Dkt. Tulia Ackson: Mshahara wa Mbunge ni Tsh milioni 4.6 na sio vinginevyo

Bila shaka wewe sio salaried worker. The more you earn the higher the taxes. Yes, kuna watu wanalipa PAYE zaidi ya 30%.
 
Usiwe unabisha ndugu kama hufahamu omba watu wakueleweshe. Kodi kwa mishahara iliyo chini ya 1,000,0000 hukatwa kwa asilimia, mfano kima cha chini kodi ni 9%. Lakini mshahara wowote unaozidi 1,000,000 kodi huwa ni 130,000 + (30%x inayozidi kwenye 1,000,000). Mfano kama mshahara ni 4,500,000 basi kodi itakuwa 130,000 +(30%x4,500,000)=130,000 + (0.3x4,500,000)=130,000 +1.350,000=1,480,000 ambayo ni karibu na 1.5 milion.
 
MMH. Sijaelewa. Hivi hayo makato yao ni tofauti na PAYE?? Maana nikipiga kodi ya kipato cha TZS 4,600,000/- ni TZS 1,070,000/- (Hapo less NSSF). Tukisema hawakatwi NSSF kodi ni TZS 1,208,000/-. Namheshimu Naibu Spika lakini hapa unatupotosha….

Nimetumia verified calculator ya TRA.
 
Nilichokiona kwanza ITV haina watangazaji wazuri wa kuuliza maswali, pia huyu bibi anaongea kama vile watanzania wote ni wajinga kama waliopo jimboni kwake.
 
Milioni zote hizo kwaajili ya kupiga makofi tu na kusifia sifia , wakati daktari binmgwa anayecheza na makamasi yao wakati wanaumwa analipwa milioni moja na nusu, sawa bwana waendelee tu , wao ni wateule
 
Hilo fungu la mshahara wa Katibu wa mbunge na dereva wanakatwa kodi?

Kwanini Bunge linalipa mshahara wa watumishi wa mbunhe ambao mchakato wa ajira zao haujapitia kwao?
 
Mwamba Ngoma..
 
Atuambie tu serikali inatoa kiasi gani kwa mwezi kulipa wabunge wote? Hapo tutagawanya wenyewe namba haidanganyi. Aliebuni namba moja kwa moja peponi.
 

Kwamba?

"Watu wa nje ya Bunge wakipiga hesabu wanadai ni Tsh 11,0000,000 jambo ambalo sio kweli. Hizo hela zinapita kwa Mbunge japo zote sio zake."

Kwani ujumla ni ngapi basi? Au nayo ni siri kama agenda za Mrema?

Hizo hela zinapita tu kwa mbunge si zake bali za dereva, katibu wabunge nk. Hivyo hawa ndiyo hawalipi kodi au kichaka cha kukwepea kodi chenyewe?

Hiiiiii bagosha!
 
Nilikuwa Mbeya juzi juzi kwa kweli anasumbua sana na misafara yake kila mara,Mbeya yenyewe mjini barabara ni moja tu inayoingia mjini.
 
Wanafikiria wanaongoza ma nyumbu, Kwa mtu mwenye upeo timamu hawezi elewa mauchafu aliyoyazungumza.
Aweke salary slip yake na bank statement ndo tujue ukweli sio hizi porojo za kuzungumzia basic salary tu na akati kuna marupurupu kibao yanaingia kwa akaunti binafsi afu mnasema pesa za jimbo sijui kumlipa dereva, bulls**t.
Watu tunakatwa PAYE kwa hesabu ya gross pay yaani maumivu makali p*****v u zao.
 
Huyu "Naibu" ni mwanasheria nguri lakini anatumia "tekinikalitizi" kujitetea kuhusu hoja ya Mhe. Jerry Silaa. Ndugu zangu watanzania tutumie elimu zetu kusaidia nchi yetu. Huu utetezi sio sahihi. PAYE kwenye mshahara wa mfanyakazi haikatwi kwenye Basic Salary tu bali kwenye Gross Salary. Huu ndio ukweli na kama kuna watu wa TRA au watalaamu wa kodi watusaidie sio wabunge kuja kujitetea.

Ameongelea kuhusu mashirika mengine kulipwa zaidi. Ni kweli lakini hicho kikubwa wanacholipwa kinakatwa kodi chote. Yaani karibu mshahara wote unarudi serikalini kama PAYE! Kama ulipwa fuel, rent allowance, sijue responsibility allowance zote hizi zinachanganywa zote na Basic Salary yako na kukatwa PAYE yaani "kodi ya mapato kwa jinsi unavyopata".

"Naibu" anasema mbunge analipwa kila mwezi posho ya dreva, posho ya mafuta, posho ya wasaidizi wa mbunge, posho ya jimbo....na hazikatwi kodi! Hapa ndio kuna matatizo na wametumia neno "posho" makusudi! Haya yote ni mapato kwa mbunge ni lazima yakatwe kodi. Tujiulize swali kidogo hizo posho za dreva na wasaidizi wake akiwapa anawakata PAYE au kodi maana kama hawakati ina maana wanapokea mapato ya mwezi bila kulipa kodi. Hapo bado hatujaongelea posho za vikao kwa siku hizo sijui shs 120,000 kwa siku! Kinachonisikitisha sana ni kwamba tuna waandishi wa habari ambao kwa mtazamo wangu hawatendi kazi zao kiweledi.
 
Haya maswali ya msingi hawayataki kujibu wanakazana kuwapa wanaodiriki kusema adhabu...Are they for public or for their personal interests?

Hivi nikiwaza hii inaweza kuwa aina fulani hivi ya institutionalized corruption ili kupunguza makali ya wao kusimamia maslahi ya waliwachagua nitakuwa nimewaza vibaya?
 
Moja ya taasisi inayofilisi kodi za wananchi ni bunge
 
Kwanini hao watumishi wa mbunge wasilipwe direct na serikali kama watumishi wengine? hapo kuna ujanja ujanja mwingi sn
Hakuna mwenye jibu, labda viongozi wa hazina na Bunge.
 
Kodi ya mshahara wa shs 4,600,000 ni shs 1,208,000 na kabla ya July 2021 ilikuwa shs 1,210,500. Je kwa nini katoa hesabu isiyo sahihi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…