Kwishaa hbr, hakuna jipya tena hapo! Ni jamaa wajipange kupoteza documents!!! Lazima tukubali tu hakuna hatua zozote zitachukuliwa dhidi ya wabadhirifu na mafisad. Bali hatua zitachukuliwa kwa wale wa vimilion!! Na hao wa vimilion ni kwamba itafanywa... Toa gambe weka gambe!! Toa huyu hapa peleka kule lete yule hapa!! The life goes on...
 
Kwahiyo walio haribu na kuisababishia Serikali upotevu wa fedha waendelee kuharibu?!! hii ndio maana yake.

Mie nadhani Serikali kupitia mamlaka za uteuzi zinaweza kuchukua hatua kabla hata ya Bunge halijapendekeza nini Cha kufanya.

Upotevu umeonyeshwa na CAG halafu bado Tena tusubirie Kamati za Bunge ziwahoji ukweli wa yaliyo bainishwa na CAG?!!!!! Hakika kama ni Sheria basi Sheria hiyo ibadikishwe haraka sana maana huo ni uchochoro wa kuwanusuru wabadhiriifu wa fedha za umma.

Tunaiomba mamlka zichukue hatua, huo mchakato wa Bunge wa Kamati za PAC ni ucheleweshwaji wa muda kana kwamba alicho kibaini CAG hakina ukweli.

CAG ni Jicho la Serikali, limeona ubadhirifu, uzembe na wizi!! kwahiyo PAC inanguvu kuliko CAG?!!!!

Hili ni jaribio la kuidhoofisha nguvu ya CAG.

CAG alicho kifanya ni kutoa mapendekezo sio kutoa hukumu, hata Bunge litaijadili ripoti na kutoa mapendekezo kwa Serikali tu.

Kwa maoni ya wananchi walio wengi wanategemea hatua zichukuliwe kwa Yale mambo ambayo Yako wazi hakuna haja kusubiria Kamati za Bunge, maana hata hizo Kamati haziwezi kutoa hukumu zaidi ya kutoa mapendekezo kwa Serikali.
 
Yuko sahihi kwa 100%. Wabunge wengi hawajielewi. Inashangaza kwenye kikao cha bajeti kuzungumzia yasiyohusiana. Bunge la bajeti lakini kila akisimama mbunge atazungumzia ripoti ya CAG na Ushoga. Tanzania tumepata bahati ya kupata spika kijana na msomi.
 
hili bunge la sasa ni hasara tu kwa Taifa. Hivi Kuna lipi wanawezasema wamelisimamia so far? Hamna namna linaweza kuvunjwa kwanza ? hii hasara CAG hajaiona mpka mimi mwanachi naiona?
 
Serikali, bunge na mahakama vimetekwa na mafisadi. Ukweli ni kubwa kila uchaguzi unapokaribia lazima CCM ipige hela ya kutosha kwa ajili ya chaguzi mbalimbali. Ukifuatilia vizuri utakuta sehemu ya mgao wa ufisadi mkubwa huingia katika mfuko wa CCM, nina uzoefu na hilo
 
Kanuni zinamruhusu Spika kupangia ratiba taarifa ya CAG baada ya kuwa imeshakabidhiwa Bungeni?
Huu uzwazwa una malengo gani hasa?
Mkuu huu taratibu na kanuni za bunge za kujadili hii report ya CAG ni mfumo unao toa mwanya wa wahusika wa ubadilifu kujipanga kwa kuhalalisha ufisadi uliojitokeza. Nadhani muda umefika wa kuwa na utaratibu ambao utaleta tija na mafisadi kuuogopa.
 
HATA MKITAKA KUACHA KUIJADILI HAINA SHIDA PIGENI PESA ZA WANYONGE
 
Safi, amefuata sheria, watanzania wana mihemko sana, kukurupuka ndio jadi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…