Dkt. Vicencia Shule: Ubora wa filamu ya Royal tour ni wa kiwango cha chini. Hata vijana wa bongo movie wangeweza kuitengeneza

Dkt. Vicencia Shule: Ubora wa filamu ya Royal tour ni wa kiwango cha chini. Hata vijana wa bongo movie wangeweza kuitengeneza

Hapa inatakiwa ubishe kwa facts sio kila kinachowekwa Hollywood ni bora kuliko vyote. Dokta anasema ubora wake sio mkubwa kulinganisha na ubora wa filamu zinginde za nyakati hizi. Mfano hata filamu za anold , Rambo na Van damme zilikuwa bora kwa wakati wake na zikaoneshwa Hollywood lakini ukiziangalia leo ni low quality

Kwa gharama gani? Kagoogle hiyo filam/ movie iligharim bei gani?
 
Utalii umekuwa ukijipromote wenyewe watu wanaijua serengeti,ngorongoro na kila kitu msianze kule uongo
Toyota inajulikana ulimwenguni kote lakini bado matangazo yake hayakomi.
•Kuna baadhi ya watu wanakamasi vichwani. Absolutely!
 
Acha uongo bilion 9 hazitoshi usemayo hata kidogo,suala unaloongelea lingehitaji bl. 200 na kuendelea!
N.b,bil 2 unajenga jengo la ghorofa 8.
Kwhy bilion200 kwny royo tua tu....wewe utakuwa umekulia Ikulu...
 
Dk. Kazungumza kiujumla sana! Ubora ktk eneo gani? Na akilinganisha na ubora upi uliojuu kwa hizo gharama. Pia, ni muhimu kuchambua aina za filamu.

Kwa mfano, ukiangalia ktk drama zipo za aina nyingi zenye maudhui, muundo, picha, wahusika na aina ya maneno tofauti tofauti, kama MELO- DRAMA ( za mapenzi kama ile ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe) huwezi kuilinganisha na HISTORICAL DRAMA (Kama Ya TheTrial of Dedan Kimath). Ukija kwa filamu ya The Royal Tour; location, wahusika,muundo na maudhui ni tofauti kabisa na zile filamu tulizozoea. Sasa mtu akisema ubora uko chini anamaanisha nini? Mchanganyiko wa rangi, maudhui, wahusika, picha au nini? #The Royal Tour itasaidia nchi tuache maneno mengi.🙏🙏🙏
Kakaaaa acheni basi kuwa PRAISE POWER mpaka aibu.... Kuna documentary nyingi tu zipo SAFARI CHANNEL Zina ubora kuliko huo wa RT ..... Na nnamini Zina gharama ndogo kuliko huu upuuzi
 
Kimsingi trela huwa vinachaguliwa vipande Bora na venye mvuto Sasa kwa zile trela nitaongea TU hata kama sauti haitasikika hapa Dr yuko sahihi na kama hela haijalipwa yote basi pafanyike mabadiliko kiwango ni Cha kawaida mno
 
Naona Umeishiwa point..anyway next time usijifanye mjuaji while kichwani ni mweupe.
JF is a home of Greak Thinkers sio watu wa hoja nyepesi nyepesi km zako za nigerian movie haziuzwi amazon.
I bet hujui tofauti ya amazon na movies distribution company or hujui Hollywood ni nn unakurupuka tu.
By theway Director ni John Feist. Ss ka mgoogle uone zaidi ya filamu za dizaini ya Royal tour ni filamu gani zaidi ka direct na ana umaarufu kiasi gani.

Unataka vitu vizuri kwa dola 3.8million, are serious!?
Ni kupoteza muda kulinganisha hiyo na filam/ documentary zingine zenye gharama kubwa! Tuna uwezo wa kununua magari used, halafu eti ujifananishe na magari mapya ya Ulaya, itawezekana? Huku ni kujitia upofu huku ukweli unafahamika
 
Unataka vitu vizuri kwa dola 3.8million, are you serious!?
Ni kupoteza muda kulinganisha hiyo na filam/ documentary zingine zenye gharama kubwa! Tuna uwezo wa kununua magari used, halafu eti ujifananishe na magari mapya ya Ulaya, itawezekana? Huku ni kujitia upofu huku ukweli unafahamika
 
ni apo utakaposikia alijiteka na akawa anajitekenya mwenyewe
 
Wanaharakati, chadema ni watu wa hovyo, wao kila kitu wanarukia tu
 
Kakaaaa acheni basi kuwa PRAISE POWER mpaka aibu.... Kuna documentary nyingi tu zipo SAFARI CHANNEL Zina ubora kuliko huo wa RT ..... Na nnamini Zina gharama ndogo kuliko huu upuuzi
ELEWENI VICHWA KAMASI;-
•Gharama ya 7bil,inajumuisha kila kitu fedha ambazo sio za serekali,ni wadau wa sekta wamechangia Mimi nikiwemo,gharama hizi zimebeba,utengenezaji filamu,kuitangaza,kutangaza utalii,kutangaza uwekezaji,kuvutia wawekezaji,Ku launch filamu,kukodi kumbi,na mengi kweli.
FAIDA;-
•Tayari makampuni ya uwekezaji yanakuja nabuwekezaji wa 11Trilion,Ambayo yataajiri vijana 300,000.
::THAT WAS 2 IN 1 TOUR,NI ZIARA NA LAUNCH ILIYOKUWA NA MAMBO MENGI NDANI YAKE.
 
Kwanza naunga mkono hoja ya Dr Vicensia Shule who has a B.A in fine and Performing Arts and Masters of Arts in Performing arts and also a lecturer who teaches theatre,film,media criticism and communication development.

Kwa wasifu huo ni mbobezi wa mambo ya filamu japokuwa ni social activists haswa kwa maoni yake dhidi ya utawala wa ccm kule twitter mpaka kupewa jina la Shangazi akijumuishwa na Maria, Fatuma na Aikande.

Ile filamu Nadhani ni proposal ya watu fulani wa ndani wakimjumuisha na Peter hivyo haikuwezekana pesa watoe watu fulani halafu filamu itengenezwe na wazawa wenye kiwango cha juu.
Ameshafanya documentary gani yeye I'll tulinganishe?
 
Hapo mlimani pana shida Nyingi basi....
Ikiwemo hii
Hawasaidie [emoji777]
Awasaidie[emoji736]
Napendekeza tutatue hili kwanza, Hoja inapungua makali kama itaandikwa vibaya.
Halafu siku za hivi karibuni uandishi wa namna hiyo umeshamiri sana. Najiuliza maswali wanaoandika hivyo wametoa wapi hiyo lugha? Shule zipi zinafundisha hivyo? Utakuta mtu anaandika:

awana badala ya hawana
Hawakubalie badala ya awakubalie
Hawaone badala ya awaone
awaongei badala ya hawaongei

Yaani panapostahili 'H' haiwekwi badala yake wanakuja kuiweka isipostahili na bahati mbaya hata ukimuelekeza sio rahisi kukuelewa
 
Hapo hata kushika kamera hajui,anadhani kutengeneza filamu ni Kama kunyoa sehemu za siri
Sawa nimekusikia, swali kwako, huyo mlengwa unamfahamu ni nani? Na fani yake ni nini?
Watanzania huwa hatuna utamaduni wa kuijadili filamu ili kuona ubora wake, na hilo ndilo linaloitesa Bongo muvi. Kwenye fani ya filamu picha ikitengenezwa lazima ijadiliwe ili kuona kama imetimiza ubora unaotakiwa.
 
Back
Top Bottom