonies sio mwanachuoni. Anapewa dharura ya ujinga. Hajui uzito wa maneno aliyoyasema. Atabaki kuwa ameasi Kwa kutenda dhambi kubwa hadi pale taratibu zitakapokamilika na kupelekwa suala lake Kwa wanazuoni.
Ama suala la muziki ni kweli ni haramu. Lakini halimtoi mtu kwenye uislamu.
Ama hadithi uliyoitaja kwamba ni mafundisho ya Mtume,si sahihi.
Bali Mtume aliulizwa kuhusiana na baba na mama, nani afanyiwe wema zaidi?
Akajibu,
Mama yako mara tatu ndio akajibu "baba yako" kwamaana mama anastahili kufanyiwa wema mara tatu zaidi ya baba.
Hivyo, Kwa mujibu wa Sheria ya kiislamu, konde boy kafanya kufru ila hajatoka kwenye uislamu hadi aukane uislamu mwenyewe au ahukumiwe na wanazuoni kwamba si muislamu.
Muhimu utambue kwenye uislamu Kuna kufanya tendo la kufru na Kuna kukufuru. Kama Ilivyo unaweza kufanya tendo la ushirikina na kuwa mshirikina. Ni vitu tofauti.