Uchaguzi 2020 Dkt. Tulia atema cheche Mbeya Mjini, awajibu Lissu na Sugu kuhusu maendeleo ya vitu watu wafurika mkutano wake

Aisee heshimuni kina mama!!
Matusi si kitu poa.
 
Umesema kweli Ndugu yangu. Huu mjadala hauna tija kabisa kwa nchi yetu maana ni wazi kabisa kuwa maendeleo ya watu hayawezi kuja bila kuendeleza vitu, yaani miundombinu ya kurahisisha shughuli zao; k.m. umeme, maji, usafiri, na rasilimali za huduma za kijamii yaani afya, elimu,n.k. Kwa hili Upinzani kubalini ili mjadala uwe namna gani tunaweza kuongeza maendeleo ya vitu kwa haraka maana tumechelewa sana. La sivyo mtaendelea kushika mabua kwenye bahari na bila shaka mtazama tuu maana Watanzania wanaelewa fika umuhimu wa vitu katika kuendeleza maisha ya watu.
 
Watu wa Mbeya sio wajinga kiasi hicho washindwe kutofautisha kati ya mtu na kiatu.

Kwamba watu wa Mbeya wachague Tulia wamuache Sugu?
Sugu kafanya nini kipindi chote cha ubunge wake?. Utashangaa wana mbeya wakimchagua tulia kwa kishindo.
 
Napendaga Ninasoma kwenye online media za Radio one, Nipashe na ITV. Kwenye mikutano ya CCM wanaandika Maelfu ya wananchi. Ila mikutano ya CHADEMA na ACT Zanzibar wanaandika mamia ya wananchi. Sijui wanaogopa nini jamani hawa watu
Uhuru wa habari upo likizo.. wanaogopa kufungiwa
 
Tatizo ni kwamba vitu hivyo kwa sasa vinanufaisha elite group tu, walalahoi wanabaki hoi! Pia kulikuwa na haja ya kuendelea kuboresha maisha ya watumishi wa uma, kuajiri nk, wakati ukifanya hayo mengine. Alafu kwenye umeme Kwanini tumeachana na mradi wa gesi ambao Kikwete aliufikisha pazuri, na gharama kubwa zilishatumika?!
 
Bibi hali yake mbaya ameanza kunyanganya bajaji na pikipiki huko mbeya,ilomba sai,veta kwa mama john nimepita week iliyopita akipata kura 1000 inaweza kuwa ajabu la 8 la dunia
 

wewe Barabara zetu wapite ? kodi unalipa wewe ?barabara ni kodi za watanzana sio za CCM
 
Kwa sasa Ccm haitakiwi kwa sababu ya mawazo yao ya kijinga kama haya
 
Nasikia wana mbeya wanamuita " atiku-papa" sijui ndio nini
 
Naona malori yaliyoleta watu hayako mbali hapo, lakini kwanini watoto wetu wasisome muda huu? kuna somo la uraia ndani ya maaarifa ya jamii kule shuleni watasoma maswala ya siasa huko
Hili la malori nimelishuhudia kwa macho yangu Lupiro wilayani Mahenge.

Watu wameswekwa kama ng'ombe kwenye fuso.
Nimeona distribution truck la pepsi lina pita kijiji kimoja kimoja, ifakara to Lupiro linakusanya wana chama tawala

Hivi kipindi hiki sheria za usalama barabarani huwa zinafutwa sijui?


Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…