Hatimaye September imefika ile ahadi ya bunge kujadili ufisadi na kuwawajibisha mafisadi walioibuliwa na CAG muda wa utekelezahi wake umefika!

Walioiba matirioni ya Watanzania tuwaone wakiwajibishwa na Bunge kisha kifunguliwa mashtaka Mahakamani!

Je, mwana JF unaamini Bunge hili la mafisadi na wezi litayawajibisha majizi?

Tulia huyu anaweza kuongoza mjadala wa kuwawajibisha wezi akiwemo mume wake?

Wacha tuone.
 
Hatujawahi kuwa na spika kiazi kama Tulia Ackson
 
Yaani ni kama katumwa na serikali kwenda kuzima hoja zote zinazohusu skendo za viongozi wa serikali bungeni. Huwa anaendesha hovyo hovyo mijadala bungeni, mbunge akisimama na hoja ya kuikosoa serikali anajifanya kumwelekeza namna ya kuongea ikiwa ni pamoja na kumuuliza maswali ya kipuuzi!! Kazi ya spika ni kusimamia mijadala na wala siyo kuwapangia wabunge nini cha kuongea na nini cha kutokuongea.

Yaani hivi vyeo vya kurithi hivi kwa kweli Watanzania awamu hii tumepatikana!!
 
Sahau maisha yako yote, hakuna mtumishi wa umma anaweza kuiba bila kuhusisha vigogo, yaani dokezo la mabilioni litoke Halmashauri liende hazina ndogo kisha BoT then bank bila serikalini kujua? hiyo sahau
 
Huyu ajuza hafai kabisa asee
 
Tjubutuuuu
Watajadili kwa povu nene kisha Bunge litahairishwa kusubiri vikao vijavyo
 
Watanyooshewa vidole wasaidizi wa wakurugenzi tu labda mkubwa mmojawapo awe hakunyoosha mkono wake kwenda kwa mkubwa mwenzie kugawana hizo bajia
 
Kamwe, haitatokea wezi na mafisadi kuwajibishwa na serikali ya CCM!! Anaepinga hili aje na majibu ya msingi!!! Zaid utasikia... Mkurugenz kakamatwa kwa upotevu wa milion moja na nusu lkn huez sikia kiongoz kakamatwa na kufikishwa mahakamani kwa upotev wa bilion 10+. Na aliesababisha upotev utasikia katolewa hapa kahamishiwa kule 🤣🤣🤣🤣
 
Ripoti ya CAG ilijaa madudu mengi na mpaka Mhe. Rais alichukia sana na kuahidi kuwa wale wote waliokutwa na ubadhirifu watachukuliwa hatua kali.

Bunge letu pia iliahidi kuwa katika kikao cha Bunge cha mwezi Septemba ripoti hii itawekwa hadharani na wale wote watakokutwa na ubadhirifu watachukuliwa hatua.

Sasa mbona mpaka sasa mambo ni kimya au ndo wamesamehewa? Nchi hii ..... iko kazi.
 
Ilishaisha hiyo.. Kuwaamini wanasiasa wa ccm kunahitaji wendawazimu above next level

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Speaker wa bunge anaendeshwa na mafisadi.

Hivyo speaker wa bunge letu ni FISADI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…